VIDEO - Aweka Rekodi Ya Kumeza Majambia 18

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
4051694.jpg

Chayne Hultgren akiweka rekodi ya dunia kwa kumeza majambia 18 Wednesday, February 10, 2010 1:06 AM
Mfanya shoo za mitaani wa nchini Australia ameweka rekodi ya dunia kwa kumeza majambia 18 kwa wakati mmoja. Angalia video ya rekodi hiyo mwisho wa habari. Chayne Hultgren, mfanya shoo za mitaani wa nchini Australia mwenye umri wa miaka 31, ameingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia baada ya kufanikiwa kumeza majambia 18 kwa wakati mmoja.

Chayne alifanikiwa kuweka rekodi hiyo kwa kuyaingiza tumboni mwake majambia 18 yenye makali kama kiwembe ambayo yote yalikuwa na urefu wa sentimeta 72.

Chayne ambaye ni maarufu kwa jina la "Space Cowboy" aliivunja rekodi aliyoiweka yeye mwenyewe mwaka 2008 alipomeza majambia 17.

Chayne anawaonya watu wanaotaka kuvunja rekodi yake kuwa yeye alijiandaa miaka mingi sana kuweza kuweka rekodi hii.

Chayne anasema kuwa alianza usanii wa kumeza majambia alipokuwa na umri wa miaka 16 alipofanikiwa kulimeza jambia moja.

"Nimekuwa nikijiandaa kuweka rekodi hii tangia nilipokuwa na umri wa miaka 16", alisema Chayne.

Chini ni VIDEO ya rekodi hiyo. GONGA HAPA KWA PICHA ZA REKODI YA KUMEZA MAJAMBIA

VIDEO - Aweka Rekodi Ya Kumeza Majambia 18 Bonyeza hapa kuiona Video http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4051694&&Cat=2
 
Back
Top Bottom