Video: Kesi ya F. A. Mbowe na wenzake, wakili aichambua hukumu ndogo ya Jaji M. Siyani...

Kisheria inaruhusiwa kukata rufaa ?
Hapana, siyo ktk hatua hii...

Hii ilikuwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi kubwa (trial within trial)...

Rufaa inaweza kukatwa iwapo kesi ya msingi itaamuliwa na hukumu yake iwe na mwelekeo kama huu wa kesi hii ndogo...

Lakini hata kama hukumu itamwachia Freeman Mbowe na wenzake huru, maamuzi ya kesi hii ndogo LAZIMA yakatiwe rufaa ili kurekebisha precedence mbaya ya kuja kuumiza watu wengine huko mbeleni...
 
Shangazi asante, naana maneno yako ni msumeno ku moyo, CCM hawana hamu na wewe kabisa!! wanadai ati umekulia CCM afu unawasema kila siku kwenye mitandao si vizuri kabisa.
 
Mkuu 'Akasankara', siyo kwamba "Mama anaona kabisa katika hii NCHI hakuna shida" peke yake, kuna jambo la msingi zaidi ya kuona shida tu!

Kidogo inashangaza, kuna shida kubwa na watu waliopo huko kwenye utawala, wanaotoa ushauri na wanaotekeleza ushauri wenyewe!

Kila mtu anajuwa kesi ipo mahakamani, inaendelea, utawala unaamua anayesikiliza kesi hiyo azawadiwe, hata kabla ya kesi haijaamuliwa.

Hivi, katika hali ya kawaida, huwezi mtu/kiongozi ukasita kidogo kufanya baadhi ya maamuzi, angalao kwa muda ili usiweke mazingira ya kuonekana unaingilia maamuzi ya kesi?
Hata kama unajuwa uwezo wa kufanya hivyo unao, kule tu kujionyesha kwenye kadamnasi kufanya jambo kama hilo, halistuwi/tahadharishi hawa viongozi?
Hawa ni watu wasiokuwa na staha katika matendo yao? Hawajali wanaowaongoza watayachukulia vipi maamuzi yao?

Hawa sasa wamekuwa ni "sikio lisilosikia dawa." Wao sasa wanajiona wanaweza kufanya lolote wapendalo kufanya bila kujali kama matendo yao yatakuwa yanawafunua kuwa ni viongozi wasiostahili kuliongoza taifa hili.
Wanafanya maamzi ya kujiona wao ndio waliumba mbingu na dunia, na kutweza UTU, HAKI na UHURU wa watu. Mimi nashauri Mama azingatie pia kuna watu wanapitia mateso makubwa moyoni.
 
Back
Top Bottom