VIDEO: Kwata ya kimya kimya na Makomandoo wa JWTZ

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,761
December 9 2016 zimefanyika sherehe za maadhimisho ya 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru Dar es salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alikuwa mgeni Rasmi.

Moja ya vitu vilivyopamba sherehe hizo ni pamoja na kwata ya kimya kimya, kwata hiyo ya kimya kimya imefanywa na kundi ambalo imeelezwa limeundwa mwezi April 2016 na kwenye sherehe za Uhuru hili ni onyesho lao la tatu.

Askari hao wameonyesha namna ya kuchezea silaha jinsi watakavyo na jinsi ambavyo wanaweza kufanya vitendo kwa haraka zaidi na kwa usahihi, kingine ni kuwa askari hao wote wana kilo si zaidi ya 45. Bonyeza play hapa chini kutazama.



Pamoja na gwaride la kimya kimya, Mbele ya Rais Magufuli Makomando wa JWTZ walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wao ikiwamo pamoja na namna ya kukabiliana na adui. Bonyeza play hapa chini kutazama.

 
Hongera JWTZ. Hii silent drill waliianzisha wamarekani kupitia regiment yao ya US Marines. Tafuta kwenye youtube utaona umahiri wao.

Gwaride la majeshi ya marekani yanatofauti kubwa dhidhi ya haya yanayofuata mfumo wa Uingereza. Katika mfumo wa Uingereza tunatumia nguvu sana katika kila tendo, iwe kupiga saluti au kuhot hima. Wamarekani wanatumia upole instead - nia ikiwa ni kueleza kuwa jeshi lenye nguvu ajabu pia linaji restraiin kuapply hizo nguvu.

Back to uwanja wa taifa, watangazaji wameharibu kabisa hi silent drill kwa kubwabwaja non stop. Walikuwa kama wanatuandaa kwa performance wakati performance ilishaanza. Raha ya silent drill ni kuiangalia kimya na kuacha milio ya chuma za bunduki zilie zinapopigwa kwa ukakamavu katika kila tendo la askari. Next time wajirekebishe
 
Jivunie cha kwako.Hao wajapani acha wajapani wenyewe wahangaike nao.
Tatizo letu watazania hatupendi kushindana na vitu bora kisa uzalendo, uzalendo haujengwi hivyo kaka nenda China,India, Russia, USA, UK,n.k utagundua uzalendo ulivyo hii ya kushangilia kitu bila kuuliza ndio imetufikisha hapa.

Naipenda Tanzania ndio maana naonyesha kwamba sie hatuna sera nzuri hivi vitu tukifundisha watoto na kukazania vijana wetu tokea watoto kushiriki kikamilifu kwenye hizi extra curriculum activities tutafika mbali. kuna tatizo la ulevi na unene hakuna mtu anasema ni aibu kuonyesha komando ana kitambi hii video nikiweka kwenye GIF online itaenda viral.

Ifike mahali ni kuweka maslahi ya taifa mbele na kusifia au kukosoa ili tufike mbali, wengi tunasahau kwamba hatushindani CCM na UKAWA au Mbeya na Kagera ila tunashindana na dunia. Uwezo wa kufika Tanzania tunayoitaka upo ila hatuna nia wala malengo mathubuti.

Mungu ibariki Tanzania
 
Kila inchi ujivunia kuwa na Jeshi imara hasa likiwa na makomandoo shupavu na Hodari lakini Kwa makomandoo hawa napata mashaka,
Show waliyotuonyesha Jana 55yrs uhuru Naona Kama imerudiwa vile ishawahi kufanyika mala Kazaa nyuma vile,,,?
1.kupigana Kwa fimbo
2.Kuvunja matofari
3. karate
4.kulalia misumari.
pia hata bahazi ya washiriki ni walewale Hulu bahazi yao wakionyesha kushindwa bahazi us mambo. Nilichokiona zaidi walikuwa wanafanya maigizo ambayo tena niwaigizaji wabongo movie sio wakina rambo wa Hollywood.
Kwa mtazamo wangu tuepuke kuonyesha uzaifu wetu mbele za watu watatuvamia tutajuta.
Wale makomandoo hata kwetu uswahilini wapo wanaweza kufanya vilevile tena na nyongeza Juu yakutembea na baiskeli ya taili moja na ngongoti.
Kwa Mimi nalipongeza Kwata la kimyakimya angalau wameniburudisha na kuonyesha Jeshi letu ni makini zaidi.
 
Back
Top Bottom