Video: Jerry Muro apasua jipu la sakata lake la rushwa!

Huko Ulaya watu binafsi wanakuwa na pingu majumbani......Swali hapa ni je kuwa na pingu ni kosa nchini Tanzania?
 
..yah wengine hutumia pingu ktk tendo la ndoa.

..hata mikwaju na mijeledi hutumika ktk tendo la ndoa.

..ila hiyo bastola aliyokutwa nayo, mhhhh!!

Mhhh..Hizi habari mbona zinachanga sana,hebu angalia hii

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaal Afande Suleiman Kova leo ameongea na waandishi wa habari na kutoa taarifa juu ya sakata la mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Utangazaji Tanzania (TBC) juu ya madai ya kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa bw. Maiko Calos aliyekuwa mhasibu wa Harmashauri ya Mji wa Bagamoyo kabla ya kutemeshwa mzigo na Waziri mkuu Mizengo pinda hivi karibuni.

Afande kova akizungumzaia sakata hilo amesema Bwana Maiko Calos alitoa taarifa polisi akidai kuna watu wanamsumbu sana na kumtisha wakidai awape shilingi milioni 10 kabla ya kuibua kashfa zake kwenye vyombo vya habari, hivyo Afande kova aliwaamuru vijana wake kufuatilia tukio hilo katika mgahawa wa City Garden jijini Dar es alaam na kuikuta gari ikiwa imeegeshwa , ilibidi Maiko awasiliane na huyo mtu ili waingie hapo hotelini hata hivyo mtu huyo alikataa hivyo wakamfuata kwenye gari na kukuta Ni jerry Murro mwandishi wa TBC.

Anasema walimchukua mpaka kituo cha polisi na kuchukua maelezo ya bwana Maiko ambaye alisema anamfahamu Jerry Murro kwani wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini, pia akadai kwamba kuna miwani yake aliisahau kwenye gari ya Jerry Murro na pia kuna pingu na Silaha yaani bastola ambvyo mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia kumtishia ili atoe hizo fedha.

Hata hivyo afande Sulaiman Kova hakuthibitisha kwamba Jerry Murro amekamatwa na hizo shilingi milioni 10, lakini amesema kujipati fedha au kumdai fedha mtu yeyote kwa kumtishia ni kosa la jinai, hivyo kutokana na mazingira ya maelezo ya mlalamikaji na vielelezo vinatufanya kuamini kwamba tukio hilo lilikuwepo, ameongeza kuwa hawakuweza kuwashirikisha (PCCB) Kikosi cha kuzuia Rushwa katika mtego huo kwakuwa muda ulikuwa ni mdogo na mtuhumiwa angeweza kukimbia na kuwapotea

Kuhusu Bastola ambayo inamilikiwa na Jerry Murro Afande Kova amesema silaha hiyo imetengenezwa nchini Chec. Republic ni SZ 97 B NO A 6466 inayobeba risasi 10 anaimiliki kihalali kabisa, ina vibali vyote na alipewa kwa ajili ya kujilinda na maadui zake kutokana na kazi zake za habari za uchunguzi, Isipokuwa pingu ambazo hakuna raia ambaye anaruhusiwa kumiliki kisheria.

Ameongeza kwamba Kesi hiyo wataipeleka kwa mwanasheria wa Serikali ili aone kama kuna kesi ya kujibu na kuipeleka mahakamani ili haki itendeke kwa kila upande na kama itakuwa vinginevyo watamuita bwana Maiko Calos ambaye ni mlalamikaji na kumwambia yaliyojiri kutoka kwa mwanasheria wa Serikali




Hii ni kwa mujibu wa John Bukuku wa hapa http://fullshangwe.blogspot.com/
 
Hivi Jerry Muro ni nani?

katika hii video kuna mambo ambayo ningependa kujua kwa undani

1.Jerry Muro anasema Kova is very minor person;siyo jeshi la POLISI.

Mshkaji angepunguza jazba kidooogo.

Habari hii sasa inachukua mkondo mwingine na inaweza ikamalizwa kimya kimya na watu wasijue nini kimetokea
 
Huyo dogo wanamtime tu, either that au anahitaji kupewa kazi Hollywood.

Halafu hiyo pingu ni non issue. Ningependa kujua amesemaje kuhusu hiyo ya bunduki.
 
