Mkuu;
Nadhani sijakuelewa, wawepo kwenye bunge la burudani au kwa ajili ya burudani. Kule Uingereza walikuwepo watu wa aina hii wakiitwa Clowns. Nilidhani picha ya photoshop kwa kweli.
Ndungai una kazi kubwa. Hawa wanaachwa kuichangia bajeti ya nchi, wenye mawazo wanafanyiwa fitna watoke wawapishe hao. Nchi yangu ina kazi
Huyu msukuma ni mbunge anawakilisha chama gani? Kuna taarifa nimepata kuwa ni mbunge wa ccm; kama ni hivyo basi JPM na chama chake wana kazi kubwa kuhakikisha kuwa nchi yetu inakuwa na wabunge wenye hadhi na uwezo, na hili kulifanikisha over the long term ni lazima ccm ianzie na uchaguzi wa wabunge watakaowakilisha nchi kwenye bunge la Afrika Mashariki. Safari hii ni lazima nchi kupitia vyama vya siasa vijaribu kuteua wawakilishi wenye hadhi na uwezo watakaoendana na heshima ya nchi badala ya kuchagua watu kwa kufuata urafiki na majina lakini hawala uwezo, matokeo yake ni kuitia nchi aibu kwa tabia chafu na michango katika mijadala iliyo duni!!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.