Video: Karume, Okello na Babu pamoja masaa baada ya Mapinduzi - Wasikilize mwenyewe

hivi kweli watu wanafikiria mafuta ya Pemba yatazidi utajiri wa mafuta ambao unaweza kupatikana bara? ukijumlisha na utajiri mwingine wa madini lukuki? Really?

Mzee Mwanakijiji, Tanzania hakuna sehemu watu wanapenda na kufuatilia siasa kama Zanzibar. To what level they really understand the big picture of the critical issues surrounding them including security? Hapo sijui sana, ingawa nahisi wana siasa wanataka kuwazidi maarifa watu wenye kipato na uelewa kidogo wa jinsi mambo ya Dunia hii yanavyokwenda. Kwa maneno hatuwezi kushindana na wazanzibar....ila naona sasa imefika mahala waamue kusuka au kunyoa. Naamini mbele ya safari watakuwa kama wale waliokuwa wanamlilia Musa awarudishe Misri maana walikuwa wanalikuwa wanakula nyama.
 
Last edited by a moderator:
Huu muungano naona kama Nyerere aliwalazimisha Wazanzibar! Kumbe Karume alikua hata Kiiengereza hajui? halafu kwenye makubaliano hayo ya huo muungano uliandikwa kwa Kiiengereza! Kwamtazamo wangu nahisi Nyerere pia alikua ni Dikteta! Hawa watu wapewe nchi yao.
 
Sijui ni wazanzibara au wazanzibari wanaopiga kelele muungano uvunjike? Maana sekeseke likianza wazanzibara ambao wengi wao ni wamanyema,wanyamezi,wazaramo na wandengereko watarudi bara. Sijui wazanzibari watakimbilia oman. Tukae tusubiri mwisho wa hii sinema.
 
naafiki kwa 100% mambo matatu hivi:
Kwamba tunahitaji sababu za kuungana na ZNZ mwaka 2012 na kuendelea na siyo 1964 HILI LINAHITAJI REFERENDUM kama mjumbe alivyosema na tukitoka hapo wenye nchi wakiukubali Muungano hatua nyingine ni aina ya Muungano;
Kwamba Muungano huo kama tunautaka pande zote ziridhike aina ya Muungano:serikali 3 ama 2 ama 1 ama tawala za majimbo na ZNZ iamue kama ni jimbo linalounganisha Ungujaa na Pemba ama Pemba ijitegemee
Kwamba kwa vyovyote hiyari ya wananchi itangulie juu ya maslahi ya watawala
KWAMBA Muungano wa sasa ni halali kisheria.ZNZ wangemfungulia kesi Karume kama angekuwa hai kwa kutumia madaraka vibaya na sisi wa Tanganyika tungelimfungulia mashtaka Nyerere kama tunaamini alituingiza mkenge.kwa kuwa hawapo tunaweza kuuvunja Muungano huo kwa njia za amani bila kuchomeana nyumba na kutukanana kwenye forum mbalimbali
 
Japo sijaweza kufanikiwa kuiona hii Vídeo ila
Asante kwa mwanzisha uzi, kumbukumbu kama hizi ni kumbukumbu muhimu sana kwa siku ya leo na kwa kizazi cha leo.

Tuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuenzi matokeo chanya ya Mapinduzi hayo ambao ni Muungano wetu adhimu ulituzalishia taifa moja tuu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kule Zanzibar wao wana msemo wao was
Mapinduzi Daima
Na sisi Watanzania katika umoja wetu tunasema kwa kauli moja
Tutaulinda Muungano kwa gharama yoyote, na hata kama gharama yenyewe ni kutengua demokrasia kama ilivyofanyika kwenye uchaguzi wa Zanzibar, for the sake of union, demokrasia na itenguliwe! .

Nawatakia mapumziko mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Back
Top Bottom