Jerry is right, wananchi tumuunge mkono tusimwache mwenyewe, hawa watu muhimu wananchi tukiwacha tunawakatisha tamaa sana..
 
Pape senksi kwa hiyo, part II vipi? Mi nadhani jipu ndo kwanza linaanza kuweka usaa kitu bado kabisa. Jerry naye anaonekana kupanic na kuzungumza maneno makali kwa mfano ''Kova ni mtu mdogo sana katika jamii'' duh ndo maana nasema kitu ndo kwanza kimeiva hiki
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=naM5bR4DmOU&feature=player_embedded[/ame]
 
Pingu ni chombo cha kufungia kwa muda vitu viwili ili visiachane. Polisi wanatumia pingu kufunga kwa muda ama mikono mwili ya mtuhumiwa ili kumnyima uhuru wa kuitumia, au kufunga kwa muda miguu miwili ya mtuhumiwa ili asikimbie. Vile vile polisi wanaweza kutumia pingu kufunga mikono ya watuhumiwa wawili au mkono mmoja wa mtuhumiwa na kitu kisichotembea kama nguzo ili kumzuia mtuhumiwa asikimbie.

Siyo lazima polisi watumie pingu tu ili kuwathibiti watuhumiwa, vile vile wanaweza kutumia kamba au cable ties kufanya hivyo kama inavyoonekana katika picha hii hapa.

1252.jpg


Pingu siyo silaha kwa vile hutumika tu pale ambapo mtuhumiwa anapokuwa ameshazidiwa nguvu. Ni kwa hali hiyo, pingu haiwezi kutumika kufanya ujambazi. Pingu zinanunuliwa kirahisi madukani kuliko bunduki, kwa mfano unaweza kununua pingu kwa dola 21 hapa

discounthandcuffs_top_logo.gif


Mtu yeyote anaweza kunua pingu kwa matumizi binafsi ya namna nyingi tu; kwa mfano, kufungia baiskeli kwenye nguzo isiibiwe. kufunga mbwa mkali kwenye nguzo asiume watu wakati wa mchana, na kadhalika. kwa hiyo Uharamu wa bwana Muro kumiliki pingu mimi siuoni. Kuna maduka fulani ya bunduki hutoa bakshishi ya pingu moja ambayo unaweza kuitumia kufungia bastola yake sehemu flani ili isitumiwa na watu wengine ndani ya nyumba bila kibali chako. Inawezekana Bwana Muro alipewa pingu zile kama sehemu ya bakshishi yake baada ya kunua bastola ile.


Kama kesi hii ya kukutwa na pingu litakuwa ni kosa kubwa sana, basi Tanzania tuna sheria za kibwanyeye kweli kweli zinazohitaji kuangaliwa. Haiwezekani iwe halali mtu kumiliki kitu hatari kama bastola lakini iwe haramu kumiliki pingu isiyokuwa na hatari yoyote kwa raia. Hata hivyo sishangani kuwepo kwa sheria za namna hiyo kwa sababu niliwahi kuambiwa kuwa kuvaa nguo za mabaka mabaka kama alizokuwa akivaa marehemu Lucky Dube eti ni kosa linaweza kumfanya raia alazwe selo. Au eti kuvaa viatu vya kazi (boots) vinavyohimiri mazingira magumu pia ni kosa hapa kwetu Tanzania.
img_1542web.jpg

 
Huyo dogo wanamtime tu, either that au anahitaji kupewa kazi Hollywood.

Halafu hiyo pingu ni non issue. Ningependa kujua amesemaje kuhusu hiyo ya bunduki.

Nanukuu


'Kuhusu Bastola ambayo inamilikiwa na Jerry Murro Afande Kova amesema silaha hiyo imetengenezwa nchini Chec. Republic ni SZ 97 B NO A 6466 inayobeba risasi 10 anaimiliki kihalali kabisa, ina vibali vyote na alipewa kwa ajili ya kujilinda na maadui zake kutokana na kazi zake za habari za uchunguzi, Isipokuwa pingu ambazo hakuna raia ambaye anaruhusiwa kumiliki kisheria
Ameongeza kwamba Kesi hiyo wataipeleka kwa mwanasheria wa Serikali ili aone kama kuna kesi ya kujibu na kuipeleka mahakamani ili haki itendeke kwa kila upande na kama itakuwa vinginevyo watamuita bwana Maiko Calos ambaye ni mlalamikaji na kumwambia yaliyojiri kutoka kwa mwanasheria wa Serikali'
 
Nanukuu


'Kuhusu Bastola ambayo inamilikiwa na Jerry Murro Afande Kova amesema silaha hiyo imetengenezwa nchini Chec. Republic ni SZ 97 B NO A 6466 inayobeba risasi 10 anaimiliki kihalali kabisa, ina vibali vyote na alipewa kwa ajili ya kujilinda na maadui zake kutokana na kazi zake za habari za uchunguzi, Isipokuwa pingu ambazo hakuna raia ambaye anaruhusiwa kumiliki kisheria
Ameongeza kwamba Kesi hiyo wataipeleka kwa mwanasheria wa Serikali ili aone kama kuna kesi ya kujibu na kuipeleka mahakamani ili haki itendeke kwa kila upande na kama itakuwa vinginevyo watamuita bwana Maiko Calos ambaye ni mlalamikaji na kumwambia yaliyojiri kutoka kwa mwanasheria wa Serikali'

Hamna kesi hapo, wanataka kumzushia tu non issue iwe issue.

Hilo swala la pingu hebu mcheki Mzee Kichuguu kashuka utirio fresh kabisa. Kama sheria za Tanzania ziko Draconian hivyo mbona hata freaks wanaopenda ku role play kwenye bedrooms na pingu watapata tabu.
 
kwa namna yoyote ile hainiingii kichwani kwamba Jeryy muro amefanya hicho kitu ila tusubiri sheria naukweli tuu!
 
Kweli system wakati mwingine ni gereza. Kova kweli kavutika kutetea mchongo ambao hauna kichwa wala miguu? Wakati tunaposubiria sheria kuchukua mkondo wake na haki kutamalaki tunamwomba kova na jeshi lake wahakikishe usalama wa Jerry. Maana dhara lolote litakalompata jerry tunalazimika kuamini limetekelezwa na vijana wa Kova.
 
JERRY MURO ATINGA GLOBAL, APASUA JIPU, PWAA!!!


1265037100_exclusiveusifutenew.jpg

1265037555_jerrymuro.jpg


Jerry Muro, akiwa katika chumba cha habari cha gptz.com jioni hii akipasua jipu kuhusu sakata lake!
 
Baadhi ya maneno ya huyu bwana Muro yanaonyesha kuanza kulewa sifa. Kazi aliyoifanya mpaka sasa ni nzuri na muhimu sana kiasi cha kwamba ujinga kama huu na kebehi dhidi ya Kamanda Kova vinaweza kuharibu harakati zake na nyingine zinazohusiana.

Ushauri wa bure ni kwamba ndugu Muro apunguze munkari, ajifunze kutafakari, kuchagua na kupanga maneno yake hususani pale anapokuwa anaongelea watu ambao kwa mujibu wa sheria wana haki ya kufanya walichofanya mpaka sasa hivi.

Heshima mbele
 
JF proved to be the Home of great Thinker,
Hii habari ya Jery ni tamu sana na inavyoonekana ni mtego wa watu wachache ambao amekuwa akiwaweka wazi hata kipindi wanapokea rushwa.Nadhani watu kama hao sasa hawatakiwi TZ kama J.Muro asivyotakiwa na wanyonyaji wachache.Tuamini ukweli utajulikana tu.
 
Baadhi ya maneno ya huyu bwana Muro yanaonyesha kuanza kulewa sifa. Kazi aliyoifanya mpaka sasa ni nzuri na muhimu sana kiasi cha kwamba ujinga kama huu na kebehi dhidi ya Kamanda Kova vinaweza kuharibu harakati zake na nyingine zinazohusiana.

Ushauri wa bure ni kwamba ndugu Muro apunguze munkari, ajifunze kutafakari, kuchagua na kupanga maneno yake hususani pale anapokuwa anaongelea watu ambao kwa mujibu wa sheria wana haki ya kufanya walichofanya mpaka sasa hivi.

Heshima mbele
good point bwamdogo ana confidence kali sana,lakini ajiangalie asije kukalia kuti kavu,na ujana mwingi sana naona,mahali ambapo jamaa watatake advantage,shauri yake nafuata popcorn narudi.
 
Back
Top Bottom