VIDEO - Azifunga Kufuli Sehemu za Siri za Mkewe ili Asitoke Nje ya Ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIDEO - Azifunga Kufuli Sehemu za Siri za Mkewe ili Asitoke Nje ya Ndoa

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Oct 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  <tbody>[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG]
  Sitabai Chouhan akiwa hospitali baada ya jaribio lake la kujiua[/TD]
  [TD]Mwanaume mmoja wa nchini India ili kumlinda mkewe asitoke nje ya ndoa aliutoboa uke wa mkewe na kuufunga kwa kufuli kila alipokuwa akimuacha peke yake huku funguo za kufuli hilo akitembea nazo akiwa amezificha kwenye soksi anazovaa.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Kwa miaka minne iliyopita, Sohanlal Chouhan, mwanaume mwenye umri wa miaka 38 wa Indore, India alikuwa akiufunga kwa kufuli uke wa mkewe kila alipokuwa akienda kazini ili kumlinda mkewe asitoke nje ya ndoa.

  Kwa mujibu wa polisi, uchunguzi wa polisi ulianzishwa mwezi julai mwaka huu wakati mke wa Sohanlal aliyejulikana kwa jina la Sitabai Chouhan, alipowahishwa hospitali ili kuokoa maisha yake kufuatia jaribio lake la kujiua kwa kunywa sumu ya panya.

  Madaktari walikuwa wanajiandaa kuingiza mrija kwenye sehemu za siri za Sitabai ili kusaidia kunyonya sumu ya panya toka kwenye mwili wake wakati walipogundua kuwa uke wake ulikuwa umefungwa kwa kufuli.

  Iligundulika kuwa Sohanlal Chouhan alianza kuliweka kufuli kwenye sehemu za siri za mkewe miaka minne iliyopita kwa kuhofia mkewe angemsaliti na kutoka nje ya ndoa.

  Wapelelezi walisema kuwa Sohanlal alifanikisha zoezi lake la kuweka kufuli kwenye uke wa mkewe kwa kumlewesha mkewe na kisha kutumia sindano kutoboa matundu mawili kwenye kuta mbili za uke.

  Kufuli dogo lilipitishwa kwenye matundu hayo na lilikuwa likifungwa kwa ufunguo kila siku asubuhi wakati Sohanlal alipokuwa akitoka kuelekea kazini.

  Kwa kuwa siku zote Sohanlal alikuwa akiondoka na funguo za kufuli hilo, madaktari walishindwa kumpatia tiba ya kutosha hadi mumewe alipolazimishwa atoe funguo ili kulifungua kufuli hilo.

  Polisi walisema kuwa Sohanlal alikuwa ameificha funguo ya kufuli hilo kwenye soksi wakati alipokamatwa na kutiwa mbaroni.

  Sohanlal amekiri kosa lake akidai kuwa alilazimika kufanya hivyo kwakuwa wanawake wengi kwenye familia yake walikuwa si waaminifu kwenye ndoa zao.

  Sitabai ambaye amefanikiwa kuzaa watoto watano na Sohanlal ilidaiwa kuwa aliamua kujiua baada ya kugundua kuwa Sohanlal alikuwa akiisaliti ndoa yao.

  Sohanlal alitupwa rumande na kufunguliwa mashtaka ya kufanya shambulio la kudhuru mwili.

  Angalia VIDEO ya tukio hilo chini.

  [/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...