Victoria simon wa harusi yetu maisha magic bongo huyu dada nampenda sana anaejua jina analotumia instagram anijulishe

donga

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
1,197
2,000
Victoria Simon, mtangazaji mpya wa Harusi Yetu!
Msimu mpya na mambo mapya! Victoria Simon ni mwana mitindo bora na mtangazaji wetu wa Harusi Yetu!
09 JULAI 2018
Ndugu watazamaji wetu, tumefanikiwa kuwa pamoja nanyi katika mengi mazuri na mazuri zaidi! Kuanzia msimu wa kwanza hadi sasa, upo msimu wa tatu, tukaona sio mbaya tukibadili mboga, au sio? Katika msimu huu wa tatu, tunawaahidi watazamaji wetu simulizi maru maru na shamra shamra za kukata na shoka!
Mwaka huu, tunawaletea mtaalamu anayejulikana sana katika ulimwengu wa burudani, mitindo na fasheni. Yeye ni Msomi katika nyanja ya teknolojia, haswa, katika ufundi wa I.T, ni nani atakayeuwa mtangazaji wetu mpya wa Harusi Yetu?


Victoria Simon ni mtangazaji mpya wa msimu wa tatu wa kipindi cha harusi yetu! Victoria alizaliwa nchini Tanzania mkoani Songea mnamo mwaka 1994. Alihitimu masomo yake ya O'level mnamo mwaka 2011 katika shule ya sekondari Mbalizi jijini Mbeya, na baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambapo alihitimu shahada yake katika masomo ya IT (Teknolojia ya Habari) mnamo mwaka 2014.
Ndani ya moyo wake , Victoria alikuwa na ndoto kubwa ya kuwa mtangazaji maarufu nchini kwani hupenda zaidi kutangaza, Kuimba, kuwa mwana mitindo, na ucheshi.


Vicky alifanya kazi katika hoteli ya Ruhuwiko jijini Songea kama fundi wa IT kwa miezi kadhaa, kisha akaacha baada ya kupata kazi kwenye kipindi cha Televisheni kwa ajili ya demo ya kipindi cha watoto kiitwacho playground lakini hakufanikiwa kuendelea kutokana na matatizo ya kiofisi yaliyoikumba kampuni hiyo.
Kutokana na kusimamishwa kwa kipindi, Victoria hakuwa na jinsi, bali kuhama kutoka kuwa mtangazaji na kuanza kazi za kuwavalisha waigizaji katika short film kama vile Tamala, Leah, Matonge 4 na kipindi cha Mwantumu.
Victoria alipona tangazo la shindano la kutafutwa mtangazaji mpya wa kipindi cha Harusi Yetu, aliamua kujaribu bahati yake na kuibuka kidedea katika shindano baada ya kuchaguliwa na chaneli ya Maisha Magic Bongo kati ya ma binti 120 walioshiriki.
Haya basi, jitayarisheni kupata vipindi vya kusisimua, hadithi za kupapasa moyo, ufundi wa kipekee, mitindo ya kila aina na uhondo chungu nzima kuanzia tarehe 19 Julai, saa 1 usiku pamoja na Victoria Simon katika msimu mpya wa Harusi Yetu!
 

donga

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
1,197
2,000
itakua njia nzuri sana kama nikipata nafasi ntamfikishia kwenye insta yake nikijua jina
 

Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,154
2,000
Kimsingi huwezi kumaliza O' Level 2011, halafu ukamaliza Shahada ya I.T UDSM 2014, kwanza labda amesoma UCC maana kwa UDSM kozi za IT ni Computer Engineering and IT iliopo COET, COiCT wao wana BSC Computer Science, BSC with Computer Science na Electronics Communication huyu atakua na Diploma ya I.T toka UCC - Univeristy Computing Centre
 

donga

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
1,197
2,000
Kimsingi huwezi kumaliza O' Level 2011, halafu ukamaliza Shahada ya I.T UDSM 2014, kwanza labda amesoma UCC maana kwa UDSM kozi za IT ni Computer Engineering and IT iliopo COET, COiCT wao wana BSC Computer Science, BSC with Computer Science na Electronics Communication huyu atakua na Diploma ya I.T toka UCC - Univeristy Computing Centre
usibishe hii story cjatunga nimeitoa maisha magic bongo dstv
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom