VIDEO - Laptop Mpya za HP zina Ubaguzi wa Rangi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Laptop Mpya za HP zina Ubaguzi wa Rangi?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Jan 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  VIDEO - Laptop Mpya za HP zina Ubaguzi wa Rangi?
  [​IMG]
  Black Desi akiwa mbele ya Webcam yake Friday, December 25, 2009 3:24 AM
  Kampuni kongwe duniani ya teknolojia ya HP imekiri kuwa kamera zake mpya za kompyuta (Webcam) zenye uwezo wa kutambua sura za watu, zina matatizo ya kuwatambua watu weusi. Kampuni ya HP ilishutumiwa kufanya ubaguzi wa rangi baada ya kamera zake mpya za kompyuta (Webcam) ambazo zina uwezo wa kuitambua sura na kuifuata jinsi mtu anavyokisogeza kichwa chake kuzitambua sura za wazungu tu na kushindwa kuzitambua sura za watu weusi.

  Tatizo hilo liliingia kwenye mtandao mwanzoni mwa mwaka huu wakati mwanaume mmoja mweusi wa Marekani anayejiita "Black Desi" ambaye ameoa mzungu alipoweka video kwenye YouTube akishutumu HP kwa kufanya ubaguzi wa rangi.

  Katika video hiyo, Webcam ya HP iliweza kuionyesha na kuifuata sura ya mke wa Black Desi anayejiita "White Wanda" lakini iligoma kuionyesha sura ya Black Desi jinsi alivyokuwa akikisogeza kichwa chake.

  Video hiyo ya Black Desi ilifanikiwa kuwavutia watu zaidi ya laki tano kwenye YouTube ndani ya muda mchache.

  Katika video hiyo Black Desi alionyesha jinsi webcam hiyo ilivyokuwa ikifanya kazi kama inavyotakiwa iwe wakati mke wake alipoionyesha sura yake lakini ilisimama ghafla wakati Black Desi alipoingiza kichwa chake.

  Video hiyo imesababisha mjadala mkubwa kwenye forum mbali mbali duniani watu wakijadili kama kweli HP ilidhamiria kufanya ubaguzi wa rangi au la.

  Kampuni ya HP ilitoa tamko lake ikimshukuru Black Desi kwa kuligundua tatizo hilo na kuliweka wazi na wameahidi kuzifanyia kazi webcam zao kuliondoa tatizo hilo.

  Angalia Video chini Kuielewa vizuri habari hii.


  VIDEO - Laptop Mpya za HP zina Ubaguzi wa Rangi?

  http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3803946&&Cat=2
   
Loading...