VIDEO - Chaja ya Simu Yatolewa Toka Kwenye Kichwa cha Mtoto

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,868
30,339
VIDEO - Chaja ya Simu Yatolewa Toka Kwenye Kichwa cha Mtoto
5977766.jpg

Chaja ya simu ikiwa imezama kwenye kichwa cha mtoto
Friday, September 30, 2011 2:31 AM
Madaktari wa nchini China wamefanikiwa kuokoa maisha ya mtoto wa mwaka mmoja ambaye alidondoka toka kitandani na kuangukia kwenye chaja ya simu ambayo ilizama kwenye fuvu la kichwa chake.
Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja aliwahishwa hospitali kwenye mji wa Qingyuan katika jimbo la Guangdong baada ya mama yake kumkuta akiwa amelala chari chini huku chaja ya simu ikiwa imezama kwenye kichwa chake.

Mtoto huyo alidondoka toka kitandani na kuangukia juu ya chaja ya simu ambayo ilikuwa pembeni ya kitanda.

"Baada ya kufanyiwa CT scan, chaja ya simu ilionekana imezama kwenye sehemu ya nyuma ya kichwa chake", alisema Dokta Li Guofeng ambaye pia mkurugenzi wa hospitali hiyo.

Madaktari walitumia masaa matatu kulifunua fuvu lake na kuindoa chaja hiyo.

"Mtoto huyu angefariki ndani ya sekunde chache kama mishipa ya damu kwenye ubongo wake ingepasuka", alisema daktari Li Guofeng.

Angalia VIDEO ya mtoto huyo chini. bonyeza hapa
VIDEO - Chaja ya Simu Yatolewa Toka Kwenye Kichwa cha Mtoto
<embed src="http://outlandishnews.com/wp-content/uploads/jw-player-plugin-for-wordpress/player/player.swf" height="315" style="width: 490px" allowscriptaccess="always" allowfullscreen="true" flashvars="&dock=false&file=http%3A%2F%2Foutlandishnews.com%2Fwp-content%2Fuploads%2F2011%2F09%2FChinese-baby.mp4&gapro.height=291&gapro.trackpercentage=true&gapro.trackstarts=true&gapro.tracktime=true&gapro.visible=true&gapro.width=560&gapro.x=0&gapro.y=0&image=http%3A%2F%2Foutlandishnews.com%2F%3Fp%3D826&mediaid=825&plugins=viral-2%2Csharing-1%2Ctweetit-1%2Cgapro-1&sharing.height=291&sharing.visible=true&sharing.width=490&sharing.x=0&sharing.y=0&tweetit.height=291&tweetit.link=true&tweetit.visible=true&tweetit.width=560&tweetit.x=0&tweetit.y=0&viral.allowmenu=true&viral.bgcolor=0x333333&viral.fgcolor=0xffffff&viral.functions=embed&viral.matchplayercolors=true&viral.oncomplete=true&viral.onpause=true">

<tbody>
</tbody>
 

Vinci

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
2,638
660
Dah!..Jesus christ. miugiza hii....ingekuwa ni bongo wangeichomoa pindi tuu mtoto alipoiangukia hiyo charger na hapo wangesababisha mishipa kukatika na ndio ungekuwa mwisho wa uhai wake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom