Video: Kumbuizi ya miaka minne (4) ya kupigwa risasi 37, Tundu Lissu ajibu swali la kupigiwa simu na Dr. Willbroad. P. Slaa...

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,327
2,000
Lissu mtu mbinafsi kupita kiasi. Ingekua mandela amegeuza kufungwa kwake ndio ajenda kuu kwenye siasa zake sijui ingekuaje. Halafu unakuta mijinga inamlinganisha lissu na mandela. Mtu tangu ajeruhiwe na watu hawajulikani ndio imekua siasa zake. Anafikiria usalama wake binafsi na kulipiza kisasi tu. Mtu mbinafsi muoga kama kunguru anaweza kuongoza kitu gani zaidi ya kutafuta maslahi binafsi?
Thomas Sankara alisema tofauti ya mwanamapinduzi na mchumia tumbo ni namna mtu alivyo tayari kutoa uhai wake bila kujutia katika kupigania maslahi ya umma. Lissu ni mwanasiasa mchumia tumbo tu. Kwa hofu ya maisha yake yeye na familia yake amewakimbia wale anaodai kuwatetea kwenda kuishi brussels kwa fadhila ya mabeberu. Mji wa brussels ubeljiji ndio mahali wakoloni waliketi mwaka 1884 kugawana bara la afrika.
Ulaya ndio kimbilio la waafrika wanaoteswa na waafrika wenzao Ili wamalizwe
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,434
2,000
Lisu ni mropokaji tu!! Hana lolote, aendelee kutafuta huruma ya wananchi. Kila siku story ile ile, kupigwa risasi, kupigwa risasi
Mbona hili linakuchukiza sana! Vipi ni moja wa wasiojulikana? Not pleased because things didn't go the way you wanted them to...!!!
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,201
2,000
Na wakamficha Dereva mpaka Leo.
Risasi kibao zipigwe kutokea kushoto, alafu zitue kwenye mguu wa kulia!
Alafu Dereva aliyeko kulia isimpate risasi hata moja! Kisha atoreshwe kwenda nje ya nchi!
Alafu wazee wa propaganda za mapicha picha, CHADEMA, wasionyeshe hata picha moja mpaka Leo!
Hakika tukio Lina maswali mengi ambayo bado hayajapata majibu!
Unaweza ukafanya dhambi yoyote mbaya kabisa ukiwa gizani wanadamu wasikuone lakini Mungu anaona yote.
Na maisha haya ni ya muda tu ,uwe na madaraka au usiwe nayo ,uwe na fedha au usiwe nazo ,muda ukifika utakwenda mbele za Mwenye dunia na kila kitu ,mwenye kupima matendo ya kila mtu kwa haki.

Kama alijipiga risasi mwenyewe haina sawa,kama alipigwa sawa : Yote ipo siku Mungu atajibu.
Waovu wanaongoza kila mahali Afrika ,huku wema wakitiwa hofu kwa uchawi,ushirikina na mitutu ya bunduki.

Katiba mpya itakuja kwa uwezo wa Mungu mana katiba ya sasa ni kivuli cha waovu kutawala watu wema kwa manufaa yao binafsi huku wakijiimarisha kwa dhulama na kuwatisha watu kwa kutumia vyombo vya dola. Tunataka katiba inayowafanya wanajeshi wetu wawathamini watanzania wote kwa usawa badala ya kuwachongamisha na ndugu zao na kuwafanya wengine kuwa ni maadui.
 
Turnkey

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
7,323

Utakuwa huna utu na mkatili sana
 
mundaliku

Senior Member
Oct 17, 2012
106
225

Halafu Hamza pamoja na kufa polisi wameweza kujua Hamza ni nani!!
 
mundaliku

Senior Member
Oct 17, 2012
106
225
Dunia iko hivyo, wengi tu hupigwa risasi na wengine hupoteza kabisa maisha, aliyepigwa lisasi akabaki hai, ni mhimu kumshukuru MUNGU

Nambo mengine huwezi kuyabadirisha, yatakuwa hivyo kwa Lisu siku zote, hata tukikumbushana na kukumbushana tukio hilo bado itakuwa hivyo hivyo

Na aishivyo MUNGU, hawezi kuruhusu mtu aliyejeruhiwa akawa na wazo moyoni mwake kwamba, ngoja aombe uongozi ili wamtambue waliomfanyia ubaya, Mungu hawezi kumpa hiyo nafasi hata kidogo, na kama bado ako na mawazo hayo kama waleta crp zake hapa wanaziandika eti iko siku!!

Mungu hawezi kuruhusu kumpa uongozi mtu mwenye mawazo ya ugaidi kuongoza nchi licha ya kwamba yeye kafanyiwa ugaidi

Kisasi ni cha Mungu mwenyezi
Hechilema
 
King klax

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
3,682
2,000
Na wakamficha Dereva mpaka Leo.
Risasi kibao zipigwe kutokea kushoto, alafu zitue kwenye mguu wa kulia!
Alafu Dereva aliyeko kulia isimpate risasi hata moja! Kisha atoreshwe kwenda nje ya nchi!
Alafu wazee wa propaganda za mapicha picha, CHADEMA, wasionyeshe hata picha moja mpaka Leo!
Hakika tukio Lina maswali mengi ambayo bado hayajapata majibu!
Usiwe mbumbumbu eneo lile la serikali au Chadema?
Nani aliondoa walinzi wa eneo lile?
Nani aliondoa CCTV eneo lile?
 
JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,234
2,000
Unaweza ukafanya dhambi yoyote mbaya kabisa ukiwa gizani wanadamu wasikuone lakini Mungu anaona yote.
Na maisha haya ni ya muda tu ,uwe na madaraka au usiwe nayo ,uwe na fedha au usiwe nazo ,muda ukifika utakwenda mbele za Mwenye dunia na kila kitu ,mwenye kupima matendo ya kila mtu kwa haki.

Kama alijipiga risasi mwenyewe haina sawa,kama alipigwa sawa : Yote ipo siku Mungu atajibu.
Waovu wanaongoza kila mahali Afrika ,huku wema wakitiwa hofu kwa uchawi,ushirikina na mitutu ya bunduki.

Katiba mpya itakuja kwa uwezo wa Mungu mana katiba ya sasa ni kivuli cha waovu kutawala watu wema kwa manufaa yao binafsi huku wakijiimarisha kwa dhulama na kuwatisha watu kwa kutumia vyombo vya dola. Tunataka katiba inayowafanya wanajeshi wetu wawathamini watanzania wote kwa usawa badala ya kuwachongamisha na ndugu zao na kuwafanya wengine kuwa ni maadui.
Tatizo mmetekwa sana kihisia na kufanya akili isitumike ipasavyo! Hata mimi ni binadamu na siungi mkono dhuruma au unyama kwa binadamu.

Nilichohitimisha mimi ni kusema maswali mengi hayana majibu. Au kwako kila kitu ni bayana?

Alafu kujidanganya kwamba katiba mpya ni muarobaini wa kila kitu ni kuweka akili mfukoni. SA imesifiwa sana kwamba ina katiba nzuri, lakini angalia mauaji yalivyotamalaki!
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,201
2,000
Tatizo mmetekwa sana kihisia na kufanya akili isitumike ipasavyo! Hata mimi ni binadamu na siungi mkono dhuruma au unyama kwa binadamu.

Nilichohitimisha mimi ni kusema maswali mengi hayana majibu. Au kwako kila kitu ni bayana?

Alafu kujidanganya kwamba katiba mpya ni muarobaini wa kila kitu ni kuweka akili mfukoni. SA imesifiwa sana kwamba ina katiba nzuri, lakini angalia mauaji yalivyotamalaki!
Wewe unafikiri wakati Mandela apipokua kifungoni alikua anatamka maneno ya kuwapenda makaburu ?

Hebu tutumie akili zetu vizuri ili hata watakao kuja baadae wajue kuwa tulishauri mambo mazuri.

Mandela amewasamehe Makaburu baada ya kutoka Gerezani na kuwa Rais.
Makaburu walikuwa weshaweka Sheria na katiba isigoruhusu tena Ubaguzi na wakaruhusu Shughuli za kisiasa ndio maana mandela aliposhinda walimtangaza.
Makaburu na unyama wao lakini hawakuvuruga uchaguzi ili waonekane kuwa wameshinda kisanii , walimpa ushindi Mandela ili amani irejee.

Kwa hiyo na usomi wako kabisa unaona kuwa Katiba ya Tanzania inaweza kuitawala Afrika Kusini hata mwaka mmoja bila kutokea vita ya makabila.? Katiba inayotoa mwanya kwa watawala waliochaguliwa kidemokrasia kuongoza nchi kijeshi haiwezi kuvumiliwa na Wazulu.

Usifikiri Serikali ya Afrika ya kusini ni wajinga kutumia nguvu ya kadiri kuwanyamazisha waandamanaji wa kule.
Wale wanawajua watu wao walivyo. AFRIKA kusini na ubabe wote wa makaburu lakini walishindwa kuzuia vurugu za kujitoa mhanga za wapigania uhuru.
Na nakuahakikishia hata tanzania kama CCM na serikali yake hawatabadilika nchi hii haina miaka 20 mbele bila watu kutoana ngeu. Vita ni ya Mungu siku zote . Wewe usije ukadhani bimadamu wote unaowaona wamezaliwa kwa ajili ya kula bata huku wenzao wakiwa wananyanyaswa . Hapana hata kidogo kuna watu wamezaliwa kwa ajili ya wengine , hao tangu enzi na enzi wapo. Hata uwaue watu kwa mabomu ya sumu kama alivhofanya Sadam lakini watapinga dhulma kwa nguvu zote.
Lisu alisema wazi kuwa kama angechaguliwa basi angeunda tume ya maridhiano ili waliofanya makosa wakiri na kuwaomba msamaha waliowakosea. Hakuwahi kusema kuwa atalipa Kisasi.

