Video inayosambaa ikionesha jinsi upigaji wa pesa za miradi unavyotokea

Mbona hilo ni jambo la kawaida sana katika kila halmashauri na kazi zote za kandarasi nchini. Hata kazi za ujenzi wa barabara ni hivihivi.

Makampuni ya Kichina hata wanaambiwa na serikali yao kwamba mnapodaiwa percentage punguzeni kwenye ubora wa kiwango sio kwenye faida ya kampuni. Ndio maana utaona kampuni cha China zikifanya kazi sehemu hakuna rushwa wanafanya kazi zenye ubora sana
 
..meishia nusu sijaendelea...huyu jamaa kajimwambafaii, anahitaji ngao ya ulinzi 🤣
 
Miradi ya ujenzi inayosimamiwa na halmashauri hii ni reality. miradi yote ya ujenzi hii ni reality. Aliyekuwa waziri mwenye dhamana na ujenzi kwa muda mrefu ndiye Rais.

No wonder ujenzi ni kila mahali sasa ili wapate percent. Kuleni jamani kuleni kiongozi yuko magogoni lakini sharti mkumbuke kutuma ten percent kupitia kwa mwana mpenzi wa jiji la maji chumvi.
 
Nimeanza kuwalewa CDM walivyosema kwamba dawa ya Tanzania ni kubadilisha mfumo wa kiutawala katika nchi; tatizo ni mfumo..bila hivyo vitendo kama hivi ni vigumu mno kuviondoa!!

Wenzetu wazungu aka mabeberu wao wanaomba 10%, lakini sisi tunaomba hadi 60% afu ukibisha unatishwa tishwa.
 
Ukweli ni kwamba kuchukua kandarasi katika halmashauri zetu ni tabu sana.

Ili upate kandarasi lazima utoe pesa na pesa za mradi lazima mzigawane na wakurugenzi na maengineer wa wilaya.

Ili ulipwe shahiki zako lazima napo mzigawane na wakurugenzi.

Halafu wanasiasa wanalalamikia wakandarasi wa ndani hawana uwezo wakati hata kulipa hawalipwi kwa wakati na hicho kidogo wanacholipwa wanakigawana na wakurugenzi.
 
Magufuli anakazi ngumu sana, ila tuendelee kumpa support. Hawa wezi watafutwe wafikishwe mahakamani
 
Back
Top Bottom