VIDEO: Alichozungumza Dr Slaa na Watanzania DMT na majibu ya swali kuhusu Bwn Sohooba Keith Smith

Slaa akivaa suti anaonekana mtu mstaarabu wa kawaida. Aliyemshauri asivae magwanda kafanya vizuri.

Unamhusudu sana Google uone kama ameanza kuvaa suti kwa safari ya marekani au huna mlo leo kwa kumtaja unapata book saba mara mbili, gwanda atalivaa kwa sababu ni mamuuzi yake
 
Mkuu hawa CCM followers hili haliwezi kuwaingia akilini nimewaambia watuwekee hapa tujue Mwigulu alizungumza nini hakuna anayerespond.... wanabisha hata kwenye mambo ya msingi wakisahau hapa ni utaifa kwanza
wala ucpoteze muda wako, wanajua sana wanachofanya, wala siyo bahati mbaya! wanajua mwigulu atakuwa ameongea utumbo wakutosha na wana chofanya nikupiga propaganda ili waenelee kuwa madarakani, lakini wanajua watu wameisha wachoka sana tu....
 
Slaa akivaa suti anaonekana mtu mstaarabu wa kawaida. Aliyemshauri asivae magwanda kafanya vizuri.

Wewe ukikutana na uzi unamzungumzia Dr Slaa lazima utakaa humo unapost hata masaa 10 kuuharibu ili maana ya uzi wenyewe isijadiliwe. Kwa taarifa yako hata kama tunaficha ID zetu za kweli bado tufanyapo ujinga tujionee aibu kama watu timamu. Una jua mtu mwenye akili timamu hata kama yuko peke yake AKIJINYEA anaona aibu ingawa hakuna aliyemuona. Au wewe ni tofauti?
 
Wewe ukikutana na uzi unamzungumzia Dr Slaa lazima utakaa humo unapost hata masaa 10 kuuharibu ili maana ya uzi wenyewe isijadiliwe. Kwa taarifa yako hata kama tunaficha ID zetu za kweli bado tufanyapo ujinga tujionee aibu kama watu timamu. Una jua mtu mwenye akili timamu hata kama yuko peke yake AKIJINYEA anaona aibu ingawa hakuna aliyemuona. Au wewe ni tofauti?

Kwahiyo unamaanisha Slaa amejinyea au?
 
Slaaa ameanza kuongea story za kiijiweni!!! Ukiona mtu mzima kama Slaa anazunguka mitaani kunadi hadithi feki kuwa Rais aliamuru ndege iende china kumuokoa mtuhumiwa wa madawa ya kulevya ujue ameshiwa hoja.

Mkuu, hivi kuna kitu gani alichokisema Slaa ambacho ni kipya kinachoednana na gharama ya tiketi ya business class aliyolipiwa yeye na Josephine? Ndio amekuja kusimulia story za vijiweni?

Tanzania diaspora ni jamii pevu. Haina muda wa kusikiliza porojo za namna hiyo. Mshaurini Slaa atumie muda mwingi kuzungumza kuhusu workable solutions kuliko kuongea porojo za vijiweni kama hizo.
...mbona amezungumza - ulikuwa unalala? workable solution ni kuuondoa mfumo mzima wa wezi serikalini. Unapokuwa na rais (aka mwenyekiti wa CCM) muuza madawa ya kulevya, katibu mkuu wa chama -JANGILI. Workable solution hapo ni kuung'oa mfumo mzima tuliokoe taifa.
 
Kama Dr. Slaa amefikia hatua anajifananisha na Mwigulu basi mwisho wake umeshafika rasmi. Mwigulu ameanza siasa mwaka 2010, just 3 years ago. Before that there was nobody with such a name in Tanzanian politics. Slaa kaanza siasa lini? Mtu aliyegombea Urais anapojifananisha na mtu ambaye cheo pekee cha dola alichowahi kugombea ni Ubunge basi kuna tatizo hapo.

Mwigulu yuko katika ascending phase ya political career where as Slaa is in stagnat or discending phase. Jikumbushe ile curve ya kuzaliana kwa bacteria.

