Video: Halmashauri kuu ya TLP yampitisha Dr. John Magufuli kuwa Mgombea Urais 2020

Chama cha TLP kimemteua Rais Dk Magufuli kuwa mgombea wa urais kupitia chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema amesema Halmashauri Kuu ya TLP ilifanya uteuzi huo ilipokutana miezi miwili iliyopita.

Akizungumzia uteuzi huo amesema Rais huyu ni bora, tukimpoteza, hatupata mwingine. Hivyo ameeleza kuwa wanachama wa TLP na viongozi wake waishangaa CCM, kwani hawaoneshi kutambua mchango na utumishi uliotukuka wa Rais Dk Magufuli.

Ameweka wazi kuwa chama hicho kitamuunga mkono kwenye uchaguzi ujao.
Source: SwahiliTimes

FB_IMG_1563980903226.jpeg
 
Kwa maana hiyo kamati kuu ya ccm inatakiwa kumfukuza magufuli auanachama wa ccm, maana tayari ni mwnachama wa TLP na kashapitishwa kugombea urais kwa tiketi ya tlp
 
Huyu hapa Lyatonga Mrema akifafanua

Sisi kutokana na utendaji bora uliotukuka wa Rais wetu mpendwa Dr. Magufuli, Halmashauri kuu ya TLP ilikutana miezi miwili iliyopita na kumpitisha Rais Magufuli kuwa mgongea wa urais wa TLP 2020.

Sisi tutamuunga mkono huyu Rais bora, tukimpoteza hatuwezi kupata Rais mwingine kama huyu.
Misukosuko ni mingi mpaka kufukia uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda
 
Back
Top Bottom