...Mkjj, kupika ni aina ya sayansi, kunahitaji mpangilio ulio makini ili kupata mlo wenye matumaini, kushibisha na kurutubisha mwili. Ukijiwekea mambo kwenye sufuria bila kujali ni joto gani linahitajika na nini kitangulie, utaishia kupata miuji-uji isiyonyweka although contents ni zilezile!
...Lile gazeti la Telegraph la kule Uingereza lililofanikisha kuwatibua na kuwalipua baadhi ya wabunge wa nchi ile hadi spika wao, lilifata mpangilio uliokuwa umefikiriwa kwa makini kabla ya kuwa executed. Bila hivyo gazeti lingeweza kufungiwa na lingeweza kutofanikisha lengo lake ipasavyo, hata kule kuwahabarisha tu watu.
...Kwenye hii ishu ya Meremeta, inatakiwa watu/wabunge wenye uwezo. Tatizo tunao wachache mno kwenye bunge letu. Tukitegemea kupata bonge la menu, bila kufata recipe ipasavyo, tusishangae kujikuta tunaletewa mezani miujiuji isiyonyweka!!
...Kwa wenye kuhitaji kuiona Darwin's Nightmare kupitia kwenye mitandao, documentary hiyo inapatikana hapa: Darwin's nightmare - Darwins Albtraum
...Kama hupendi kuangalia background issues, unaweza ukaforward hadi dakika ya 40 hivi, mambo ya Mh. Mkapa na Serikali ndipo yanapoanza kuongelewa.
SteveD.
Naomab link ya ku-download "darwin's Nightmare">>>basi nimeipata