Video: Hotuba ya Sugu kwenye msiba wa Mwabulanga yawaacha wana CCM wakijiinamia kwa aibu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,911
2,000
Huyu mtu hajawahi kumung'unya maneno.

Hiki kilichotokea mbeya leo ni salamu tosha kwa CCM kwamba Sugu ni Rais wa mioyo ya wana Mbeya, pole sana Tulia haya yanatokea mbele ya macho yako chadema hua tunachana ukweli tu no kupepesa macho

 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,705
2,000
Hapa ndipo tumefika ambapo hata misiba inakuwa ni sehemu ya kupashana!
Si dalili nzuri kwa wale wanaoelewa!!!!!!!!!!!
Nadhani ni dalili nzuri, kifo ni mawaidha. Ni ukumbusho kuwa hapa duniani tu wasafiri,tutendeane wema katika nyanja zote za maisha.

Iwe kijamii, kisiasa na kidini.Marehemu alikuwa kiongozi wa siasa wa chama pinzani wa kanda, alipitia unyanyasaji mwingi sana na vitisho kwa walio na madaraka na dola. Leo amefariki wanakuja kuongea maneno ambayo walipaswa si tu kuyaongea wakati akiwa hai, bali kumtendea.

Kwa sababu amekufa, hawezi kujibu. Waliokuwa karibu naye akiwa hai wacha waongee na kufikisha ujumbe ambao angelikuwa hai, naye angeufikisha
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,513
2,000
Siasa zinatengeneza kitu kibaya Sana kwenye jamii

Inamaana hata kwenye msiba kunafanywa siasa?

Ni upumbavu ambao ukilelewa mwisho wake watu watatwangana makonde Mbele ya mwili wa marehemu,

Naomba kutumgwe Sheria ya kuheshimu na kutoleta mizaha kwenye misiba
 

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,698
2,000
Siasa zinatengeneza kitu kibaya Sana kwenye jamii

Inamaana hata kwenye msiba kunafanywa siasa?

Ni upumbavu ambao ukilelewa mwisho wake watu watatwangana makonde Mbele ya mwili wa marehemu,

Naomba kutumgwe Sheria ya kuheshimu na kutoleta mizaha kwenye misiba

Siasa kwa kifupi ni maisha ya watu ya kila siku sheikh

1. Utamaduni, ushirikiano na mahusiano
2. Shughuli za uchumi
3. Itikadi zetu kama taifa
4. Elimu
5. Afya
6. Mazingira
Nk

Huwezi kutenganisha siasa na utamaduni, mahusiano, uchumi nk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom