Video:Bob Marley album "Survival",mahubiri kila ukweli kuhusu Afrika na Wafrika

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,380
5,871
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nasikiliza sana nyimbo za Bob Marley bila ya kufahamu maana ya nyimbo na ujumbe wa nyimbo zake kwasababu nilikuwa sijui kingereza..

Leo hii nimeingia kwenye Youtube na kusikiliza hili album lake "Survival" kwa kweli nimeshangaa yale niliyoyasikia katika nyimbo zake,huyu jamaa naona alikuwa mtume

Bob Marley ni mtu ambae ninaweza kumuweka katika jumuia ya Watu kama akina Muhamad,Yesu...



Tafadhali poteza muda wako na usikilize mahubiri ya Bob Marley,na nini anabashiri,na nini kinatokea katika hizi zana za "Digital Technology" kama Bob Marley alivyobashiri...
 
Andika hapa hayo mashairi/mahubiri, wengine tunatumia simu za tochi.
 
Heshima Mkuu.

Watu, baadhi hatumsikilizi Bob Nesta Marley (R.I.P). Na siyo hatumsikilizi pekee, hatumuelewi alikuwa akiimba nini. Ni wachache tu kati yetu ambao wanaelewa ni mashairi ya namna gani alikuwa akiimba Bob Marley.

Upeo wake ulikuwa mkubwa sana. Siyo kama sie tunaaona Lugha kama mawasiliano, Bendera kama kitambaa chenye marangi rangi, Olimpiki kama michezo, Dini kama Imani, Rastafarians colours kama uhuni na orodha inaendelea..

Hakuwa msanii wa kubahatisha na wala hakuwa na bahati ya kuwa msanii. Taasisi ya Reggae ilikuwa na bahati ya kumpata msanii kama yeye.

Alikuwa msanii bora. Alifahamu nini anafanya. Hakuwa m'binafsi. Aliitazama dunia kwanza. Alijali utu na mengine mengi.

Narudi, kumradhi. Updates/postscrits.


Aliimba mengi, aliimba Ukweli, aliimba Ukombozi, Amani, Jinsi ya kujikwamua toka kwenye makucha ya kikoloni katika uchumi, fikra, siasa na utamaduni..

Ni wachache tu kati yetu wanaotambua ni kitu gani kinachomfanya Msanii awe Msanii. Namaanisha mtu asiyeweza kufa moyo; Mtu asiyeweza kukata tamaa.

Mtu asiyetegemea wengine wamfanye yale anayoweza kuyafanya yeye mwenyewe.

Mtu asiyemlaumu Mungu, asiyelaumu mazingira; Mtu asiyelaumu bahati mbaya kwa hali yake kimaisha.

Bali yule mtu awezaye kutoka na kujitengenezea mazingira yatakayomuwezesha kuishi.

Usanii siyo kuiga Umagharibi. Usanii ni kuuishi wewe, kuuenzi wewe, kuuimba wewe na kuuvaa wewe. Nje ya hapo wewe siyo msanii, Nb; kwa mantika ya Sanaa ni Lugha.

Emancipate yourself from mental slavery, non but ourself can free our mind- Bob Marley.

Overcome the devil with the things called Love-Bob Marley.

Ahsante, Thank you sana Bob Nesta Marley.
 
Jasusi wa CIA, Bill Oxley aliyekiri kumuua Robert Nesta Marley naye anakufa taratibu kitandani tena kwa maumivi makali sana. Hakika alifanya jambo la kusikitisha sana kwa mpigania haki. R.I.P Bob..
 
Wanamuziki wengi wa kizazi chake waliimba nyimbo haswa za ukombozi wa muafrika....wanamuziki wa kizazi hiki wengi wanatafuta pesa na hadhira inahitaji ujinga tu wa kuwafariji na shida nyingi zinazowasonga.....mimi nimetumia muda mwingi kuwasikiliza peter tosh na bob...peter tosh aliimba vya msingi vingi sana na alitunga sana....nyimbo zao ukizielewa zinaleta hisia fulani na hasira dhidi ya watu waliotutawala
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom