Video: Mawakili waishangaa Polisi kwa Lissu na dereva wake kutohojiwa; wadai wanaweza kuhojiwa hata kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano


mmh

mmh

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
1,456
Likes
1,563
Points
280
mmh

mmh

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
1,456 1,563 280
nyie muliomsukuma Mbowe nyuma ya Nondo ndio munahangaika yeye anakomboa taifa hajajifunza kunya kwenye vyoo vya kuvuta ukubwan amezaliwa anaogelea raha lakini he has devoted his life to serve this nattion hangaika wewe unayedhani itambadirisha kitu mshamba wa karomije chakula cha watu mpuuzi mkubwa hivi GSM wameacha kukulegeza
Inaonesha umezaliwa miaka ya 2000 wewe asee, kwanza nijibu unijua y2k?
 
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
892
Likes
779
Points
180
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
892 779 180
Wauaji wanazidi kuumbuka ,kwepakwepa nyingi ,uongo mwingi , penye ukweli uongo hujitenga .
 
JUAN MANUEL

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Messages
1,283
Likes
1,319
Points
280
JUAN MANUEL

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2010
1,283 1,319 280
Sijawahi ona au sikia mtu anahojiwa kienyeji namna hii.
Umapomuhoji mtu, physical presence, kuongea nae face to face na kumsikia hata anavyovuta pumzi ni muhimu zaidi. Kwenye video conference au njia nyingine hupati true coorperation.
Wewe upo dunia gani?unaweza kuhojiwa ana kwa ana,na ukadanganya,ujawahi sikia watu wanaoweza kuidanganya hats POLLYGRAPH,?!!
Iwe Karibu au mbali,tekinolojia inawezesha makachero kutambua ukweli na uongo!!
Hatuko mwaka 47!!!
Maofisa wa ubalozi ubeligiji,walimtembelea Lisu Hospitali,kwanini hakukaribishwa ubalozini ahojiwe?akiiingia tu ubalozini,ni sawa kama yupo hapa nyumbani!
Hawataki kuhoji,kwa sababu vijana mliowatuma,waliburunda kazi waliyopewa,hawakuwa professionals,
Eti utasikia Mfanyabiashara kawapiga risasi maofisa wa TISS!kweli?!!ofisa wa TISS anapigwaje risasi na RAIA?mnatuma maofisa saba kumkamata MTU mmoja!!!tena mchana,wanashindwa,wanaokolewa na polisi!!
Haya ni mazwazwa yaliyopewa ajira kindugu tu,hayajuhi chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
G

Gellangi

Member
Joined
Apr 11, 2016
Messages
41
Likes
31
Points
25
G

Gellangi

Member
Joined Apr 11, 2016
41 31 25
hakuna haraka atahojiwa uso kwa uso akiwa na pingu
Pingu za nini tena?Yeye ndiye mhalifu?
Wewe ni kati ya wanaoamini kuwa alijishambulia au chama chake kilimshambulia?Tuwe waungwana kwa kutokupotosha mambo kwa kutoa hoja na utetezi wa ovyo jinsi huu.
 
M

Msororo69

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2016
Messages
2,532
Likes
816
Points
280
M

Msororo69

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2016
2,532 816 280

Baadhi ya wanasheria wameshangazwa na Jeshi la Polisi kushindwa kumhoji mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na dereva wake.

Wamesema sheria na utaratibu wa jeshi hilo unaliwezesha kuendelea na uchunguzi hata kama mbunge huyo yuko nje ya nchi.

Wakizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Februari 11, 2019 baadhi ya wanasheria wametaja sheria zinazowezesha Jeshi la Polisi kumhoji mtuhumiwa au mtu yeyote wa tukio la jinai akiwa popote duniani.

Ijumaa iliyopita Februari 8, 2019 Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alilieleza Bunge kuwa kesi ya kushambuliwa kwa risasi Lissu imeshindwa kuendelea kutokana na mbunge huyo pamoja na dereva wake kushindwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwani wao ndio mashuhuda muhimu wa tukio hilo.

Lugola alisema hayo alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakichangia taarifa ya kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

Lugola alisema siku ya tukio hilo Septemba 7, 2017 ndani ya gari, Lissu alikuwa na dereva wake ambao ni mashuhuda muhimu katika kesi hiyo.
Lissu alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 mchana wa Septemba 7, 2017 katika makazi yake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria vikao bungeni ambapo kwa sasa ametoka hospitali na anaendelea na ziara barani Ulaya na Marekani.

Lissu amekuwa akihoji sababu ya Jeshi la Polisi kutomhoji tangu alipokuwa Nairobi, Kenya, huku pia akishangazwa na hatua hiyo, akisema kama angefariki dunia polisi wangefanya nini.

Mwanasheria wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Paul Mikongoti ameitaja Sheria ya Kusaidiana kwenye mambo ya jinai (Mutual assistance in criminal matters) akisema ndiyo inayoliongoza Jeshi la Polisi kwenda kuhoji wahalifu au waathirika wa matukio ya jinai wakiwa nje ya nchi.

