Victoria Mwanziva awapongeza vijana kwa kushiriki uchaguzi ndani ya Chama cha Mapinduzi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,886
938
VICTORIA MWANZIVA AWAPONGEZA VIJANA WENZAKE KWA KUSHIRIKI UCHAGUZI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Hongereni sana Vijana wenzangu wote ambao kwanza; mmeshiriki mchakato wa uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Nawapongeza kwa uthubutu wenu; Nawapongeza kwa utayari wenu wa kuhudumia Vijana wenzenu ndani ya Chama na Tanzania kiujumla.

Vijana tuna nafasi kubwa ya ushiriki ndani ya Chaguzi hizi na hakika ushiriki umekuwa mkubwa na wenye hamasa kubwa kwa vijana wote katika Chama Cha Mapinduzi kwa maana ya Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi; Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jumuiya ya Umoja wa Wazazi (UUW), na Jumuiya yetu bingwa kabisa ya Vijana - Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).

Nawapongeza vijana wa kushiriki kikamilifu- na kwa wale waliopata nafasi na kushinda nafasi za uongozi na uwakilishi katika ngazi hizi zinazoendelea ningependa sana kuwapongeza na kuwaambia neno; Hongereni sana
Wanachama wote wa CCM ambao mmeshiriki kikamilifu katika chaguzi; Naomba niwape pongezi sana; na Hongera kwa wawakilishi wetu mliopewa dhamana kwenye Mashina, Matawi na ngazi ya Kata.

Naomba niwasisitize kuwa chaguzi zinaendelea, Vijana wenzangu tushiriki kikamilifu katika maeneo yetu; tushiriki kikamilifu katika chaguzi hizi ili tusipoteze haki yetu ya kuchagua wabeba maono na wawakilishi wetu kwenye ngazi mbalimbali.

Narejea kwa walioaminiwa; Hongereni sana, unganeni na wenzenu wote mliowania nafasi; unganeni na wenzenu wote mlioshiriki mchakato. Tukumbuke neno muhimu kuwa CHAMA KWANZA MTU BAADAE; Hivyo tukumbuke kuwa yote tufanyayo ni kwa maslahi ya Chama na Tanzania yetu.

Makundi hayana nafasi; kujiona wewe ni bora sana hakuna nafasi, tuunganishe nguvu katika kuhakikisha tunakuwa madaraja ya huduma kwa jamii inayotuzunguka. Tuunganishe nguvu katika ujenzi wa Chama na Taifa; Tuunganishe nguvu katika kuhakikisha kuwa uwepo wetu ndani ya Chama una thamani na manufaa kwa wanachama wenzetu.

Vyeo ni dhamana ambazo zimetokana na kudra za Mwenyezi Mungu; katika vitu ambavyo uwe navyo makini usiruhusu Cheo kikakubadilisha ukadharau wengine, ukajiona bora sana, ukajiona mwenye haki sana, ukajiona mwenye weledi, upeo na uwezo sana. HAPANA! Cheo ni huduma, usitenge wenzako kisa umepata uongozi.

KUNA MAISHA BAADA YA CHEO, ISHI NA KILA MTU KWA UPENDO.

VICTORIA MWANZIVA
KATIBU UHAMASISHAJI NA CHIPUKIZI UVCCM TAIFA💪🏻
KAZI IENDELEE

1 FRZCI5skm6zqqqrhX3C-DA.jpeg
 
Back
Top Bottom