VIDEO: Mbunge Charles Mwijage (CCM) apigwa mawe, mkutano wake wavunjika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO: Mbunge Charles Mwijage (CCM) apigwa mawe, mkutano wake wavunjika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mathias Byabato, May 6, 2011.

 1. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Sikiliza, tazama mwenyewe kwenye hii video

  Angalizo kuna baadhi ya picha (Scene) kwa yaliyotokea pale siwezi kuzionesha kwenye TV au hii Youtube yenye ID ya jina langu kwa sababu maalum ikiwemo heshima ya mbunge huyo nk

  Atakayezitaka ani-PM nimtumie

  M.B


  [​IMG]

  Story nzima ipo hapa: http://www.fikrapevu.com/habari/mbunge-apigwa-mawe-na-wananchi-akiwa-mkutanoni

  ===================
  Story Kutoka FikraPevu:

  MBUNGE wa Muleba Kasikazini (CCM) Charles Mwijage juzi alijikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa mawe na wananchi katika mkutano wa hadhara akidaiwa kuikimbia ofisi na kupindisha maamuzi ya vikao.

  Hali hiyo ilitokea katika eneo la Izigo ambapo aliposimama kuhutubia wananchi walioonekana kuwa na jazba walianza kutawanyika huku mawe yakivurumishwa kuelekea jukwaani.

  Miongoni mwa malalamiko ya wananchi ni kuisusia ofisi iliyoachwa na Ruth Msafiri na kukosa sehemu ya kupeleka kero zao,na kudaiwa kupinga eneo hilo kuwa makao makuu ya Wilaya ya Kamachumu ambayo mapendekezo yako katika hatua mbalimbali.


  Katika hali iliyoonekana kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya chama kabla ya kurushwa mawe wenyeviti wa vijiji ambao wanatokana na chama hicho waliwaongoza wananchi kumsusia mbunge wao.

  Wenyeviti hao walidai wao ndiyo walitumika kuwashawishi wananchi ili apate kura na kuwa hivi sasa wanashangaa kwa kuonekana kuanza kuwasaliti kwa kile alichodai kuwa hata bado hakujapambazuka.

  "Tunataka uitambue na kuitumia ofisi ya mbunge iliyojengwa hapa Izigo, tunataka uendeleze maamuzi mema ya watangulizi wako lakini tumeanza kupoteza imani hata kabla hakujapambazuka"alisema George Merkiory Mwenyekiti wa kijiji cha Itoju kabla mkutano huo haujavurugika.

  Pia Mwenyekiti huyo alimweleza Mwijage kuwa wananchi walianza kumtilia shaka pale alipodaiwa kutamka kuwa ofisi ya mbunge wa zamani itumike kwa matumizi mengine na yeye hayuko tayari kuitumia.

  Fikrapevu ilipomtafuta mbunge huyo kwa njia ya simu ili kujua kama amepeleka malalamiko polisi baada ya kupigwa mawe mkutanoni simu yake iliita mara kadhaa bila kupokelewa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Huyo ni mbunge mkoa gani na wa wilaya gani hapa Tanzania?
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kweli watanzania wamebadilika, viongozi kuweni makini, hivi mpaka lini mtaambiwa msome alama za nyakati, heko wana Muleba, wamezidi blaa blaa hao wabungwe wa chama cha magamba
   
 4. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  video aifunguki mkuu.

  labda kwangu tu?
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda inaweza kuwa tatizo la kompyuta yangu, lakini kwa hakika hiyo video wala siioni
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimeipenda hii clip - Pamoja na kwamba hiyo ndiyo mitaa ya nyumbani kwetu, nimefurahishwa sana na MASWALI yaliyoelekezwa kwa Charles Mwijage (MB) - Wananchi wamechoka na wanataka suluhisho la matatizo yao ... basi .. siyo ulaghai..

  Charles anasema "... nitakuwa nawafuata wananchi huko waliko kutatua matatizo yao ..." - Shame on him!
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Jimbo la Muleba Kasikazini - Mkoa wa Kagera
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
 9. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Muleba Kaskazini
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Bofya hapa chini:-

  YouTube - Byabato1's Channel
   
 11. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Safi sana wananchi. hiyo ni haki yenu
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Duuh kwa kweli siku hizi ukitaka kugombea uongozi lazima ujijue utaweza vingievyo utatandikwa viboko hadi ukome,Pole mheshimiwa mbunge sikunyingine chunga kauli yako
   
 13. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dah, wananchi wana hasira hadi wanataka kumvua gamba mbunge wao live, tena kwa kulilegeza kwanza kwa kumtwanga mawe? Jamani waheshiniwa wabunge, hakikisheni mnawatumikia wananchi maana wa leo sio wa wakati uleee wa zidumu fikra za mbunge hata kama ni potofu
   
 14. escober

  escober JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  he deserves it
   
 15. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Picha imeonekana ila hujatoa details na hasa kichapo alichopata.
   
 16. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli sasa watanzania tumeamka hakuna tena kudanganywa, toka lini ofisi ikawa bweni??
   
 17. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 18. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  MS umeiona hii?
   
 19. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Huyu walimwibia Kura Watu wa Magamba, Atajuta kwa nini alikubali!! Inabidi magamba wajue Chagua la wananchi ni chaguo la Mungu
   
 20. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #20
  May 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hapa kuna kila dalili kwamba mbunge huyu alipata hiyo nafasi kwa kuchakachua kura na wala hakushinda kihalali na ndio maana the so called wapiga kura wake hawamuheshimu wala kumuona kama kiongozi wao.

  Itafika mahali wabunge wataogopa kwenda majimboni kwao!!!!

  Tiba
   
Loading...