video: Balozi wa ufaransa aongea kiswahili, mwenyeji aongea kiingereza.. yaleyale!

PingPong

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
926
160
Balozi wa Ufaransa nchini juzi aliwaacha hoi wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu Tanzania na katibu mkuu wa shirika hilo Alhaj Adam Kimbisa kwa kutoa risala yake kwa lugha ya kiswahili tena kile kilichonyooka ile kinoma...wakati akikabidhi msaada wa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro .

Kilichosikitisha wengi ni Mwenyeji wake ambaye ni katibu mkuu wa shirika hilo Alhaj Adam Kimbisa...yeye aliongea kwa lugha ya kiingereza.

Je kwa style hii kiingereza cha nini kwa hotuba zinazotuhusu wabongo??
fungua hii link kwenye browser yako uone video..
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=Eg1UrtU2YSE&feature=player_embedded"]http://www.youtube.com/watch?v=Eg1UrtU2YSE&feature=player_embedded[/ame]

source: darhotwire.com
 
Miafrika ndivyo tulivyo, ulimbukeni na sifa zisizomsingi wala kuhitajika!!
 
Hahahahaha....that's what's up bwana balozi. Yaani Kiswahili swaaafi kabisa na lafudhi ni nzuri kabisa. Ingawa sijaona popote kwenye hicho kipande ambapo huyo Mtanzania aliongea Kiingereza, lakini kama alifanya hivyo basi na aone aibu.
 
na hicho kingreza chenyewe nakitilia mashaka sijui kitakuwa kilifananaje??!!
 
......Huyo mtanzania naye mashauzi tu.

nafikiri labda mtz aliongea kiingereza kwa sababu kulikuwa na watu wa mataifa mbalimbali,lakini kwa mfaransa,mjerumani ni bora aongee kiswahili kuliko kiingereza
 
nafikiri labda mtz aliongea kiingereza kwa sababu kulikuwa na watu wa mataifa mbalimbali,lakini kwa mfaransa,mjerumani ni bora aongee kiswahili kuliko kiingereza

Sounds like a good excuse. Very interesting indeed, basi mfaransa naye angeongea lugha hiyo ya watu wa mataifa mbalimbali.
 
Sounds like a good excuse. Very interesting indeed, basi mfaransa naye angeongea lugha hiyo ya watu wa mataifa mbalimbali.
Iliwahi kunitokea ila mie ilikuwa tofauti kidogo ila baadae nilicheka sana, ilikuwa Karagwe huko miaka flani nimemsindikiza consultant toka Makerere University tunazunguuka huko ndani ndani huko vijijini, sasa consultant yeye ndio alikuwa mtafsiri wangu akiongea na wananchi ananitafsiria kwa kiingereza au wananchi wananitafsiria kwa kiswahili. Consultant alikuwa Mnyankole wa Uganda na wananchi ni Wanyambo wa Karagwe, Tanzania (kimsingi lugha zao zinaingiliana kwa kiasi kikubwa kasoro maneno machache hivyo jamaa alikuwa anateremsha Kinyankole wananchi wanapiga Kinyambo alafu wanafsiri kwangu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom