VIDEO: Mbunge Charles Mwijage (CCM) apigwa mawe, mkutano wake wavunjika

Mkuu unachoona kwenye video ni trela tu, picha lenyewe mwombe Mathias aandike asiweke video... Alikuwa eneo la tukio


Mkuu kabla ya haya kutokea kuna mtu toka maeneo hayo aliniambia kuwa baada ya kuwa mbunge alishauri kisiwa kimoja kilichopo Muleba Kaskazini kihamishiwe Mwanza. Wananchi hawakuridhika na hili. Hii issue nao imeandikwa na gazeti la Mtanzania leo.

Mbunge azomewa mkutanoni Muleba

Na Arodia Peter

MBUNGE wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage, ameanza kuonja shubiri ya kisiasa baada ya kuzomewa na kurushiwa mawe akiwa kwenye mkutano wa hadhara juzi jioni katika Mji mdogo wa Izigo ulioko Kata ya Izigo wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera. Shuhuda wa tukio hilo, aliliambia MTANZANIA kwa njia ya simu jana, kwamba vurugu hizo zilianza wakati Mwijage alipowasili katika eneo hilo ambapo alipokewa kwa mabango mbalimbali yaliyokuwa na maneno ya kutorodhishwa na uongozi wake.

Pamoja na hayo, shuhuda wetu alisema vurugu hizo zilichagizwa na risala ya wananchi waliyoiandaa kwa ajili ya mbunge huyo ambapo alishutumiwa kwa hatua yake ya kukataa kuwa na Katibu katika ofisi yake ya ubunge iliyopo eneo hilo la Izigo. Shutuma nyingine ni hatua ya mbunge huyo kupendekeza katika vikao vya wilaya kuwa Kisiwa cha Goziba kiondolewe Muleba Kaskazini na kupelekwa Mwanza jambo ambalo linapingwa na wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa litapunguza mapato ya wilaya yao kwa kuwa kisiwa hicho kina wavuvi na samaki wengi.

Alipozungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mwijage alikiri kuzomewa na kurushiwa mawe na wapiga kura wake ingawa alisema tukio hilo lilitokea kwa kuwa baadhi ya wananchi hawaelewi vipaumbele vyake. "Pamoja na mkutano wangu kuvurugwa, bado nitaendelea na mipango yangu ya kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi kwa kuanzisha Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) pamoja na ufugaji wa nyuki na samaki.

Kutokana na vurugu hizo, taarifa kutoka Muleba zinasema kuwa, kilichomtokea mbunge huyo ni matokeo ya mgawanyiko wa Chama Cha Mapinduzi na makovu ya uchaguzi mkuu uliopita kwenye kura za maoni. Taarifa hizo zinasema kuwa kitendo cha Mwijage kukataa kutumia ofisi ya mtangulizi wake, Ruth Msafiri, kimetafasiriwa vibaya na kimekuwa ni kichocheo cha wananchi kugawanyika na kuwa makundi mawili.

Mbunge azomewa mkutanoni Muleba
 
Siku akirushiwa mawe bosi wake dah ntafanya sherehe maana huku kwetu kamachumu hawataki hata kumsikia
 
Hapa ndio pa kujifunza kwa wale wengine ambao bado hawajakumbwa na masaibu haya!
 
Tatizo hapa ni mgawanyiko ndania CCM si mbunge kushindwa kazi. Hapo Izigo ndipo anapotoka mtangulizi wake, Ruth Msafiri. Kwa hiyo msafiri aliweka ofisi yake hapo nyumbani kwao. Kumbuka hapo si wilayani Muleba ambapo tungetarajia ofisi yz mbunge iwe. Huyu mwijage kwake ni Kata na tarafa nyingine ya Kamachumu. Kwa jiografia ya maeneo hayo ilivyo, si rahisi kwake kutumia ofisi iliyopo Izigo, jambo ambalo wananchi wa eneo hilo wanataka na walizoe wakati wa Msafiri.

Pili katika siasa za pale, wanahisia kuwa Wilaya ya Muleba inaweza kuhawanywa, kupata wilaya mpya, hivyo wanataka ofisi ya mbunge iwe sehemu ya vigezo na ushawishi wa kuvuta makao makuu ya wilaya hiyo kuwa Igizo, hili lina ubishi na ushindani mkubwa na wakazi wa Kamachumu amnao wanataka Mji wa Kamachumu uwe ndio makao makuu, na pengine jina la wilaya hiyo mpya. Otherwise mbunge alishinda kihalali, hizo siasa ndo zimeibua vurugu hizo.

Nawasilisha
 
Wabunge waliofikiri bunge ni kijiwe cha wastaafu hawana jipya kwa wananchi.mawe ni stahili yao.AKOME.
 
Wabunge waliofikiri bunge ni kijiwe cha wastaafu hawana jipya kwa wananchi.mawe ni stahili yao.AKOME.

Huyu naye amejitakia. Makamba alishawakataza tangu mwaka jana wasikubali kujibu maswali ya wananchi zaidi ya kuwahutubia tu. Halafu tangu lini wabunge wa ccm wanakutana na wananchi kusikiliza kero?

Kajitakia mwenyewe kuiga tamaduni za Chadema. Majimbo mengine Kama wananchi hawana mawe ya kutosha waniambie nitapeleka kokoto fuso nzima
 
Wale wanaotoka mapovu mdomono mfano wa malaria sugu kwa kuishadidia ccm mbona hawaonekani kwenye topic hii?
Jamani karibuni mchangie.....tunataka kusikia maoni yenu. Lol ccm? acha niiteme mate....twuuuuh
 
Wale wanaotoka mapovu mdomono mfano wa malaria sugu kwa kuishadidia ccm mbona hawaonekani kwenye topic hii?
Jamani karibuni mchangie.....tunataka kusikia maoni yenu. Lol ccm? acha niiteme mate....twuuuuh

Yuko wapi JiniasBrein mkereketwa halisi pasipo kujali maslahi ya nchi?
 
Kweli watanzania wamebadilika, viongozi kuweni makini, hivi mpaka lini mtaambiwa msome alama za nyakati, heko wana Muleba, wamezidi blaa blaa hao wabungwe wa chama cha magamba

hawa jamaa sijui kwa nini wanakuwa wagumu kuelewa, hapo penye red ndicho hasa wanatakiwa kutambua, wananchi wamechoshwa na chama cha magamba chenye ahadi lukuki zisizo na utekelezaji, haya sasa mmeanza kuumbuliwa, bado kidogo mtarushiwa mawe na kutokuwa na wa kupoteza muda wake kuwasikiliza, hivi mbunge unawezage kusema ofisi itumike kama bweni??? tafakari....
 
Kweli watanzania wamebadilika, viongozi kuweni makini, hivi mpaka lini mtaambiwa msome alama za nyakati, heko wana Muleba, wamezidi blaa blaa hao wabungwe wa chama cha magamba

hawa jamaa sijui kwa nini wanakuwa wagumu kuelewa, hapo penye red ndicho hasa wanatakiwa kutambua, wananchi wamechoshwa na chama cha magamba chenye ahadi lukuki zisizo na utekelezaji, haya sasa mmeanza kuumbuliwa, bado kidogo mtarushiwa mawe na kutokuwa na wa kupoteza muda wake kuwasikiliza, hivi mbunge unawezaje kusema ofisi itumike kama bweni??? tafakari....
 
kweli wananchi wameisha ichoka ccm yaani miezi kadhaa tu toka uchaguzi upite tayari mbunge ameisha anza kupigwa mawe?
 
Hii inatakiwa iwe Tanzania nzima wote wasio waaminifu wanang'olewa kwa nguvu ya umma
 
wako kwenye sherehe ya kuchaguliwa wamewasahau wananchi, migomba inakauka hakuna utafiti wala ufuatiliaji hii ndio adhabu yao
 
Back
Top Bottom