Video: Mazishi ya Sheikh Mgaza katika makaburi ya Kisutu leo

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Salaam,

Hii video inayoonekana, Mazishi ya sheikh Mgaza kisutu leo.

KLABU ya Simba imepata pigo lingine leo Alhamisi baada ya kuondokewa na mwanachama wao na Haji Mgwaza aliyefarikia katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema Marehemu Mgaza ni mwanachama wa muda mrefu pia alikuwa alihusika kufanya dua wakati wa shughuli mbalimbali za klabu hiyo ikiwemo ufunguzi wa Uwanja wao uliopo Bunju miezi minne iliyopita.

Manara amesema anamkumbuka Mgwaza kipindi cha mwaka 1991 alipowafuata vijana mtaani kwao Kariakoo na kuwataka waende wakasome dua kwaajili ya mchezo wa Simba na Yanga.

"Alikuja mtaani na kutuchukua vijana kama watano, tunajuana vijana wa Simba pale mtaani kwahiyo tukaenda na kuanza kupiga dua kwa siku tatu mfululizo,".

"Tukiwa tunapiga dua pale huyu Mgwaza alikuwa na rafiki yake anavisenti kwahiyo kila tukitoka kwenye dua alikuwa anatupa shilingi 300 ndani ya siku tatu nilikuwa na 900 na ndipo nikaenda kufungua akaunti posta kwa shilingi 500,".

Aliongeza kwa kusema "Baada ya dua hiyo Simba ilifungwa 2-0 magoli yaliyofungwa na Athuman China na Abubakari Salum sisahau hilo tukio mpaka leo, huyu ni Simba kwelikweli,".

Mgaza ameihudumia timu hiyo kwa takribani miaka 20 tangu timu hiyo ikiwa chini ya Hassani Dalali akiwa Mwenyekiti mpaka leo hii umauti unamkuta.
 
Back
Top Bottom