Mwendo Kasii
JF-Expert Member
- Sep 10, 2016
- 203
- 212
Jiji la Nairobi limeingia tena kwenye headlines mpya baada ya kupitisha sheria itakayowabana wafugaji wa Mbwa. Ripoti zinasema iwapo Mbwa wako atabweka kwa dakika 6 mfululizo ndani ya saa moja au dakika tatu mfululizo ndani ya dakika 30 utatozwa faini ya Shilingi elfu tano za Kenya ambazo ni sawa na Shilingi laki moja na elfu saba mia sita za Tanzania au utatumikia kifungo cha miezi miwili jela.
Wataalamu wa mifugo wanasema pamoja na kupitishwa kwa sheria hiyo, kuna muda ukifika inakua vigumu sana kumfundisha Mbwa kubweka na kunyamaza.
Kituo cha TV cha K24 wameripoti kuhusu kero ya kelele za Mbwa kubweka kiholela imesababisha kutungwa kwa sheria ya kudhibiti ubwekaji wa aina hiyo.
source: Millard Ayo