Video: Azam TV tunzeni heshima yenu, hivi ni vitasa feki

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
1,340
2,000
Kwanza hongereni sana kwa kuleta revolution ya tv hapa bongo. Soka mmefanikiwa, bongo movies pia naona mnakomaa na ndondi pia mmeamua kutuletea.

Ila dah ndugu zangu kilichotokea Dodoma kwa Dulla Mbabe ni uhuni. Ni kama vile mnashirikiana na matapeli kuokota walevi mnawaleta hapa waje wapigane wachukue hela tu!

Yaani mwezi mzima mna-hype pambano bila hata kuangalia backgrounds za hao wapiganaji. Kweli Mwakinyo alikuwa sahihi alivyosema kuna watu wanapigana na walevi toka nje ya nchi.

Hebu angalia knockout ya Dullah Mbabe, ngumi ya bega moja tu mkenya chali keshachukua hela yake.

SaidAlly

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
2,271
2,000
Naona mnaongea kwa hisia lakini hamjui mchezo wa ngumi
Nakubaliana na wewe kabisa.

Nashangaa hata wale wachambuzi ambao nao ni maboksa kabisa wameshindwa kuona ngumi 2 za haraka mwanzo ambazo moja ya kulia ilimpata kwy kidevu, ya pili ilipiga juu kichwani.

Kwa kawaida kama bondia yuko vizuri, hizo punch 2 zinakata kabisa stim, sema mkenya ni mzoefu na mgumu ndio maana aliendelea kuguard....

Uzito wa ngumi ya 4 ambayo jamaa alidondoka ni sababu jamaa aliisha lewa...lakini pia angalia ilivyo mrusha japo aliiguard...mkenya yuko sahihi alipima ule uzito na hali yake ya kurecover akaona akirudi hata kuwa na guard ya kuhimili bora ajiokoe

Mie naona Dulla kashinda kwa uwezo wake mkubwa na Mkenya kama alivyosema kuna kesho hakuona sababu ya kwenda kwy matibabu makubwa endapo angeendelea maana angeweza kupigwa knockout kali sana
 
adriz

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
1,193
2,000
Kabla ya ile ya bega Mkenya alipokea za uzani mbili tatu za fasta ila yote kwa yote hakuwa bondia mzuri ,Kongole kwa Dula Mbabe .
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
5,529
2,000
Kwanza hongereni sana kwa kuleta revolution ya tv hapa bongo. Soka mmefanikiwa, bongo movies pia naona mnakomaa na ndondi pia mmeamua kutuletea.

Ila dah ndugu zangu kilichotokea Dodoma kwa Dulla Mbabe ni uhuni. Ni kama vile mnashirikiana na matapeli kuokota walevi mnawaleta hapa waje wapigane wachukue hela tu!

Yaani mwezi mzima mna-hype pambano bila hata kuangalia backgrounds za hao wapiganaji. Kweli Mwakinyo alikuwa sahihi alivyosema kuna watu wanapigana na walevi toka nje ya nchi.

Hebu angalia knockout ya Dullah Mbabe, ngumi ya bega moja tu mkenya chali keshachukua hela yake.

Ndio tabia za Wakenya kufanya utapeli au wizi. Kimsingi yule Mkenya hakuwa tayari kupigana. Alipohojiwa akawa anasema kuanzia asubuhi mwili wake haukuwa vizuri.
 
Gwele

JF-Expert Member
Jun 7, 2016
1,164
2,000
Hebu waende wakapigane nje kwanza tumechoka na maigizo yao yaani mchezo ukianza 100% unajua mbongo atashinda hivi huku mhindi hayupo tumpige hela kiurahisi?
 
Franky Samuel

JF-Expert Member
Oct 10, 2018
633
1,000
Mim tangu niangalie lile pambano la twaha kiduku na yule Thailand (sijui) nikaona jamaa mweupe analeta ukatuni ulingoni sijakaa niangalie tena huu upumbavu
 
0ozg Tz

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
1,622
2,000
Toka nianze kufatilia Haya mapambano kwa tv ya azam,IBRA class ndo bondia pekee ambae alikuwa na mshindani wa kweli hao wengine sijui wakina Mwakinyo,kiduku huwa wanaletewa mabondia wakawaida sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom