Video: Mauaji ya kikatili Musoma (too graphical)

:confused:Such a barbaric & inhuman horrendous act!:mad:

Hata mimi nimetoa machozi. Wafiwa wote poleni sana.
Nina imani wananchi wakishirikiana na vyombo vya dola wataweza kuwapata hao waliofanya vitendo vya kinyama ambavyo haviwezi kuvumiliwa popote.

Huu ni msiba wa Manispaa ya Musoma na Taifa kwa ujumla.
 
Oh! so sad hawa jamaa ni wahalifu, wanatakiwa wanyongwe wote waliohusika
 
Poleni sana wafiwa jamni inasikitisha sana!
Chakushangaza mzee mzima huyoo anakula bata nchi za watu!
 
mzee mzima akitoka ubatani ataenda kuhani!...... kama alivyofanya kwenye vifo vya waliofunikwa na kifusi huko moshi. kule kwenye jimbo la mama Kilango.
 
Hivi serikali ya Tanzania haina 'killing machines' kama serikali ya Marekani? Killing machine wanafaa wapewe vitendea kazi kuwatafuta wauaji wa familia hiyo! Hao wauaji wa hiyo familia ni magaidi kwakweli. Hata wakinyongwa ni sawa tu! Potelea mbali.

Hawa wauaji waombe Mungu wadakwe na serikali kwanza ole wao wananchi wawamtie mikononi ni upanga kwa upanga tu. Damu ya hawa marehemu haitapotea bure, naungana na yule kiongozi Mungu yupo!
 
but why Musoma???

Ikiwezekana mkoa huu pekee ujiunge na East Africa!

tunawaone huruma ndio, tunalia pamoja jamani, lakini

mbona kama hizi tabia mmezifuga kwenu?
 
but why Musoma???
makabila karibu yote ya mkoa wa Mara kwao panga, rungu ni kitu cha kawaida. sisi tunashangaa mauaji hayo lakini wao utakuta wanaona sawa tu! si ajabu baada ya muda ukasikia tena wamechinjana!
 
Sasa wale watoto wadogo na wanyama KOSA lao nini!
Lazima hao wauaji watakua na matatizo ya AKILI,, na NDIO MAANA binaadamu ameandaliwa Jehanamu,,wanyama hawawezi kufanya mambo kama haya!
 
Poleni sana wafiwa jamni inasikitisha sana!
Chakushangaza mzee mzima huyoo anakula bata nchi za watu!
Tena kaenda kutunukiwa shahada ya uzamivu! lol, hata hajatuma salamu za pole kwa wahanga!
 
Hivi serikali ya Tanzania haina 'killing machines' kama serikali ya Marekani? Killing machine wanafaa wapewe vitendea kazi kuwatafuta wauaji wa familia hiyo! Hao wauaji wa hiyo familia ni magaidi kwakweli. Hata wakinyongwa ni sawa tu! Potelea mbali.

Wewe eeee!!!!!!!! Watakusikia wanaharakati wa haki za binaadam. Hivi adhabu ya kifo kwa nini ifutwe katika mazingira haya? Wanaopinga adhabu ya kifo sasa wapo kimyaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!
 
Hii ni Musoma zaidi ya tuijuavyo, kwa kweli inatisha sana watu kuwa wakatili kiasi hiki !!
 
Hii ni preamble tu ya EAC, subirini mambo bado. Nimesikia rais ana mambo mengine muhimu ya kufanya.
 
Mods weka hii thread kwenye siasa bana hii sio mambo ya habari mchanganyiko.
 
Kwahili nadhani wa kwanza kulaumu ni jamii ya watu wa maeneo hayo... wameishi na kuvumilia ukatili kwa muda mrefu na imekua kama kalcha yao.... tumeachia serikali kila kitu

halafu wa pili kwa lawama ni serikali, yaani imeshindwa kuwa na intelligency ya ku-detect such a huge crime?? lazma ilikuwa in the making for some time, mbona baada tu ya mauaji watu wameshajua nani kafanya??

security yetu ni ya kutia shaka hasa tunapoelekea uchaguzi, lakini sisi wanajamii huko makwetu tunalea wezi na maharamia wengi sana, achilia mbali mafisadi

Mkuu mimi nafikiri lawama zote ya mauaji yanatokea sehemu mbali za nchi yetu na hasa Musoma lawama ni za Serikali maana wao ndiyo wenye wajibu mkubwa wa kulinda mali na uhai wa Watanzania ndani ya mipaka yetu na miaka ya hivi karibuni Serikali hii imeshindwa kufanya hivyo na kuwapa nafasi kubwa wauaji wafanye wanachokitaka bila woga wowote ule. Hawa wananchi wa Musoma hawawezi kufanya lolote lile ili kujilinda labda kama na wao Serikali iwaruhusu waanze kuwaua wabaya wao kitu ambacho kitafanya hali iwe mbaya zaidi. Serikali hii imelala usingizi na ndiyo maana amani ndani katika baadhi ya mikoa inapotea taratibu.
 
Kwahuu unyama uliotokea musoma,ata Tanzania sio kisiwa cha amani kama tunavyo fikiri,haya mapanga ya musoma hayana tofauti yoyote na yale ya Rwanda kati ya wahutu na watusi,au yale ya Kenya kipindi kile cha uchanguzi,kwahiyo wote wana wa East Africa ni kuomba mungu sana kama alivyo sema mkuu wa mkoa....Kanali
 
Mkuu mimi nafikiri lawama zote ya mauaji yanatokea sehemu mbali za nchi yetu na hasa Musoma lawama ni za Serikali maana wao ndiyo wenye wajibu mkubwa wa kulinda mali na uhai wa Watanzania ndani ya mipaka yetu na miaka ya hivi karibuni Serikali hii imeshindwa kufanya hivyo na kuwapa nafasi kubwa wauaji wafanye wanachokitaka bila woga wowote ule. Hawa wananchi wa Musoma hawawezi kufanya lolote lile ili kujilinda labda kama na wao Serikali iwaruhusu waanze kuwaua wabaya wao kitu ambacho kitafanya hali iwe mbaya zaidi. Serikali hii imelala usingizi na ndiyo maana amani ndani katika baadhi ya mikoa inapotea taratibu.
inataka serilaki ianze utaratibu wa kulinda nyumba moja baada ya nyingine?
 
Hivi serikali ya Tanzania haina 'killing machines' kama serikali ya Marekani? Killing machine wanafaa wapewe vitendea kazi kuwatafuta wauaji wa familia hiyo! Hao wauaji wa hiyo familia ni magaidi kwakweli. Hata wakinyongwa ni sawa tu! Potelea mbali.

Unauliza majibu !!!!! Hivi wewe ni m-TZ kweli ?? Unalinganisha TZ na Marekani. Ajabu kweli. Wakati mwingine hao majambazi tunawalea wenyewe maana tunaishi nao, tunawafahamu vizuri ila woga wetu ndio utaendelea kutuponza. Jamani, serikali itakuwa kila mahali na kila kaya ??
 
Back
Top Bottom