“Sheria zipo zinazoliwezesha Jeshi la Polisi kumhoji Lissu. Hata wao Polisi wenyewe wanaweza kwenda kwa kushirikiana na majeshi ya Polisi kama ya Kenya au Ubeligiji au mtandao wa Polisi wa kimataifa (Interpol),” amesema Mikongoti.

Amesema Serikali inaweza kutumia ofisi za ubalozi kumhoji Lissu na dereva wake tangu alipokuwa nchini Kenya na Ubeligiji.

“Tuna ubalozi Kenya, tuna ubalozi Ubeligiji wangeweza kutuma maofisa wao kwenda kumhoji. Sijui kwa nini hawajamhoji, wao wenyewe wanajua, lakini kuna sheria inayoitwa Mutual assistance in criminal matters, inayotoa mwongozo wa kwenda kuhoji watu kama hao,” amesema.

Mmoja wa mawakili ambaye hakutaka jina lake kuwekwa wazi amesema Jeshi la Polisi halina sababu ya msingi la kushindwa kumhoji Lissu popote alipo duniani.

“Issue (suala) si sheria, Jeshi la Polisi linapotakiwa kumhoji mtu, kama nje ya nchi na hasa alipokuwa Kenya alipopata fahamu wangekwemda kumhoji. Kwa hiyo wanaweza kumhoji mahali popote hakuna kitu chochote kinachozuia kwenda kumhoji,” alisema wakili huyo.

“Hata kama mtu ni shahidi muhimu na yuko nje ya nchi na imekuwa ngumu kumleta, Jeshi la Polisi linakwenda kumhoji. Sioni kama ni defence kwamba hajahojiwa,” amesema.

Amesema Jeshi la Polisi katika upelelezi linaweza kwenda popote, hata kama ni Marekani.

“Ni ngumu kutetea kwamba Jeshi la Polisi limeshindwa kuendelea na upelelezi kwa sababu halikwenda kumhoji, haiingii akilini,” alisisitiza wakili huyo.

Wakili mwingine kwa sharti la kutotajwa jina amesema pia ameitaja sheria hiyo ya kusaidiana katika masuala ya jinai.

“Kifungu cha 14(1)(b)(ii) kinaeleza bayana, unapokuwa Tanzania kuna uchunguzi wa jinai unafanyika, halafu kuna mtu mwenye ushahidi muhimu lakini hayupo Tanzania, Mwanasheria mkuu akiona ushahidi muhimu anachukua mamlaka ya kuwasiliana na nchi nyingine ili wachukue ushahidi kule aliko mtu,” amesema wakili huyo.

“Iwe Kenya iwe Ubelgiji, yaani kwa hali ya kawaida, mgonjwa alazwe Uingereza halafu muache kuchunguza ugaidi?” Alihoji.

Ametaja pia mabadiliko ya sheria ya ushahidi ya 2017 yalifanyika ili kuendana na kasi ya teknolojia akisema mtuhumiwa au mwathirika anaweza kuhojiwa popote alipo duniani kwa njia za mawasiliano ya elektroniki.

“Mabadiliko hayo yaliyotanguliwa na mahakama za juu nchini, Polisi wanaweza kuhoji mtu akiwa nje ya nchi. Wewe ni askari wa upelelezi unaweza kuyarekodi maelezo yenu kwa njia ya video, si unamwona kule kule anatoa ushahidi? Kwa nini ishindikane kumhoji mtu aliye Nairobi au Ubeligiji?” Amehoji.

Amesema njia ya tatu ya kutuma watu alipo mwathirika wa tukio ili kumhoji akisema pia inawezekana.

“Haiwezekani maisha yakasimama 2019 eti kwa sababu mtu hayupo nchini,” amesisitiza.
     
Mbona hao ndio walimwambia lisu uwepo wa hiyo sheria. Hao mawakili wanatoka kwenye kampuni tanzu ya chadema hivyo mawazo yao yanafanana.
Dereva hakuumia polisi ilipomuhitaji kuja kuisaidia kwa kutoa maelezo.
Nani asiyekumbuka mahojiano ya msigwa na lema huko Kenya kuwa dereva hawezi kwenda kuhojiwa na polisi kwani angeteswa.
Sheria hiyo ilitungwa kuisaidia polisi kufanya kazi. Hakuna mazingira ya kumzuia dereva kuja kuandika maelezo. Kwa kuweka masharti hayo ni sawa na kugoma kushirikiana na jeshi la polisi. Kwakuwa aliyetendewa ndiye hataki kuhudumiwa polisi haiwezi kulazimisha. Kama kungekuwa na waathirika wengine zaidi yao hatua zote zingechukuliwa. Kwasasa ni kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi
 
Kajiru Kanyika

Kajiru Kanyika

Member
Joined
Nov 28, 2018
Messages
39
Likes
42
Points
25
Kajiru Kanyika

Kajiru Kanyika

Member
Joined Nov 28, 2018
39 42 25
Hii ni geresha yule mtu (dereva) alikuwepo maeneo yote
Area D kwenye tukio.
Hospitalini muda wote
Airport kusindikiza bosi wake. Sema police wamemkumbuka siku 2 baadaye tena akiwa ameshasafiri kwenda Kenya.

Nia ya kufanya upelelezi haukwepo, na ndiyo maana wiki mbili baadaye IGP alitoa taarifa, ya kufungwa jalada la upelelezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Walijua anakufa yaan hawakuwa na plan b
 
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,710
Likes
1,507
Points
280
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,710 1,507 280
Mnaamua kumtoa dereva na maelezo mpaka mtakapotaka nyinyi nasio polisi,mbona kipindikile cha nyuma mlikuwa hamji na hoja kama hizi? Mmejichelewesha mpaka ushahidi unaanza kupotea ndio mnakuja na usaka wenu, Acheni ulofa nyie chadema tumechoka na maigizo yenu ya futuhi.
 
Kajiru Kanyika

Kajiru Kanyika

Member
Joined
Nov 28, 2018
Messages
39
Likes
42
Points
25
Kajiru Kanyika

Kajiru Kanyika

Member
Joined Nov 28, 2018
39 42 25
Mnaamua kumtoa dereva na maelezo mpaka mtakapotaka nyinyi nasio polisi,mbona kipindikile cha nyuma mlikuwa hamji na hoja kama hizi? Mmejichelewesha mpaka ushahidi unaanza kupotea ndio mnakuja na usaka wenu, Acheni ulofa nyie chadema tumechoka na maigizo yenu ya futuhi.
Na polis watolee maelezo zile CCTV Camera ziliondelewa kihuni ili kuharibu ushahid
 
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,710
Likes
1,507
Points
280
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,710 1,507 280
hakuna haraka atahojiwa uso kwa uso akiwa na pingu
Uko sawa kabisa,maana ata wao chadema hawajawai kuwa na haraka ya upelelezi wa hii kesi,siku dereva akifika tz atahojiwa face to face.
 
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,710
Likes
1,507
Points
280
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,710 1,507 280
Kuku wako wako mwenyewe manati ya nini subiri.jioni ataingia bandani. Team ya polisi kwenda huko ni ghalama.haina haja maana kesi yenyewe haina uharaka tokana na walalamikaji wenyewe wanavyoipeleka kesi.
Sasa wanashindwa nini kwenda kuwahoji?

Kwanini hata Nairobi hamkwenda?

Na ni kwanini Polisi hawakumuhoji dereva wa Lissu pale hospitali ya mkoa wa Dodoma siku ile ya tukio?
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
14,378
Likes
14,159
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
14,378 14,159 280
Sasa wanashindwa nini kwenda kuwahoji?

Kwanini hata Nairobi hamkwenda?

Na ni kwanini Polisi hawakumuhoji dereva wa Lissu pale hospitali ya mkoa wa Dodoma siku ile ya tukio?
Kwa ni polisi waende ubelgiji? kwa nini Lisu na dereva wake wasije Tanzania kuhojiwa? Sasa hivi wote wazima Lisu na dereva waje wao Tanzania.Halafu Toka lini polisi wanapangiwa na mtu kuwa wamhoji wapi.Polisi ndio hupanga sio mtu kuwapangia
 
M

Mwananchi

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2012
Messages
2,385
Likes
1,134
Points
280
M

Mwananchi

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2012
2,385 1,134 280
Kwa nini mnamficha dereva na kafikaje belgium bila passport ya tz?
Wamefanya hivyo maana intelijensia ya Chadema ilionyesha kwamba kwa sababu ya nia hovu ya kutaka kumuua Lissu basi mkimpata dereva wake mtahakikisha mnafuta hapa duniani ili kufuta ushaidi. Dereva na Lissu wanajua wauaji na ndiyo maana Lissu anawambia ni swala la muda kila kitu kitakuwa wazi. Kwa hiyo mnang'ang'ania kuhoji physical ili mmtoe roho na kupoteza ushaidi. sasa hivi ni mkimbizi wa kisiasa na haji na ndiyo maana aliweza kusafiri kwa passport ya Ubelgiji maana nia hovu ilishajulikana
 
Francis mwaijulu

Francis mwaijulu

Member
Joined
Nov 4, 2018
Messages
17
Likes
10
Points
5
Francis mwaijulu

Francis mwaijulu

Member
Joined Nov 4, 2018
17 10 5
Write your repl
in short, wasiojulikana walikua na mtazamo wa upande mmoja tu wa kuua, kwahiyo walichojiandaa nacho inawezekana ilikua ni kuhudhulia mazishi sababu walikua hawajulikani. dereva anadai alikuwepo mpaka siku ya ij'maa kwanini hakukamatwa ili ahojiwe? mwacheni mungu aitwe mungu, pasipo haki mungu anapiga upofu, anagandisha akili.
 

Forum statistics

Threads 1,262,068
Members 485,449
Posts 30,112,312