Video ajali ya ndege - maisha ya watu aliyookolewa Poland | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Video ajali ya ndege - maisha ya watu aliyookolewa Poland

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Nov 2, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
 2. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Jamaa walikuwa na bahati sana sana. Huyo Pilot ni jamaa mzoefu sana sana katika kuendesha ndege.

  Ameshaendesha sana hizi ndege zisizo na engine ziitwazo Glider (Sailplane) na huko akawa mzoefu mzuri.

  Kumbuka kuwa hizo ndege za Glider huwa hazina matairi na hivyo kwake ilikuwa ni kama kazi ya kila siku.

  Uwanja wa ndege wa Okecia (Choppin Air port) ni uwanja pekee wenye huduma ya kupokea "Majeneza" kama hili kwenye video.

  Kabla ndege hajatua, waliunguza kwanza mafuta angani wakiwa chini ya muongozo wa F-16 mbili. Baada ya kuwa wamshindwa kabisa kushusha matairi basi uamuzi ukapitishwa na barabara ya kutua ndege ikamwagiwa mapovu na watu wa fire Brigade na kitu kikaja kikateleza na kutua salama.

  Hakuna aliyeumia na wote wametoka salama kabisa. Ndiyo maana binadamu tunaishi sana maana ajali kibao watu wanapona.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG][SUP]​[/SUP]
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Duh ilikua ni bahati yao hao abiria kunusurika!
   
 5. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nadhani wengine walikuwa wanasali, wengine wanatubu, wengine walilia, wengine mkojo na mashuzi vinaponyoka, ili mradi humo ndani hali ilikuwa mbaya mbaya! Poleni sana kwa msukosuko huo!
   
 6. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wasiwasi zaidi ulikuwa kwa ndugu na jamaa waliokuja kuwapokea uwanjani mara baada ya kuona ndege inapitiliza na hakuna information. Jamaa walipofika Warsaw, walitoa taarifa mapema kuwa wana matatizo na jamaa walianza kuwazungusha karibu na Airport kama saa nzima hivi ili kuchoma na kumwaga mafuta. Muda huo juhudi zilikuwa zinafanywa ili matairi yatoke.'

  Mwisho walifanikiwa kufungua ule mlango unaoficha matairi na wakategemea kuwa yataanguka yenyewe kwa gravitation. Muda huo tayari uwanja ulishaandaliwa kwa kuweka mapovu ili watue kwa tumbo mara matairi yakishindwa kushuka yenyewe. Iliposhindikana kukawa hakuna tena muda wa kusema warudie tena kutua. Dakika kama tano kabla ndiyo abiria wakaambiwa kuwa kutakuwa na kutuwa kwa dharula na wajikunyate kwenye viti vyao. Hawakujua nini hasa kilikuwa kinaendelea.

  Baada ya kutua, ni mama mmoja tu alilalamika kuwa kidogo ndege ilikuwa ikigongagonga. Baada ya kuona milango inafunguliwa na godoro linawekwa,wengine ndiyo wakaja kujua kuwa wametua kama jeneza (bila matairi).

  Wengi walipata mshtuko baada ya kuwa wametoka nje na kuona jinsi walivyotua. Rubani ni mzuri sana na anakiri kuwa kwenye SIMULATION, ametua sana bila matairi na kwake ilikuwa na kama mazoezi kwenye simulation. Nafikiri waliosaidia ndege kutua salama zaidi walikuwa watu wa uwanjani pale na zaidi ni FIRE BRIGADE walioweka povu kubwa uwanjani kwa dakika 15 tu. Wafanyakazi ndani ya ndege nao walifanya kazi safi sana kwani ilichukua dakika chache sana, watu wote wakawa wameshatoka.

  Kama kulikuwa na mzamiaji, angeliweza kuzamia kabisa maana wengi walikuwa hawana documents..... :)

   
 7. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Mh!!Nahisi mle ndani ilikuwa patashika nguo kuchanika!!!watu wamesali mpaka sala zao za mwisho
   
Loading...