Video: Halmashauri kuu ya TLP yampitisha Dr. John Magufuli kuwa Mgombea Urais 2020

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
724
1,421
Mrema anazeeka vibaya na kwa mipango hii 2020 kajihakikishia nafasi ya kuwa serikalini.

Chama cha TLP kimemteua Rais Dk @MagufuliJP kuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu 2020. M/kiti wa TLP, Augustino Mrema amesema Halmashauri Kuu ya TLP ilifanya uteuzi huo ilipokutana miezi 2 iliyopita. Amesema Rais huyu ni bora, tukimpoteza, hatupata mwingine.
EAQIrAIXUAEFFEC.jpeg
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,164
29,164
Mmh......

Haya yanapaswa yawe miongoni ya maajabu ya dunia, ambayo yanapaswa yaingie kwenye kile kitabu cha Guinness!

Kwa chama kinachojiita cha upinzani badala ya kumtaja mgombea wake wa Urais, wenyewe wamempitisha Rais Magufuli, kuwa mgombea wa urais, kwa tiketi ya TLP!

Wakati huyo Mwenyekiyi wa TLP, Augustine Lyatonga Mrema akitangaza hivyo, tunamjua Rais Magufuli kuwa bado yupo CCM
 

stinger_bug

JF-Expert Member
Jul 14, 2019
856
1,713
Mwenyekiti wa TLP Ndg. Augustine Lyatonga Mrema amethibitisha kwamba miezi miwili iliyopita Halmashauri kuu ya Chama hicho(TLP) ilikutana Na kumchagua/ Kumpitisha Dr. John Pombe Joseph MAGUFULI kua MGOMBEA wao wa URAIS mwaka 2020 kupitia Chama chao cha Tanzania Labour Part (TLP).
View attachment 1161805
Maskini Augustine Lyatonga Mrema. Akili zake zimeanza kuleta mushkeli.

Ni lini huyo waliyemteua aliomba? Hiki chama chao hakina katiba? Huyo waliyemteua alishaomba hata uanachama kwenye chama chao?

Mrema astaafu tu jamani. Tumwombee Mungu ampe afya njema na akili zimrudie huyu mzee wetu.
 

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
24,277
35,922
Chama chenyewe wako kumi na mbili nchi nzimaa.kila la heri mzee wa kirarachaa
 
16 Reactions
Reply
Top Bottom