(Video) - Huwezi kuamini hata ukiangalia kwa macho yako mwenyewe!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Sasa sijui kama hii ni siasa au vipi lakini bado akili yangu imeshindwa kuunganisha ninachokiona na tafsiri yake kwenye ubongo wangu. Naomba mnisaidie:

Last edited by a moderator:
Sasa sijui kama hii ni siasa au vipi lakini bado akili yangu imeshindwa kuunganisha ninachokiona na tafsiri yake kwenye ubongo wangu. Naomba mnisaidie:

Mzee Mwanakijiji sorry, tunaomba ufafanuzi kitu gani hicho ambacho hujaelewa? Ni huko kuimport samaki au? Kama ndicho kwani ni kitu gani ambacho hatuimport? Tunaimport kila kitu, kuku, mboga za majani, tomato/chili source, mayai, nguruwe (kiti moto) na vingine kwanini tusiimport samaki? Then tunalalamika kwani shilingi inashuka kila siku against US $, huku ni zaidi ya kurogwa si bure. Lakini pia sishangai binafsi sishangai kwani huyo mmalawi anayeongoza wizara ya fedha degree yake naambiwa hata kuku au nguruwe angeweza kuwa nayo so what else should we expect from him?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli inasikitisha sana, licha ya kuwa tuna bahari, maziwa, mito na mabwawa mengi lakini tunaagiza samaki toka nje! Sijui tumerogwa au ni laana!
 
NI KWELI SAMAKI wanakua imported ? nimewahi kumuuliza hili swali jamaa mmoja anafanya kazi kwenye kampuni moja ya samaki hapa Mwanza, alinijibu "........... ni kweli, wanatoka Asia ya mbali."
akaendelea , tunaagiza samaki kwasababu ya ukosefu vyombo vya kuvua samaki wengi kutoshereza soko la samaki hapa Tanzania...."
nikapigwa butwaa , mwishoe nikaagiza konyagi nyingine , maisha yakaendelea jioni ile, ila inashangaza.
 
Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?
 
The funny thing is, where I am Samaki in particular Sangara ndiyo the only product you can easily find kutoka TZ ofcourse huwandikwa produce of Kenya, Uganda and Tanzania.

Hivi mkuu are you aware kwamba hadi ile mifuko ya plastiki kuna ambayo ni imported hapo Bongo?
 
"Comperative advantage" haiihusi kabisa nchi yetu ya TZ;hii nchi si bure nahisi mkono wa Mungu upo juu yetu!
 
Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?
Labda tunaagiza samaki kwa soko la wenye kipato cha chini. Wavuvi wengi siku hizi wanauza samaki wao moja kwa moja kwenye hoteli za kitalii. Samaki wanaobaki huko ndio upelekwa mnadani...
 
tena niliwahi kumsikia mtu akisema wale imported fish ni rejecrted fish katika hizo nchi za asia.
 
Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?

Kwa sababu our minds are set to worship things from western world (for christians) and arab nations (for Muslims) to a point that we can not be pride of our culture, heritage hata vitu vyetu wenyewe, huwezi kuamini kuwa kuna watu wakienda ferry wakikuta mswahili anauza samaki aliowavua yeye mwenyewe hawawezi kununua they will just go for imported ones.

You will be supprised that hata magazeti ya kufungia vitumbua yanaagizwa iran, dubai, malaysia, etc.
ghrrrr
 
Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?

Kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua, kwani mwaka juzi Magufuli si alikamata meli ya uvuvi ya kigeni ikitusaidia kuvua samaki kwenye nchi yetu ambao baadaye tutawaagiza? Samaki wanavuliwa kwenye bahari yetu halafu tunawanunua kwa mihela kibao kutoka huko kwao wakishapelekwa huko kusindikwa.
 
......sisi CHADEMA tutaliangalia hilo kwa jicho la tatu na nne na kulikomesha mara moja. Vitu kama vibiriti, tooth pick, nyanya, matunda ya aina zote, vegetables za aina zote, juice za aina nyingi, plastic houseware, nyama, samaki, kuku toka nje tutaviwekea kodi kubwa na kutoa nafuu ya kodi ya mitambo na malighafi ya kutengenezea hizo bidhaa. Hawa CCM ambao kila kukicha wahindi na wafanyabiashara wakubwa wanakimbilia ubunge they never think of mkulima mmatumbi wa nchi hii.
 
Mh pole sana mzee mwanakijiji kwa uchungu uliokupata kutokana na hilo la kuingiza samaki frozen kabisa kutoka ng'AMBO.kwakweli kwa mtu ambae ni mzalendo lazima itakuuma tu.ni biashara ya mtu hiyo anakiwanda chake soko ndio tanzania kwani hulijui hili.kaaeni chonjo kuna mengi yanakuja
 
Mzee Mwanakijiji sorry, tunaomba ufafanuzi kitu gani hicho ambacho hujaelewa? Ni huko kuimport samaki au? Kama ndicho kwani ni kitu gani ambacho hatuimport? Tunaimport kila kitu, kuku, mboga za majani, tomato/chili source, mayai, nguruwe (kiti moto) na vingine kwanini tusiimport samaki? Then tunalalamika kwani shilingi inashuka kila siku against US $, huku ni zaidi ya kurogwa si bure. Lakini pia sishangai binafsi sishangai kwani huyo mmalawi anayeongoza wizara ya fedha degree yake naambiwa hata kuku au nguruwe angeweza kuwa nayo so what else should we expect from him?

Mwanakijiji umeenda Marekani siku nyingi sana. Ukiwa hapa Tanzania utasikia vijana wanasema ooohh nchi yetu ina mabadiliko, ohh tunapiga hatua. Lakini ukweli ni kuwa hatupigi hatua. Leo asubuhi nilijaribu kutafuta kitu ambacho ni made in Tanzania milmani city, iliniwia taabu sana, huwezi amini hata kiti moto inatoka afrika kusini. Tumepiga hatua nyingi sana kurudi nyuma, na hakuna anayejali. watu wanaona kuimport vitu tunavyoweza kuzalisha ni maendeleo.

by the way unajua kuwa bei ya mitumba Tanzania ni kubwa kuliko nguo mpya? na kuvaa mitumba ni more prestige than kuvaa nguo mpya.THIS IS TANZANIA.
 
Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?
Mzee Mwanakijiji, nini samaki!, tunaagiza maziwa, kwenye ma supper markets yetu, maziwa karibu yote ni imported sababu pekee ni eti hatuna maziwa ya kutosheleza soko la ndani. Wakati kwenye ranch ya Kongwa, maziwa yanakamuliwa na kumwagwa ili ngombe wasiugue!. Lowasa alilazimisha yagawiwe bure kwenye shule za jirani, tatizo likawa namna ya kuyafikisha tuu hata hapo shule za jirani!. Tanzania ni nchi ya tatu kwa mifugo barani Afrika, ukiondoa Botwana na Namibia, lakini ndiye importer mkuu wa maziwa ya Kenya, let alone blue band na vikorokoro vyake japo ni margarine, wanaita siagi!.

Mitaa ya Dar kwenye kila mabarabara kwenye foleni za magari, vijana wanauza apples, machungwa na machenza kwenye vimifuko vidogo vidogo, Alas! kumbe vyote ni imported toka Afrika Kusini, wakatui zile apple za Lushoto, zinaozea mitini na machungwa ya Segera, yanaozea pale barabarani kwa kukosa masoko!.

Ingia Shoprite na The Game pale Mlimani City, mpaka mchicha, karoti, spinach, vitunguu etc etc vyote ni imported!.

Kwa walaji wa Steers, zile kuku na beef kwenye burger zao ni kutoka kwao, eti za hapa hazina viwango!.

TBL nako sio haba, kuanzia chupa tupu, office furniture, na all consumables ni kutoka Kusini.

Hivi wiwanda vya nguo ikiwemo Karibu Textile, wanaiport ready made majora toka India na kinachofanyika pale ni kuprint tuu hizo kanga na kuacha takataka za sumu ya yale marangi zikimiminikia mtoni na kutuchafulia mazingira, huku pamba ya Mwanza ikiozea ghalani kwa kukosa masoko.

Tusishangae sana, kama hata kutengeneza tooth pick ni mpaka Chini, hata kutengeneza pini tuu ni issue, unategemea nini?.

Ila pia kwenye sifa lazima tujisifu, Watanzania ni wazuri sana katika kujieleza, tumefanya hivi...., tumefanya vile... tuongezeeni miaka mitano mingine tukamilishe ile ahadi ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, kwani sasa tunakuja na Ari Zaidi.., Kasi Zaidi na Nguvu Zaidi!.

CCM Oye!.
 
Tanzania hatuna medium na large scale investors wanao weza kuwekeza huko? nNijuavyo mimi samaki ni biashara inayo lipa haswa ukiwa na vitendea kazi.
 
Bongolander;1037359]Mwanakijiji umeenda Marekani siku nyingi sana. Ukiwa hapa Tanzania utasikia vijana wanasema ooohh nchi yetu ina mabadiliko, ohh tunapiga hatua. Lakini ukweli ni kuwa hatupigi hatua. Leo asubuhi nilijaribu kutafuta kitu ambacho ni made in Tanzania milmani city, iliniwia taabu sana, huwezi amini hata kiti moto inatoka afrika kusini. Tumepiga hatua nyingi sana kurudi nyuma, na hakuna anayejali. watu wanaona kuimport vitu tunavyoweza kuzalisha ni maendeleo.

by the way unajua kuwa bei ya mitumba Tanzania ni kubwa kuliko nguo mpya? na kuvaa mitumba ni more prestige than kuvaa nguo mpya.THIS IS TANZANIA.

100% you are correct. Huo ndio mtazamo wa atanzania wengi, nenda mwenge,Kariakoo,tandika,posta,kila kona ya mji huu ni mitumba tuuuuu!!!!!
Tunahitaji tuitishe sala ya kitaifa kuombea jamhuri hii maana inelekea upotevuni
 
Mwanakijiji
Mbona umelenga samaki tu. Tufanye analysis ya haraka haaka Tanzania inajito sheleza kwa kitu gani.

• Mchele , Sukari, Ngano Tunaagiza
• Juice za kwenye maboksi na Matunda halisi pia tunaagiza
• Maziwa ya ngombe tunaagiza na nyama za kwenye makopo. Idadi ya ngombe tulionao tunawazidi Botswana lakini wao wanatuzidi export sisi tunawazidi import
• Ukumbuke tulitaka kuagiza hata mvua
• Bidhaa za mbao, kama sofa, makabati hata viti vya kukalia wageni kwenye maofisi mengi ni kutoka nchi ambazo hazina hata misitu. Hata toothsticks tunaagiza.
• Kanga, mashuka,kanda mbili

Sasa cha kusikitisha zaidi sijui kama hata Ofisi ya Takwimu ina michanganuo yeyote kuhusu matumizi , mahitaji na uzalishaji wa bidhaa za chakula na nyinginezo kwa Watanzania. Hawa jamaa sijui kama wanajua umuhimu wao kwa Taifa. Hawa jamaa wakifanya homework zao issue na nyingine tunaweza kupata picha kamili
• Tujue hao samaki tunao export wanathamani gani na kiasi gani na tunaoimport wana thamani gani na kiasi gani vile vile
• Tujue matumizi ya ndani ya watanzania ni kiasi gani
• Tujue % kubwa ya wazalishaji wa samki wanaoingia kwenye soko ni wanatoka viwandani au ni wavuvi binafsi
• n.k

Inasikitisha leo hii ukitaka kuanzisha kiwanda kidogo cha tootstick huwezi kupata takwimu za matumizi ya bidhaa husika.
 
Back
Top Bottom