Video: Hivi ni kweli binadamu anaweza kupambana na mamba pasipo ndumba?

Traveller X

JF-Expert Member
May 2, 2017
271
500
Wadau nauliza hili kwa maana nimeona hii video ikimuonyesha jamaa wa huko cambodia akipambana na kumkamata mamba bila tatizo lolote, yani kama vile anakamata kuku, Hii kweli inawezekana au wanakua wamechanjia kidogo???
 
stable-negro

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
494

sasa huyo ni mamba au mtoto wa mamba...huyo si hata mtoto wa miaka 4 anamdaka vizuri kabisa
 
stable-negro

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
494
500
Unawajua mamba au unawaskia tu, hata awe mdogo kama mjusi bado atakutoa jasho tu
nawajua vizuri sana maana nimezaliwa na kukua karibu na mto....nilikua nawaona na bado naenda kuogelea; japokuwa kuna siku mwenzetu alidakwa na mamba ila sio kamamba hako ndugu
 
Mdakeo

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
556
1,000
Wanaoishi pembeni ya mito na maziwa wanajua siri iliyopo kati ya mamba na binadamu.

Wanadai mamba hawana ukorofi na binadamu labda uwachokoze.

Wanasema ukisikia mamba amefanya ukorofi ujue ametumwa.

Wakati fulani nilikua napita maeneo ya Korogwe niliwakuta watu wakichimba mchanga pembeni ya mto Pangani nikawahoji kuhusiana na mamba wao wakanieleza mamba wanapishana nao kama kawaida hapo wala hawana taabu, wakadai kuna mamba wa kufugwa na mamba wa kawaida, walidai kwamba wanao uwezo wa kumuita huyo, walichotaka niwape hela wakanunue udi kisha wamuite.

Kwa bahati mbaya si muumini wa mambo hayo nikawaaga na kuwashukuru kwa maelezo yao, niliwaachia pesa ya soda nikaondoka
 
mumak

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
958
500
Mamɓa akiwa ktk maji ndio anakua na nguvu sana kuliƙo nchikavu hivƴo ni timing tu,
 
Al-kindy

Member
Nov 11, 2017
33
95
Wadau nauliza hili kwa maana nimeona hii video ikimuonyesha jamaa wa huko cambodia akipambana na kumkamata mamba bila tatizo lolote, yani kama vile anakamata kuku, Hii kweli inawezekana au wanakua wamechanjia kidogo???
Yap inawezekana mkuu mbona hata wewe ukiwa unaishinao mara kwa mara unaweza tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom