Video: Azimia jukwaani baada ya kutumbuliwa na Makonda

Nimesikitika na kuhuzunika sana nilijaribu kuwa ktk viatu vya huyu mkuu wa idara wallah imenisononesha. Inawezekana kuna majibu mazuri angeweza kuwa nayo na pengine ni mtendaji mzuri aliekosa kueleza anayoyataka muheshimiwa. Najua kuna uwezekano mkubwa wa huyu mkuu wa idara kukosea data lkn haikupasa afanyiwe haya. Tunao utaratibu maalum wa kushughulikia mambo kama haya. Hivi tujiulize kama mkuu wa mkoa angewapa nafasi ya kumpa data kamili ingeharibu nini. Kisha nashindwa kuelewa hivi kila lalamiko ni mgogoro? Maana kama nimesikia vizuri mkuu wa idara kaulizwa kuhusu Migogoro na si malalamiko ambayo mkuu wa mkoa anatakwimu zake. All in all RC hakuitendea haki nafasi yake. Hakuthamini thamani ya utu wa mtu kwani hata pale mtu alipoanguka bila kujua amepata athari kwa kiasi gani aliimba nyimbo kuonesha alichokifanya yuko sahihi. Wananchi pia wamenifedhehesha sana wakati mtu ameanguka akipigania uhai wake watu wamekosa ubinaadamu wakaanza kushangilia... Upo wapi upendo wetu....
Wale walioshangilia ni binadamu siyo " watu"!
 
Wenzako wamesoma kwa bidii , wewe unawatumbua....... Ni vyema kukumbuka vyeo vya kisiasa ni vya msimu, kwa hiyo busara na hekima inatakiwa kutumika ili kutatua kero za wananchi na wala sio vyema kucheza na majukwaa.
Kama unaamini wewe ni msomi na bado unaendelea kuongozwa na mtu unayeamini siyo msomi na anakidharirisha basi wewe ndiyo mjinga kwanini usijiajiri??
 
Wadau kuweni na huruma, Kuna watu humu nahisi hawajawahi kuwa watumishi wa serikali ndio maana wanacomment hivyo. Kuwa MKUU wa idara ni lazima uwe Afisa Mwandamizi, maana upo kazini zaidi ya miaka 7 ukiwa AFISA na pia lazima vetting ikubali, yaani watuflani wakubali utendaji wako ndipo hupewa ukuu wa idara. Huyu MZEE ni mkongwe kazini, anajua kazi lazima ana zaidi ya miaka 15 kwenye field yake, katoa data za ukweli alizonazo, tena katiririka vizuri sana kwa kweli. Rc naye anadata zake kadiri ya vyanzo vyake, hivyo si lazima zilingane kwa kuwa baadhi ya watu huenda wa wameripoti tu upande mmoja. Na wananchi wanashangilia tu, na wengine mnachukulia mlivyotendewa na kufurahia hili tukio, kweli??? Binafsi nimetumia sana.
 
Afu anajifanya eti yeye ni mcha Mungu aliyetukuka...
Afu nasikia amepondea mahakama kuwa "mahakama zinajifanya hazitaki kuguswa kwa kisingizio cha kuwa mhimili mwingine, zimechukua nafasi ya Mungu na yeye ni mteule wa Mungu hivyo lazima aziseme"
 

Attachments

  • IMG-20180210-WA0113.jpg
    IMG-20180210-WA0113.jpg
    48.5 KB · Views: 32
. Najua kuna uwezekano mkubwa wa huyu mkuu wa idara kukosea data.

Hapo mimi ntakupinga. Huwezi kuwa na takwimu ulizojitengenezea mwenyewe then hizo ndo zitumike kunihukum ukaacha takwimu zangu za ofisini kwangu. Twende mahakamani ndo itaamua takwimu sahihi ni zipi?
Tukiintatein hii tabia ya viongozi kuja na takwimu zao mfukoni hakuna alie salama
 
Afu nasikia amepondea mahakama kuwa "mahakama zinajifanya hazitaki kuguswa kwa kisingizio cha kuwa mhimili mwingine, zimechukua nafasi ya Mungu na yeye ni mteule wa Mungu hivyo lazima aziseme"
Huyu Dogo anapaswa kupimwa akili asee...

Hakyamama wallah!!
 
Huyu mkuu wa Idara anastahili kutumbuliwa.... Hana uwezo wa kukabiliana na Changamoto.

Kama mkuu wa mkoa tu anazimia.... Akija waziri atakufa moja kwa moja.. Hapo bado hajaja Waziri mkuu ama Raisi.


Hivi hawa wanaojiita Wasomi wana matatizo gani ktk vichwa vyao?
 
Kuna watu ni wajinga na watumwa wa elimu zao, huwezi kuniita kuniuliza maswali ya kijinga mbele ya watu halafu utegemee nikujibu unavyotaka wewe tena mambo muhimu sana yanayohitaji umakini wa kuyajibu.
Hii imla wanayofanyiwa na kumchekea huyu ni upuuzi na udhalilishaji mkubwa, kama waliajiriwa wafanye kazi majukwaani ingekuwa vizur, kuna watu wanatakiwa wafatwe ofisini kwao waulizwe kupitia takwimu walizo nazo kwenye mafaili na sio kuulizana mbele za wati tena wanaoshangilia na kuzomea.
Utendaji wa aina hii uliisha baada ya vita kuu ya pili ya dunia na hapo tukawapoteza kina Hitler na kuanza ustaarabu mpya wa kuongozana.
 
Back
Top Bottom