VIDEO: Mahojiano na Mh. Zitto Kabwe katika Makutano Show

Safi sana Fina Mango nakukubali sana since day one ukianza mziki kwa kushirikiana na GK(Mama),pili kipindi chako kizuri kinabamba pia wekeni live stream kwenye website tuwe tunapata online(sometime tunakua nje ya nchi),keep doin JF luv ya'

•Fanyeni mpango mumlete Irene wa SSRA tumuulize maswali ya msingi.
Haswaa mkuu na mimi natamani huyo mgeni aje kwenye kipindi ili ajibu maswali yetu na siyo kujirecord na kutuwekea ujumbe km mahubiri ya Mchungaji yasiyotoa nafasi ya kuhojiwa.
 
Nitasikiliza jmosi. Ila naomba mfanye kama star tv. Uweke mada hapa mapema na kutujulisha mgeni utakayekuwanae ili tuanze kuuliza maswali yetu mapema. Ila hilo la kutaja id zetu, ngoja nimalizie ndovu ya pili nirudi!
 
Fina,

Siku ukiwapata hawa wafuatao nina maswali mengi sana kwao:-

Nape, January, Nchemba, Ndungai, Kilango, Lowassa, Magufuli, Membe, Rwakatare [mchungaji], Nyalandu, Mzee wa kusinzia, Mwakyembe na Sitta.

Opposition: - Baba mwenye nyumba Freeman, Mzee Cheyo, Nassari, Hamad, Mngodo, Sugu na Naomi.

Huko uraiani Tutafutie Rais wa Walimu, Dr Deo [Aliekuwa na Ulimboka siku ya utekaji], SSRA na jamaa wa TCRA wale wa kitengo cha analogia kwenda Digital]
 
Fina,

Vipi unaweza pia ukamjumuisha Kipanya katika kipindi? Manake nyie wawili mkiwa pamoja mnafanya kazi nzuri sana...rejea enzi zile mkiwa pamoja pale radioni.

Mkuu Masoud Kipanya yuko busy anaandaa kijiji cha Maisha Plus kwa sasa. Ila kiukweli kujitoa kwao Clouds kumewajengea heshima maana huko udaku umezidi. Najua sio vyema kuwasema wengine ila kule hapakuwa pa watu makini kama Fina na Kipanya.

I hope soon utakuwa live na wazee wako wenye uzalendo wakina Hamza Kasongo na Jenerali.
Huku tunaendelea na Fiesta Supa Nyota
 
Well come! Safi mwanzo mzuri. Vp maboss wako wamekuruhusu kutumia jf. Maana kuna watu wamefukuzwa kazi na kwa kukuta wanafungua jf. Wengine wameomba jf ifungiwe kisa imegusa vitumbua vyao!
 
Fina Mango unaonaje mwisho wa vipindi vyako vya ukawafahamisha wasikilizaji wa Magic FM '' maoni na majadiliano yanaendelea ktk JF''

Sababu muda wa kuchangia ktk majadiliano ndani ya vipindi kama cha TV/Redio live ni mchache sana.

Shukrani dada Fina Mango, maana ni jambo zuri kupata kila kitu bila chenga hapa JF nasi tukatoa mrejesho (feed-back) juu ya kila kitu kinachohusu Tanzania, maana wa-JF hatuwezi kuchangia moja kwa moja live ktk vipindi vya redio, tv n.k lakini humu ktk JF muda ni mkubwa wa kuchangia baada ya kipindi.
 
Fina,

Siku ukiwapata hawa wafuatao nina maswali mengi sana kwao:-

Nape, January, Nchemba, Ndungai, Kilango, Lowassa, Magufuli, Membe, Rwakatare [mchungaji], Nyalandu, Mzee wa kusinzia, Mwakyembe na Sitta.

Opposition: - Baba mwenye nyumba Freeman, Mzee Cheyo, Nassari, Hamad, Mngodo, Sugu na Naomi.

Huko uraiani Tutafutie Rais wa Walimu, Dr Deo [Aliekuwa na Ulimboka siku ya utekaji], SSRA na jamaa wa TCRA wale wa kitengo cha analogia kwenda Digital]

Fina, kama itifaki zitaruhusu, jitahidi umpate Mh. Othman wa TISS, IGP Mwema, Mansoor Himid (Waziri Zanzibar)
 
Aisee zitto vipi tena, basi vaa vizuri ndugu yangu,wewe ni mheshimiwa lakini naona umerudia vidudu vyako ulivyo kua ukivaa kigoma.
 
Fina Mango unaonaje ktk vipindi vyako vya TV ukatuwekea ktk tv-screen chini '' maoni na majadiliano yanaendelea ktk JF''

Sababu muda wa kuchangia ktk majadiliano ndani yavipindi kama chako cha TV/Redio live ni mchache sana.

Shukrani dada Fina Mango, maana ni jambo zuri kupata kila kitu bila chenga hapa JF nasi tukatoa mrejesho (feed-back) juu ya kila kitu kinachohusu Tanzania, maana wa-JF hatuwezi kuchangia moja kwa moja live ktk vipindi vya redio, tv n.k lakini humu ktk JF muda ni mkubwa wa kuchangia baada ya kipindi.

Kwa sasa ni redioni na maswali yanasomwa hewani lakini ikifikia hatua ya kwenda kwenye TV hapana shaka yatapita maswali/maoni yenu.
 
utafika mbali,hongera kwa kipindi kizuri.napenda sauti yako
 
Fina mimi nilikuwa mpenzi mkubwa wa vipindi vyako wewe na Jimmy K, atleast you lads knows what you are doing!

You are always straight forward and you call a spoon, spoon! Sio kama makanjanja wengi wa radio na tv! Bigup saana dada
 
Makutano Show,
Nimefurahi sana kusikia kwa mara nyingine tena sauti ya "my favorite" Fina Mango, umenikumbusha enzi zile za Power breakfast ya ukwee!! alongside Masoud Kipanya.

Kiujumla show ni nzuri sana kwa jinsi nilivyoisikiliza, muhimu ni kuwa tayari kusikiliza na kupokea mawazo ya wadau hapa JF, mengine yanaweza kuwa ya hovyo, ama ya kukera, kukukatisha tamaa lakini nakuomba usimame imara kwani wengi wetu tuko pamoja na wewe,tunatambua uwezo wako.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom