VIDEO: Dr. Ulimboka; kwa kinywa chake mwenyewe! | Ambayo hukuyajua...

serikalini wapo wataalamu wa digital forensics lete mkanda original tujue kama haujawa doctored kukidhi matakwa yenu, hata mtoto wangu anaweza ku-edit mkanda akaweka sauti ya nyani dume, mnao mkanda orginal uwasilisheni kwa kamanda kova unafanyiwa forensics analysis kujua kama hayo yaliomo humo ya ulimboka, mara ngapi hapa zinatolewa sauti ya usama na inathibitishwa sio sauti yake, acha kushabikia usilolijua au utaalamu nalo huo mkanda tu kama mkanda mwengine na kwa taarifa yako haukubaliki mahakamani kama sehemu ya vielelezo ikibidi.

kapige mswaki kwanza
 
Pole zake kwa kweli... nasikitika tu kuwa hatuna guts za kufanya lolote, ingekuwa nchi za wenzetu pangekuwa padogo kwa Serkali.
Hapo ndo penye ukweli, halafu itaonekana kama tamthilia tu, then inapita, halafu unafuatia tu msamiati, ooh wataku "Uli" ooh "watakumwagepande", basi tunaishia hapo hadi tamthilia nyingine ije...
 
Mungu mwenye mamlaka juu ya haki, tawala, falme na enzi azidi kuinusuru na kuilinda roho ya Dr. Ulimboka.
 
Tunashukuru kwa hii clip Invisible, ndio nimemuona kwa mara ya kwanza live toka tukio. Hii inasikitisha kwa kweli... In some way hata Ulimboka alikuwa na makosa. Kuonana na mtu ambae hamfahamu vizuri usiku ni hatari saana ukizingatia nafasi, hali, demand na circumstances zake. Maybe ali undermine umuhimu wake, else naamini kabisa alitegeka kirahisi mno.

Pole zake kwa kweli... nasikitika tu kuwa hatuna guts za kufanya lolote, ingekuwa nchi za wenzetu pangekuwa padogo kwa Serkali.

nadhani sio kama hamfahamu mtu aliyekuwa anakwenda kuonana nae,mpaka wamekaa na kuongea na kutaka kuaga inamaanisha wanafahamiana vizuri sana,ndio maana waliweza kukaa na kuongea nae kwa muda,tatizo ni kwamba walidhani kuwa wangeweza kummaliza Dr na kupoteza ushahidi na walisahau kuwa Dr siku ile alikuwepo na rafiki yake ambae ni Dr Deo na bado angekuwa shahidi namba moja kama Dr uli asingeonekana ktk dunia hii
 
Damu ya mtu ni nzito kuliko maji kokote waendako itakuwa kama mzimu itawafuata tuu.Wangalijua laana ya damu ikoje wasingalifanya kitendo kama hiki.Tunamtakia kila Lakheri apone mapema Mungu yupo na walio wake siku zote.Sisi tuna Mungu, Wao wana msitu wa mwabopande na mibunduki.
 
serikalini wapo wataalamu wa digital forensics lete mkanda original tujue kama haujawa doctored kukidhi matakwa yenu, hata mtoto wangu anaweza ku-edit mkanda akaweka sauti ya nyani dume, mnao mkanda orginal uwasilisheni kwa kamanda kova unafanyiwa forensics analysis kujua kama hayo yaliomo humo ya ulimboka, mara ngapi hapa zinatolewa sauti ya usama na inathibitishwa sio sauti yake, acha kushabikia usilolijua au utaalamu nalo huo mkanda tu kama mkanda mwengine na kwa taarifa yako haukubaliki mahakamani kama sehemu ya vielelezo ikibidi.

Mkuu, mbona mkali! Dr si yupo hai! au!
 
Huu ni ukatili na uvunjifu mkubwa sana wa sheria.Naendelea kuwaza sababu na asili ya unyama huu kwa Dr. Uli......mara napata picha hii, kama serikali hii ya ccm haijalaani (hata indirectly) matendo ya serikali dhalimu ya Syria chini ya Ba'ath party basi hakuna shaka (indirectly) serikali hii ya JK wanaunga mkono unyama na uuaji wa Assad dhidi ya raia wa Shamu.Hivyo ni wazi kuwa lazima tujipange na kijizatiti kikweli ili kuing'oa ccm madarakani. We need iron resolves to push over the line.
 
nadhani sio kama hamfahamu mtu aliyekuwa anakwenda kuonana nae,mpaka wamekaa na kuongea na kutaka kuaga inamaanisha wanafahamiana vizuri sana,ndio maana waliweza kukaa na kuongea nae kwa muda,tatizo ni kwamba walidhani kuwa wangeweza kummaliza Dr na kupoteza ushahidi na walisahau kuwa Dr siku ile alikuwepo na rafiki yake ambae ni Dr Deo na bado angekuwa shahidi namba moja kama Dr uli asingeonekana ktk dunia hii
engmtolera umesikiliza vizuri mkuu? Kaulizwa hapo (thou haipo evident inatakiwa uwe makini) katika hio hio video kasema kuwa huyo jamaa hamfahamu. Aliwahi muona (take note sio kuonana) nae mara moja tu; kwenye mgomo wa madaktari ule wa awamu ya kwanza...

Hata hivo inaacha nafasi ya maswali.... Tuchukulie serkali ipo responsible...

  1. Ni kwanini walimuacha hai? Kwamba serkali watatuma mtu ambae ni amateur katika kazi kama hio? Au kwamba wameacha makusudi kama vile sending a message to fellow doctors?
  2. Katika hili ilaumiwe moja kwa moja Serkali? Au walaumiwe wananchi pamoja na Doctors walo baki? sababu ikichukuliwa evidently kuwa ni serkali na bado hakuna linalofanywa... bado basi tu watoto na hatujui la kufanya bali kuongozwa na baba hata kama mlevi unakubali tu kuwa ni baba.
 
Last edited by a moderator:
Kama walimfanyia hivyo ili walegeze msimamo wao, basi wamejustify msimamo wa madaktari na mapambano yao.Kama alivyosema pale airport, ni muhimu alichokuwa akipigania kiendelezwe, hilo ndo jibu la kwanza kwa unyama huu, then ni lazima kuwepo na uchunguzi huru, namwombea awe salama huko alipo, kwasababu inaonekana kuna mengi anataka kusema lakini hana nguvu bado.Mungu amlinde tuje kupata mkanda mzima kwasababu ni wazi anahitaji mapumziko.
 
Mkuu Invisible naomba uweke katika format ( eg VLC) tunayoweza kuona na sisi mimi natumia PC lakini hii clip
inanileta hii MSg

pixel-vfl3z5WfW.gif

The Adobe Flash Player or an HTML5 supported browser is required for video playback.
Get the latest Flash Player
Learn more about upgrading to an HTML5 browser

c udownload tu 10mb
 
Last edited by a moderator:
Dr Deo si anamfahamu huyo bwana? kwanini asikamatwe huyo aliyewaita ili waonane nae na ndio iwe chanzo cha upelelezi? na kama anatoka j je watu wa j hawalijui hili? hivi inawezekana huyo jamaa ajitokee pekee kama kichaa na kwenda kupanga maongezi na akina Uli?
kuna sintofahamu nyingi sana ktk hili swala
 
Hapo ndo penye ukweli, halafu itaonekana kama tamthilia tu, then inapita, halafu unafuatia tu msamiati, ooh wataku "Uli" ooh "watakumwagepande", basi tunaishia hapo hadi tamthilia nyingine ije...

hahaha... Umenifurhisha sana... umenikumbusha hapa karibuni kuna mtu wangu wa karibu alishindwa kufanya kazi na jamaa wasioaminika akisema anaogopa wasije "wakam-ulimboka"; hio isha pita jmushi1, tayari inatumika.
 
  1. Ni kwanini walimuacha hai? Kwamba serkali watatuma mtu ambae ni amateur katika kazi kama hio? Au kwamba wameacha makusudi kama vile sending a message to fellow doctors?
Mkuu kabla sijaona video ya jinsi walivyomjeruhi na maelezo yake, nilikuwa pia nikidhani kuwa hawakuwa na nia ya kumwua, lakini ukweli ni kwamba walitaka afe akiteseka zaidi, na pengine ndo maana hakwakumpiga risasi.Huyu sidhani kama walikuwa na nia ya kumwona akiwa hai tena, sidhani.
 
Asante invisible. Nashauri pia tuwekee na ile AC Msangi anaambiwa arudishe simu na waleti.
 
Back
Top Bottom