Na pakiwa na Katiba bora hata kisasi hakina maana .Waovu watajivua wenyewe kwenye uongozi.
Haiwezekani uwe na Mkurugenzi anayevuruga uchaguzi kwa wazi kabisa bila hata kificho halafu aendelee kukalia ofisi kwa sababu tu anateuliwa na amiri Jeshi mkuu na mtu anayeteua majaji wote kama apendavyo halafu unasema kuwa katiba hiyo ni nzuri.
Haijawahi kutokea kwenye historia kundi moja ndani ya jamii likawatesa wengine muda wote kwa sababu ya uimara wa Jeshi au silaha. Uimara wa jeshi ni kusimamia Haki sio kupora haki.

Unajua Osama bin Ladeni shujaa kwa Waarabu na waislam wanaoishi leo kwa amani Ulaya na Marekani . Kama sio amsha amsha ya Osama mpaka leo wasilam na Waarabu wangekua wamabaguliwa na dini yao kudharauliwa Ulaya. Kuheshimu na kumtendea mtu haki bila kujali dini yake na itikadi yake ni msingi wa amani.

Kosa la Lisu ni Lipi.?
Je, nani angefurahi kuona ndugu yake au kiongozi anayempenda anapigwa risasi bila kosa lolote?
Nani asiyejua kuwa Lisu alianza kupigania maslahi ya nchi hii kwa miaka mingi wakati hao waliokua wananugaika ndio awaliokuja kujiita wazalendo feki ili kulinda vyeo!!?

Je, kama Lisu angekua mbunge wa CCM angepigwa risasi bila mtu yeyote lukamatwa ? Yani hakuna hata mtu aliyetangaza kuwa kuna mtu anashikiliwa kwa mahojiano ?

Mungu tunayemwamini ataliweka sawa Taifa hili wala hatuna shaka na hilo. Tumechoka kutawaliwa na watu waovu ,washirikina ,wauaji,wezi, wanafiki,wazinzi,walevi,wachawi na watesaji wasiofuata sheria ama za dini au hata walizoweka wenyewe.
Ije katiba mpaya ama ya zamani Siku Kikombe cha ghadhabu ya Mungu kikijaa atajibu kwa Moto.
Ogopa mtu unayemdhulumu halafu halafu hana uwezo wa kujitetea ni bora anayepambana mana atatumia nguvu zake. Asiyepambana anamwachia Mwenyezi apambane kwa haki.

Tanzania hata wakaoloni waliondoka kwa Dua tu za Wazee wa Kiislam kwa amani na Upendo kabisa bila kuuana. Kama wageni walikaa pembeni kwa amani basi hata Wakoloni weusi wa leo wataondoka kwa amani tu mana wao ni ndugu zetu wa damu.

Katiba Mpya ni muhimu ihi hii yenye ladha ya mkoloni iondoke na viashiria vyake vyote vya kikoloni.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,127
2,000
Tatizo mmetekwa sana kihisia na kufanya akili isitumike ipasavyo! Hata mimi ni binadamu na siungi mkono dhuruma au unyama kwa binadamu.

Nilichohitimisha mimi ni kusema maswali mengi hayana majibu. Au kwako kila kitu ni bayana?

Alafu kujidanganya kwamba katiba mpya ni muarobaini wa kila kitu ni kuweka akili mfukoni. SA imesifiwa sana kwamba ina katiba nzuri, lakini angalia mauaji yalivyotamalaki!

..swali ulilouliza halikuwa na mantiki kabisa.

..mbona hukuuliza jinsi alivyoumizwa kwa risasi mikono yote?

..au risasi zilizotolewa tumboni, mbona hukuhoji kama wafyatua risasi walikuwa mbele ya gari?

..kuhusu Katiba ni kweli haitatui matatizo yote ya nchi yetu, lakini kweli kuwa itatatua baadhi ya matatizo na hilo ni jambo jema.

..Kwani Afrika Kusini, ambao umewatolea mfano, walipoandika Katiba, waliahidi kuwa itatatua matatizo yote yanayoisibu nchi yao?
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,134
2,000
Lisu ni mropokaji tu!! Hana lolote, aendelee kutafuta huruma ya wananchi. Kila siku story ile ile, kupigwa risasi, kupigwa risasi

Ama kwa hakika mzigo wa mwenzio kwako ni kanda la sufi.

Wewe ulishapigwa risasi ngapi mkuu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom