Video: Maajabu ya mwaka huko Mwanza Busisi. Ukistaajabu ya Musa, uchawi upo

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,317
11,411
Hii hali ilitokea ghafla abiria walijikuta wakiwa wamezungukwa na magugu maji na majani eneo la Busisi Jijini Mwanza. Wakiwa ndani ya kivuko pasipo kuelewa nini kimetokea.

Habari zinasema kuwa ni Mzee mmoja ambaye aliamua kufanya hivyo kutokana na kuonesha kukasirishwa na wao kumwacha ng'ambo wakijifanya wana haraka sana.

Basi akawaacha waende waendako si wana haraka. Hapo kivuko kinaonekana kikiwa kimezungukwa na magugu maji na majani na hivyo kuwawia ugumu abiria kushuka.

Habari ni ya uongo..
we unasema vingine na clip inasema vingine.

hayo magugumaji sio habari kwa watu wa kanda ya ziwa..
uenda kwenu ni Mbeya ndani ndani uko, ndo umeona hii ni habari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hali ilitokea ghafla abiria walijikuta wakiwa wamezungukwa na magugu maji na majani eneo la busisi Jijini mwanza. Wakiwa ndani ya kivuko pasipo kuelewa nini kimetokea.

Habari zinasema kuwa ni mzee mmoja ambaye aliamua kufanya hivyo kutokana na kuonesha kukasirishwa na wao kumwacha ng'ambo wakijifanya wana haraka sana.

Basi akawaacha waende waendako si wana haraka. Hapo kivuko kinaonekana kikiwa kimezungukwa na magugu maji na majani na hivyo kuwawia ugumu abiria kushuka.

View attachment 1305690
Angeotesha mahindi.... sasa magugu sio ndio asili yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui ndugu zangu wa kanda ya ziwa watabadilika lini kuacha imani za kishirikina.

Mambo ya kawaida hayo ila watachukulia ni uchawi.

Mambo ya hovyo kabisa.
 
Hakuna uchawi wowote hapo, kwani magugu maji ulitaka yakazunguke nyumbani kwako nchi kavu? Tuonyeshe video ya magugu maji yakiwa hayapo na yakiwa yanaanza kuja hadi yalipojaa hivyo.
 
Hii hali ilitokea ghafla abiria walijikuta wakiwa wamezungukwa na magugu maji na majani eneo la busisi Jijini mwanza. Wakiwa ndani ya kivuko pasipo kuelewa nini kimetokea.

Habari zinasema kuwa ni mzee mmoja ambaye aliamua kufanya hivyo kutokana na kuonesha kukasirishwa na wao kumwacha ng'ambo wakijifanya wana haraka sana.

Basi akawaacha waende waendako si wana haraka. Hapo kivuko kinaonekana kikiwa kimezungukwa na magugu maji na majani na hivyo kuwawia ugumu abiria kushuka.

View attachment 1305690

Huko ndiko kuhujumu uchumi kwenyewe
 
Mahala penye imani za kichawi namna hii kama huko,hakufai kabisa,uchawi hudumaza maendeleo ya pahala au eneo hata uwawekee maendeleo ya aina gani.
 
Mahala penye imani za kichawi namna hii kama huko,hakufai kabisa,uchawi hudumaza maendeleo ya pahala au eneo hata uwawekee maendeleo ya aina gani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom