Video: Maxence Melo awashukuru wote walioshiriki na hana tatizo na yeyote

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,151
2,000
Habari wakuu,

Baada ya kutoka mahakamani na kisha kwenye press ya Maxence Melo nimejaribu kutafuta video mtandaoni na nimepata hii japo kuna baadhi ya vitu muhimu nilivyosikia havimo. Nimepata na maelezo na kuyarekebisha kidogo.
=======

Baada ya kuachiwa leo kwa dhamana Mkurugenzi wa JamiiForums amesema mtandao wa JamiiForums haujatetereka na bado uko ngangari na amewataka watumiaji wote wa mtandao huo waondoe hofu kwa kuwa taarifa zao za siri ziko salama.

Pia amesema hana ugomvi wowote na vyombo vya dola na ana imani na mahakama za Tanzania kuwa zitamtendea haki katika kesi yake.

Ameishukuru jamii ya mitandao ikiwemo Twitter, JamiiForums na nyinginezo kwa mijadala mingi iliyotaka aachiwe huru na kutendewa haki pia amewashukuru mawakili wake.

Amewataka wananchi wote bila kujali itikadi zao waendelee kupigania uhuru wa kusema na kutoa maoni, pia amevishukuru vyombo vyote vya habari na wanahabari kwa kumuunga mkono kipindi chote alipokuwa mahabusu.

Maxence amesema kazi ya kuulinda uhuru wa vyombo vya habari sio ya Max na yeye katolewa kama mfano tu, wakati mwingine anaweza akawa yeyote hivyo kwa pamoja tuulinde uhuru wa kujieleza na kulinda watoa taarifa kwa namna yeyote inavyowezekana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom