TANZIA Vicky Nsilo Swai mwenye historia ya kuhifadhi viatu vya Hayati Mandela kwa miaka 33 afariki dunia

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mama Vicky Nsilo Swai mwenye historia ya kuhifadhi nyumbani kwake viatu vya mpigania uhuru wa Afrika ya kusini hayati Rais Nelson Mandela mwaka 1962 amefariki dunia.

Pia soma
-

viatu.jpg

Rais wa kwanza Mzalendo na Mpigania Uhuru wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela ‘Madiba’ akiwa ameshikilia viatu vyake ambavyo aliviacha nyumbani kwa Mzee Nsilo Swai alipoingia Tanzania mwaka 1962 akitokea Afrika Kusini ili kuanza harakati za ukombozi. Mzee Mandela aliahidi kuvichukua viatu hivyo pindi atakaporejea Tanzania lakini katika safari hiyo ndipo alipoishia mikoni mwa makaburu wa Afrika Kusini na kumfunga kwa miaka 27. Viatu hivyo vilihifadhiwa hadi alipotoka na kukabidhiwa kwa Mandela na mjane wa Mzee Nsilo Swai, Bi Vicky Nsilo Swai (pichani kulia) Desemba 12,1995 Mandela alipotoka gerzani na hatimaye kuwa Rais wa kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.

8738232_orig.jpg

Maandishi ya Mzee Mandela kwa Mama Vicky Nsilo Swai aliyoyaandika kwenye kitabu alichompa kama zawadi baada ya kurudishiwa viatu vyake mwaka 1995

IMG_0913.jpg

Mama Vicky Nsilo Swai na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya Mazishi ya Mzee Mandela kijijini Qunu
 
Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa huzuni na masikitiko kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Vicky Nsilo Swai kilichotokea Jumatatu tarehe 31 Mei 2021, saa tano asubuhi Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amemtaja Marehemu Vicky Nsilo Swai kama Mwanasiasa mahiri, mpambanaji, mwenye msimamo thabiti wakati wa uhai wake na kwamba alikuwa mstari wa mbele kupigania usawa wa kijinsia, utu na hadhi ya mwanamke.

“Marehemu Mama Vicky ametumia sehemu kubwa ya uhai wake kuwaunganisha Wanawake wa Tanzania na kuwahimiza katika kushiriki shughuli za maendeleo kisiasa, kijamii na kiuchumi” Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Mama Vicky Nsilo Swai amewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Kilimanjaro. Aidha, akiwa Mke wa Muasisi wa Chama, Marehemu Asanterabi Zephaniah Nsilo Swai, Mama Vicky ameshiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika pamoja na kusaidia ukombozi wa mataifa mengine kusini mwa Bara la Afrika.

“Miongoni mwa sifa kubwa alizowahi kuwa nazo Marehemu Vicky Swai, ni uaminifu, ambapo amewahi kuhifadhi viatu vya Mpigania Uhuru na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Afrika Kusini Hayati Mzee Nelson Mandela kwa miaka 33 kuanzia mwaka 1962 vilipoachwa na mpiganaji huyo wa ANC kwa familia ya Mzee Asanterabi Nsilo Swai na kuvikabidhi kwake mwaka 1995 akiwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini” Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa salamu za rambirambi na pole kwa familia ya marehemu Vicky Nsilo Swai na kuwaomba kuwa wavumilivu, wastahamilivu na wenye subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe.

SHAKA HAMDU SHAKA
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
1 JUNI, 2021
IMG-20210601-WA0021.jpg
IMG-20210601-WA0022.jpg
 
1 Juni, 2021
TANZIA

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa huzuni na masikitiko kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Vicky Nsilo Swai kilichotokea Jumatatu tarehe 31 Mei 2021, saa tano asubuhi Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan amemtaja Marehemu Vicky Nsilo Swai kama Mwanasiasa mahiri, mpambanaji, mwenye msimamo thabiti wakati wa uhai wake na kwamba alikuwa mstari wa mbele kupigania usawa wa kijinsia, utu na hadhi ya mwanamke.

“Marehemu Mama Vicky alitumia sehemu kubwa ya uhai wake kuwaunganisha Wanawake wa Tanzania na kuwahimiza katika kushiriki shughuli za maendeleo kisiasa, kijamii na kiuchumi” Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Mama Vicky Nsilo Swai amewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Kilimanjaro. Aidha, akiwa Mke wa Muasisi wa Chama, Marehemu Asanterabi Zephaniah Nsilo Swai, Mama Vicky ameshiriki katika harakati za ukombozi wa Tanganyika pamoja na kusaidia ukombozi wa mataifa mengine kusini mwa Bara la Afrika.

“Miongoni mwa sifa kubwa alizowahi kuwa nazo Marehemu Vicky Swai, ni uaminifu, ambapo amewahi kuhifadhi viatu vya Mpigania Uhuru na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Afrika Kusini Hayati Mzee Nelson Mandela kwa miaka 33 kuanzia mwaka 1962 vilipoachwa na mpiganaji huyo wa ANC kwa familia ya Mzee Asanterabi Nsilo Swai na kuvikabidhi kwake mwaka 1995 akiwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kusini.” Ndugu Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan anatoa salamu za rambirambi na pole kwa familia ya marehemu Vicky Nsilo Swai na kuwaomba kuwa wavumilivu, wastahamilivu na wenye subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina la Bwana Lihimidiwe.

SHAKA HAMDU SHAKA
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
IMG_0913.jpg
IMG-20210601-WA0006.jpg
 
IMG-20210601-WA0058.jpg
IMG_0913.jpg
 
RIP Vicky Nsilo
Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa huzuni na masikitiko kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Vicky Nsilo Swai kilichotokea Jumatatu tarehe 31 Mei 2021, saa tano asubuhi Moshi Mkoani Kilimanjaro....
 
Wachaga ndio maana hadi leo wametoboa, yaani miaka hiyo wao wanawahifadhi wageni kama mzee madiba.
nilisoma mahali, huyu mama Vicky Nsilo Swai ni mke wa aliyekuwa nadhani waziri wa fedha wa wakati huo Ndg Asanterabi Nsilo Swai.

kwahiyo, Mandela alipoingia kwa siri hapa nchini kupitia Mbeya, katika juhudi zake za ukombozi wa SA, aliishi nyumbani kwa huyo wazir badala ya hotelini kama hatua ya kujificha.

Baadae Mandela alielekea nchi moja ya west africa, na wakt wa kurudi alipitiliza moja kwa moja hadi SA ambapo aliishia kukamatwa na kufungwa.

naweza kurekebishwa, maana ni mda kidgo pengine nimesahau baadhi ya details
 
Back
Top Bottom