Vicky Kamata: Rais Samia hawezi kutibu majeraha, viongozi wa dini wagange mioyo ya watu, wamejeruhiwa

Hapa swala siyo hiyo Sir Name,point hapa ni kung’ang’ania mtoto wake apewe urithi sawa na watoto wa Marehemu,wakati hakuna uthibitisho wowote kuwa Marehemu aridhia mtoto huyo apewe urithi kama mtoto halali wa Marehemu
Ulichoandika kilijikita zaidi kwenye surname na sio haki ya huyo mtoto kurithi mali za marehemu. Mara nyingi huwa tunawa treat watoto wa kufikia kama wale tuliozaa wenyewe lakini ukweli mchungu ni kuwa bila kuuweka uhusiano huo kisheria au kumwingiza kimaandishi katika mirathi ( kitu ambacho mahakama zetu ni wepesi kuzikana kwa kuamini zaidi uzaliwa wa damu) inakuwa imekula kwa mtoto. Hata kama mtoto wa kufikia ndie aliyekuwa karibu zaidi na kumhudumia zaidi marehemu.

Amandla..
 
Mtu alikuwa ndani ya Ccm hakukosoa kipindi hicho why leo tupunguze kiwango cha UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA.
Siasa nzuri ni pamoja na kujua uwezo wako na uwezo wa mshindani wako. Kama huna uwezo wa kupambana naye kwa muda husika basi kuwa mpole kama mti wa mnazi wakati wa tufani. Unapotaka kulipiza kisasi uwe na uhakika kwamba unayepambana naye hatakuwa na uwezo tena wa kujibu mapigo. Mlipiza kisasi anayefanikiwa ni yule ambaye atakuwa amejishusha sana kwa mtesi wake kiasi kwamba yule mtesi akadanganyika kwamba jamaa kakubali matokeo na hana madhara tena kwake,kumbe mwenzake anamlia taimingi tuu... (By Busara za Babu yangu, 1947)...
 
mkapa waliomfahamu at a personal level wanadai jamaa hakutaka watu wanaojipendekeza kwake na hakuwa na urafiki yule mzee yani kwa kifupi alikuwa na maisha anayojua yeye
nasikia amewahi mara nyingi kuwafukuza wageni ikulu kuna wanasiasa aliwadisi wamefata soseji ikulu
But still akataka kutupora mgodi wetu kule Kiwira mpaka watu walipopiga kelele, no one is perfect...
 
Hii ni natural progression

Una madaraka,hutaki kukosolewa ukiwa madarakani maana unaua wakosoaji,ukifa,ni naturally ndio watu watakukosoa muda huo

Thats a natural progression ni ni right..

Sasa wewe kuja na kuwaita "wanafiki" wakati maisha ya kukosoa wakati akiwa na power ni your life on the line then wanasubiri siku haupo madarakani na upo kwenye your lowest state ndio wanaanza kukukosoa na ku-pay back on you....

Wewe kuwaita wanafiki inaonesha you just dont know human behaviour...hujui lolote!
Membe aliekosoa yeye si binadamu ?
 
Huyu naye au alikuwa miongoni mwa wanufaika wa Kikwete?
Mbona hamusahau Jiwe?
Swala kufa kila mtu atakufa,mbona kifo Cha Magufuli anakiona Kama adhabu?
Mbona mme wake alishakufa naye alionea watu ndo maana alikufa?
Hovyo kabisa.
Tena hovyo za kushangaza. Kuna watu wanasiasa wanatakaga kila awamu wao tu ndio watambe na beneficiaries zao. Ni frustrations za kutapeliwa ndoa, then kuolewa kama reserve ikifuatiwa na kutumumbuliwa ukuu wa hazina mume wake, then ikaja mumewe kunyimwa udhamini na serikali ya JPM.kufanya kazi AU aliyoihangaikia after kutumumbuliwa na kukosa uteuzi wa ndani ikapelekea mauti.

Bado Mjane akagombea jina likakatwa, na hakuna uteuzi afterwards kwa ivo VK ana hasira sana na kifua kimmejaa mengi. Hapo anatembelea mstarii ili SSH amkumbuke hata UDC kupitia huruma ya wanawake na maendeleo. La sivyo anajiandaa sijui jimbo gani sasa 2025 manake hakuna jimbo la mpinzani kama alivyodai kwenda Kibamba

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni natural progression

Una madaraka,hutaki kukosolewa ukiwa madarakani maana unaua wakosoaji,ukifa,ni naturally ndio watu watakukosoa muda huo

Thats a natural progression ni ni right..

Sasa wewe kuja na kuwaita "wanafiki" wakati maisha ya kukosoa wakati akiwa na power ni your life on the line then wanasubiri siku haupo madarakani na upo kwenye your lowest state ndio wanaanza kukukosoa na ku-pay back on you....

Wewe kuwaita wanafiki inaonesha you just dont know human behaviour...hujui lolote!
Kwa hiyo SSH wanamsubir tu akiachia madaraka then wanaye?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Kuna Mzee tunaishi nae mtaani. Huyu Mzee ni Kada maarufu wa CCM hapa mtaani kwetu. Kwa miaka mingi amekuwa mtetezi wa CCM. Hivi sasa Mzee yule kaamua kupiga kimya. Kilichomfanya awe mnyonge kwa Chama chake ni namna kinavyofanya maamuzi yake kwa sasa. Akatolea mf suala dogo la Wamachinga: Waliotoa ruhusa hata na kuwapatia vitambulisho ni CCM. Waliotoa tamko la kuwaondoa ni CCM ile ile. Sasa tunafuata ya Chama au mawazo ya mtu binafsi??

Mama ameonekana akijitahidi kuyaendeleza yale yote yaliyoasisiwa na mtangulizi wake lkn wakati huo huo akichomekea yakwake ili nae aweke alama kwenye Uongozi wake.

Amesema kitendo hiki kimefanya kuonekane Makundi makubwa ndani ya Chama. Yaani kundi la mwendazake linalowatetea Wamachinga.
Kundi la pili ni la Mama linalopingana na Wamachinga. Na kundi la tatu ni la Ndugai ambalo halina upande Bali wao wanasubiri mshindi wamuunge mkono.

Amesema kundi la Ndugai ndilo kundi baya mno kwani wao ndio wachochezi wa makundi yale mawili yenye nguvu. Yaani wanaliendesha kundi lao kwa siasa za kinafiki.

Kwa mtizamo huo kwangu mimi nakiona Chama changu kipo gizani. Hivyo acha niendelee kukaa kimya.

Swali langu ni Je kweli kuna haya makundi ndani ya CCM????
Makundi kipindi cha mwendazake yatoke wapi wakati yeye ndiye alikuwa alfa na Omega? Umesahau alivyokuwa anawazingua hadharani wenzake? Kuwaita wapumbavu, kwamba mashangazi watachapwa viboko, kama siyo mimi wengi humu musingepata ubunge etc etc
 
Ulichoandika kilijikita zaidi kwenye surname na sio haki ya huyo mtoto kurithi mali za marehemu. Mara nyingi huwa tunawa treat watoto wa kufikia kama wale tuliozaa wenyewe lakini ukweli mchungu ni kuwa bila kuuweka uhusiano huo kisheria au kumwingiza kimaandishi katika mirathi ( kitu ambacho mahakama zetu ni wepesi kuzikana kwa kuamini zaidi uzaliwa wa damu) inakuwa imekula kwa mtoto. Hata kama mtoto wa kufikia ndie aliyekuwa karibu zaidi na kumhudumia zaidi marehemu.

Amandla..

Ungerudi nyuma kidogo ungeelewa kwanini niliandika hiyo comment,ilikuwa ni mwendelezo wa hoja flan.Yes hapo pa kumwingiza mtoto kisheria ndipo alipokwama,maana Wanafamillia wanahitaji uthibitisho ambao hana,yeye amejikita zaidi kwa kuwa mtoto alitumia ubini wa Marehemu.Familia ni waelewa sana,ni vile yeye Vicky anataka kuwaletea ujuaji wake ndiyo maana wameamua kudeal nae kisheria zaidi pia.
 
Ungerudi nyuma kidogo ungeelewa kwanini niliandika hiyo comment,ilikuwa ni mwendelezo wa hoja flan.Yes hapo pa kumwingiza mtoto kisheria ndipo alipokwama,maana Wanafamillia wanahitaji uthibitisho ambao hana,yeye amejikita zaidi kwa kuwa mtoto alitumia ubini wa Marehemu.Familia ni waelewa sana,ni vile yeye Vicky anataka kuwaletea ujuaji wake ndiyo maana wameamua kudeal nae kisheria zaidi pia.

Samahani, unaposema familia unamaanisha wakina nani? I am just curious.

Amandla...
 
Makundi kipindi cha mwendazake yatoke wapi wakati yeye ndiye alikuwa alfa na Omega? Umesahau alivyokuwa anawazingua hadharani wenzake? Kuwaita wapumbavu, kwamba mashangazi watachapwa viboko, kama siyo mimi wengi humu musingepata ubunge etc etc
Hawa wote walipopata Ubunge kama kina Gwajiboy na wenzie unafikiri wako kundi gani???
 
Samahani, unaposema familia unamaanisha wakina nani? I am just curious.

Amandla...

Familia ya upande wa Mumewe wakiwemo watoto wa Marehemu.Pana VN ilivuja akiwa anawapiga mikwara siku ya kikao cha familia baada ya msiba.
 
Sioni ktk hayo aliyomlalamikia jiwe chochote chenye maslah kwa Taifa zaidi ya kulalamikia tumbo lake.
Hawa ndio wanasiasa wetu, wamejipa hati miliki ya vyeo walivyoshika.
 
Samahani mkuu wangu,kwan kufanya kazi AU au UN ni lazima hadi serikali yako ikudhamini?? Naomba ufafanuzi kama hautojali!!

Ni kwa zile kazi za kupigiwa kura ambazo wagombea (candidates) lazima wadhaminiwe na majina yao kuwasilishwa rasmi na nchi husika. Top jobs zinazoenda kwa mizunguko ya mabara (regions) na nchi.
 
matatizo aliyoyapata hukuyaona?

his private conversations where leaked,ni kifo tu alisubiria

mkuu sikiliza

Mtu akiwa kwenye his highest point of his powers hua anaachwa ila siku zikishuka ndio muda wa kulipa kisasi

Vicky sijui Diallo,sijui Wyatt,sijui etc etc...ndio muda wa kulipa kisasi kwa magufuli na his nonsense

Hii ni pure revenge issue,na issue yako ya "unafiki" ni irrelevant kabisa hapa

Mkuu umeeleweka. Hii ni muhimu kwa watu waliokuwa na msimamo dhidi ya Magufuli kama kina Lissu, Kinana, Membe, Heche, Mch Msigwa, n.k.

Lakini kwa hizi modeli za Vicky Kamata au Zitto ambao walikua wanavizia fursa ya “kupendwa” na Magufuli bila kujali uovu wake, hawana credibility ya kumsema vibaya. Angewapa fursa hawa wangetetea hata Lissu kupigwa risasi kama alivyofanya Mollel na Slaa.
 
Amesema kiongozi wa awamu ya tano (jiwe) alikuwa mtu katili sana kiasi cha kumfanya apate taabu sana.

Amewasihi watanzania kuishi kwa kutenda mema maana duniani tunapita. Jiwe alilewa madaraka.

Amemaliza kwa kusema pamoja na kufuta andiko lake la kumshutumu jiwe ni kweli jiwe aliniumiza sana.

Source: StarTv (Medani za Siasa) muda huu.

==========

Mwandishi: Hujaeleza mheshimiwa Vicky Kamata, umezunguka sana. Swali la msingi, ni kitu gani kigumu ama ni jambo gani, wakati gani ambao ulikumbana na jambo gumu ambalo ukitafakari unaona kabisa kidogo likutoe kwenye reli?

Vicky Kamata: Unazungumza wakati tayari niko bungeni au wakati natamani kuwa kwenye siasa?

Mwandishi: Tayari uko kwenye siasa

Vicky Kamata: Nikiwa bungeni, labda kile kipindi ambacho awamu ya tano iliingia, mimi ilikuwa tayari ndio nimeolewa, nina ndoa changa tu ikatokea bahati mbaya, siwezi kusema bahati mbaya, mwenye ofisi yake akisema pumzika nataka huyu akae hapa utalalamika? Huwezi kulalamika.

Hicho kilitokea kwa mume wangu, alikipokea very positively, binafsi nilikipokea kawaida kabisa na maisha yakawa mazuri kabisa lakini sasa wenzangu pale bungeni wakaanza kama kunitenga.

Chochote ninachoshauri naonekana ninashauri kwa sasabu nina hasira, kitu ambacho sikuwa nacho wala sikiwazii kwasababu mhusika mwenyewe hajalalamika, walihusisha kazi ya mume wangu na kazi yangu.

Tena wanaCCM wenzangu mpaka walikuwa wanachangia wazi kabisa yaani flani, anakupiga kijembe cha wazi kabisa kwamba una hasira, mume wako ametumbuliwa.


Mwandishi: Umekuwa mbungewa viti maalum kwa miaka 10 mkoa wa Geita, kwanini ukaja huku(Dar-Kibamba) ambako hukufanya chochote kwa ajili yao? Hofu yako ilikuwa nini Geita?

Kamata: Sikuwa na hofu isipokuwa katika majimbo yote ya Geita, yote yalikuwa na wabunge ambao ni wazuri, kaka zangu na wanafanya kazi nzuri kiasi huoni sababu ya kwenda kusukumana na Dotto Biteko, Kanyasu au uende kwa Msukuma

Mwandishi: Kwa mantiki hiyo unataka kutuambia Kibamba hakukuwa na mbunge anayefanya vizuri?

Kamata: 'Exactly' mimi ni CCM mbunge aliyekuwepo wakati ule alikuwa ni wa upinzani na niliona ilikuwa ni wakati sahihi wa kurudisha jimbo letu kwenye chama cha mapinduzi, Kibamba nilienda kwasababu jimbo lilikuwa upinzani na kule kwetu hakuna jimbo lolote lilikuwa upinzani, majimbo yote yalikuwa ni CCM na yalikuwa na wabunge wanapendwa

Mwandishi: Unataka kuwaaminisha watanzania, majimbo ambayo yanaongozwa na wabunge wa CCM ndio yanayopofanya vizuri

Kamata: Sijasema hivyo, inawezekana yapo majimbo ya wabunge wa CCM na hayafanyi vizuri lakini kwa mkoa wangu wa Geita wana sifa nzuri na wanafanya kazi nzuri.

Mwandishi: Ni kweli kwamba wanawake wengi walioko kwenye siasa wanatumika kwenye rushwa ya ngono?

Kamata: Mimi kama mbunge wa viti maalum nilipigiwa kura na wanawake wenzangu, sasa ukiniambia kuna rushwa ya ngono sijui hata inakuwaje lakini sidhani, siwezi kulijibia hilo.

Mwandishi: Hivi karibuni tulishuhudia andiko lako katika mitandao ya kijamii ambalo liliibua hisia za watanzania na nikiona kila mmoja akiipost kwa walichodai umetoa povu, nini ilikuwa dhamira ya andiko lako?

Kamata: Ningeshangaa usingeniuliza hilo swali, dhamira ya andiko langu ilikuwa ni kukumbusha watanzania wenzangu au mtu yoyote ambae angepita kwenye 'page' yangu kwamba hapa duniani sio mahali petu pa kudumu, tujitahidi kusihi vizuri ili tutakapoondoka tuache historia nzuri kwasababu hakuna atakaebaki hapa, hapa tumepewa muda mchache tu lakini katika muda huu mchache tuyafanye yale mzee Mwinyi amekuwa akituambia, kwamba maisha ni hadithi tu.

Mwandishi: Kwanini viongozi wengi wanatumia nafasi zao vibaya kama ulivyosema?

Vicky Kamata: Nadhani ni hulka ya mtu mwenyewe, walikuwepo viongozi ambao wapo kwa ajili ya kutesa watu wa Mungu na Mungu alijua jinsi ya kushughulika nao leo tunawasoma kama historia.

Mwingine anapambana apate madaraka fulani ili amkomeshe fulani.

Mwandishi: Athari yake katika taifa ni nini?

Vicky Kamata: Athari yake ni kutengeneza Taifa la watu wanafki, waongo, wavivu wasiojiamini na madhara yake pia ni makubwa sana kwasababu hakuna kitakachoendelea, nchi itasimama.

Juzi nimemuona askofu Arusha akimwambia mama, mama tibu majeraha, kwanini amesema hivyo? Ina maana kuna waliojeruhiwa, mimi nataka kuongezea hapo kwa askofu, sio mama atibu majeraha ila ninawaomba viongozi wa dini wagange mioyo ya watu wamejeruhiwa kwasababu ile post yangu imenipa vitu vya ajabu, nimepigiwa simu nyingi sana, kila mtu anaelezea maumivu aliyopitia katika kipindi fulani.

Kwa hiyo nataka kusema kwamba, sio mama Samia, mama Samia hawezi kutibu majeraha lakini viongozi wa dini wanaweza kutibu majeraha ya watu walioumizwa.

Jiwe alikuwa mwana kharam
 
Back
Top Bottom