Kweli Dunia hii ina watu! Hata kama nikutafuta nafasi yoyote serikalini au kuutaka hou UDC nafikiri hizo arguments hazikupeleki kokote. jiangalie sana hasa USONI MWAKO NA UJARIBU KUWAZA MAMBO MAWILI TU UONGO NA UZUSHI!
 
Mkuu ZeMarcopolo,

Hii hoja yako ya kusema Josephine amefungua kikao kama nani, nimeipenda mno.

Jana niliweka thread hapa JF ya kuhoji kuhusu huyo mwanamke kushirikishwa kwenye vikao au mikutano ya CHADEMA. Lakini cha ajabu thread ikafutwa na Mods baada ya Dr Slaa kushinikiza uzi huo ufutwe, maana uzi haukuwa na kasoro yoyote kuwepo JF.

Yani ni upuuzi wa kupitiliza wa kumtumia mke/hawala kwenye vikao vya kiofisi kwa namna yoyote ile (with exception of campaign of course). Kama ni shughuli za kiofisi inapaswa protokali izingatiwe na sio kufanya mambo kienyeji enyeji tu.

Nikiri tu kuwa kitendo cha Josephine kufanya ufunguzi wa kikao cha CHADEMA kimeshusha hadhi ya chama kwa kiasi kikubwa sana na ni muendelezo wa Dr Slaa kufanya blunders za kitoto kwenye siasa zake.

Tungekuwa tunajadili issues badala ya watu nafikiri tungekuwa tunasaidiana sana sisi kwa sisi na kuwasaidia sana hawa viongozi kina JK, Kinana, Nchemba na hata huyu huyu Dr Slaa mnayemwogopa sana ninyi kina Hamy D na wenzio ktk CCM.Hebu cheki hiyo ktk red bold; Una uhakika kabisa kuwa Dr Slaa "aliwashinikiza" mods wafute uzi wako? Who is Dr Slaa ktk jukwaa hili? Ni mmiliki wa Forum hii? Kama siyo sasa atashinikizaje kufuta jambo linaloletwa ili lijadiliwe na wana - forums?.....Mimi nafikiri tu kuwa labda hoja yako ilikuwa na kasoro na kutokidhi au kukiuka vigezo vya kuwepo jamvini.......labda ni uongo, au uzushi tu nk

By the way hiyo ktk blue bold umetumia neno "NAKIRI" ktk aya ya mwisho ya bandiko lako na kama ulivyomaliza kwa kujikanyagakanyaga, mimi binafsi ningependa kujua wewe ni nani kwani ktk CDM? Kiongozi, mwanachama hai au mkosoaji tu wa chama cha CDM na hasa Dr Slaa??

Mwisho kabisa, nikuulize swali hili; Umemtazama na kumsikiliza kwa makini Dr Slaa katika video hiyo? Umemwelewa? Bila kujali kama alikuwa na watu au hapakuwa na watu aliokuwa anaongea nao,kikao kilifunguliwa na Josephine au na wewe.....lililo muhimu ni kuwa,wewe na mimi ambao ni watu pia tumemwona na tumemsikia. Una maoni gani juu alichokisema (hoja zake na si yeye kama Dr Slaa)? Kuna alichokisema ambacho si cha kweli, uongo? Ukweli ni upi sasa kwa maoni yako?......

Ukininiuliza mimi juu ya mtu huyu ....... Dr Slaa nitakupa jibu moja tu kuwa ni kati viongozi wachache sana nje ya serikali ninaowahusudu kwa sababu ni jasiri na ana kila quality za A GOOD LEADER na kwa yote aliyoyasema hapo ktk video, ndugu yangu hiyo ndiyo hali halisi ya Tz yetu na viongozi wetu hawa chini ya JK!!!
 






-------------------------------------


Inashangaza sana umakini wa Dkt. Slaa. Anashangaza sana. Slaa anadiriki kutamka maneno ya kumtetea Sohoba, lakini hazungumzii kosa alilolifanya Bw. Sohoba hadi kuhukumiwa kufa nchini. Nina hakika, Dkt. Slaa anamtetea Sohoba kwa kuwa makosa ya Bw. Sohoba yanafanana na makosa na mienendo ya Dkt. Slaa.


Bw. Sohoba alikuja nchini akijiita mwekezaji. Akanunua shamba na kujishughulisha na kilimo. Bw. Sohoba alipata matatizo na kushitakiwa baada ya kuua. Bw. Sohoba alikuwa akitembea na mke wa shamba boy wake. Siku ya tukio, mwenye mume akamkuta Bw. Sohoba akizini na mkewe. Katika kumkurupusha, na katika purukushani hiyo, Bw. Sohoba akamuua mume wa mw amke huyo. Akashitakiwa na akaonekana na hatia na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa. Katika kesi yake, alikuwa na mawakili waliomtetea ambao ndio aliwakabidhi mali zake.
Kama kuna kosa ambalo Serikali ya Awamu ya Pili ilifanya ni kuruhusu Sohoba aondoke nchini. Serikali yake ya Trinidad and Tobago ilimuombea msamaha. Akasamehewa na Rais Mwinyi kwa sharti kuwa aondoke nchini na asiruhusiwe kurejea tena (persona non grata). Akaondoka na kupotea na kuibuka wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu akiwa na madai ya kurejeshewa mali zake. Ajabu, madai yake hayo anaidai serikali ambayo hakuikabidhi mali yake. Tangu lini Serikali ikasimamia mali za wafungwa?
Bw. Sohoba akaendelea kuoita huku na huko akitukana nchi yetu na mahakama kuwa zimejaa rushwa na kumdhulumu shamba lake. Eti, serikali imeruhusu watu aliowaachia mali zake kuziuza na kumdhulumu. Serikali haina jukumu hilo na haijawahi kuwa na jukumu hilo. Mali za mhalifu hubaki mikononi mwa jamaa zake au wanasheria wake. Serikali hiyo hiyo anayoitukana ikampa fursa nyingine ya kumuondolea kwa muda kikwazo cha kuingia nchini ili aje na wanasheria wake ashughulikie mali yake lakini ameshindwa kuitumia fursa hiyo. Ni kipi zaidi kiumbe huyu atendewe na serikali? Tena Serikali ambayo imepoteza raia wake kutokana na kitendo cha kinyama alichofanya Bw. Sohoba kwa mtanzania?
Inanishangaza sana kiongozi aliyewahi kugombea Urais anajihusisha na kumtetea Bw. Sohoba na kuilaumu Serikali. Ningemuelewa angekuwa aidha anamshawishi Bw. Sohoba awe anatuma fedha nchini kusaidia familia yake ambayo inaishi kwa shida, amshawishi Bw. Sohoba kuangalia familia ya Mtanzania aliyemuua kinyama kwa kutetea haki yake ya kindoa, na kwa mahaba aliyokuwa nayo kwa Sohoba, angemshawishi basi aje Tanzania kufuatilia hizo mali zake kwa kufungua kesi mahakamani dhidi ya waliomdhulumu.
Ninachoweza kuelewa ni kuwa, Dkt. Slaa anamtetea Bw. Sohoba kwa kuwa makosa aliyofanya yanafanana na yale anayoyafanya yeye ya kuvunja ndoa za watu, kuasi kiapo cha dinina vitendi vya namna hiyo. Huyu ndio kiongozi wa kitaifa!
 
Last edited by a moderator:
Kama Dr. Slaa amefikia hatua anajifananisha na Mwigulu basi mwisho wake umeshafika rasmi. Mwigulu ameanza siasa mwaka 2010, just 3 years ago. Before that there was nobody with such a name in Tanzanian politics. Slaa kaanza siasa lini? Mtu aliyegombea Urais anapojifananisha na mtu ambaye cheo pekee cha dola alichowahi kugombea ni Ubunge basi kuna tatizo hapo.

Mwigulu yuko katika ascending phase ya political career where as Slaa is in stagnat or discending phase. Jikumbushe ile curve ya kuzaliana kwa bacteria.

ZeMarcopolo kama kawaida yako na umbea wako ni vema sasa ukaitwa DOMO KAYA post zako zote za kikekike tu, hata hivyo yawezekana hiyo ndiyo jinsia yako.
 
Back
Top Bottom