Vicky Kamata: Rais Samia hawezi kutibu majeraha, viongozi wa dini wagange mioyo ya watu, wamejeruhiwa

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
8,153
2,000
Amesema kiongozi wa awamu ya tano (jiwe) alikuwa mtu katili sana kiasi cha kumfanya apate taabu sana.

Amewasihi watanzania kuishi kwa kutenda mema maana duniani tunapita. Jiwe alilewa madaraka.

Amemaliza kwa kusema pamoja na kufuta andiko lake la kumshutumu jiwe ni kweli jiwe aliniumiza sana.

Source: StarTv (Medani za Siasa) muda huu.

==========

Mwandishi: Hujaeleza mheshimiwa Vicky Kamata, umezunguka sana. Swali la msingi, ni kitu gani kigumu ama ni jambo gani, wakati gani ambao ulikumbana na jambo gumu ambalo ukitafakari unaona kabisa kidogo likutoe kwenye reli?

Vicky Kamata: Unazungumza wakati tayari niko bungeni au wakati natamani kuwa kwenye siasa?

Mwandishi: Tayari uko kwenye siasa

Vicky Kamata: Nikiwa bungeni, labda kile kipindi ambacho awamu ya tano iliingia, mimi ilikuwa tayari ndio nimeolewa, nina ndoa changa tu ikatokea bahati mbaya, siwezi kusema bahati mbaya, mwenye ofisi yake akisema pumzika nataka huyu akae hapa utalalamika? Huwezi kulalamika.

Hicho kilitokea kwa mume wangu, alikipokea very positively, binafsi nilikipokea kawaida kabisa na maisha yakawa mazuri kabisa lakini sasa wenzangu pale bungeni wakaanza kama kunitenga.

Chochote ninachoshauri naonekana ninashauri kwa sasabu nina hasira, kitu ambacho sikuwa nacho wala sikiwazii kwasababu mhusika mwenyewe hajalalamika, walihusisha kazi ya mume wangu na kazi yangu.

Tena wanaCCM wenzangu mpaka walikuwa wanachangia wazi kabisa yaani flani, anakupiga kijembe cha wazi kabisa kwamba una hasira, mume wako ametumbuliwa.


Mwandishi: Umekuwa mbungewa viti maalum kwa miaka 10 mkoa wa Geita, kwanini ukaja huku(Dar-Kibamba) ambako hukufanya chochote kwa ajili yao? Hofu yako ilikuwa nini Geita?

Kamata: Sikuwa na hofu isipokuwa katika majimbo yote ya Geita, yote yalikuwa na wabunge ambao ni wazuri, kaka zangu na wanafanya kazi nzuri kiasi huoni sababu ya kwenda kusukumana na Dotto Biteko, Kanyasu au uende kwa Msukuma

Mwandishi: Kwa mantiki hiyo unataka kutuambia Kibamba hakukuwa na mbunge anayefanya vizuri?

Kamata: 'Exactly' mimi ni CCM mbunge aliyekuwepo wakati ule alikuwa ni wa upinzani na niliona ilikuwa ni wakati sahihi wa kurudisha jimbo letu kwenye chama cha mapinduzi, Kibamba nilienda kwasababu jimbo lilikuwa upinzani na kule kwetu hakuna jimbo lolote lilikuwa upinzani, majimbo yote yalikuwa ni CCM na yalikuwa na wabunge wanapendwa

Mwandishi: Unataka kuwaaminisha watanzania, majimbo ambayo yanaongozwa na wabunge wa CCM ndio yanayopofanya vizuri

Kamata: Sijasema hivyo, inawezekana yapo majimbo ya wabunge wa CCM na hayafanyi vizuri lakini kwa mkoa wangu wa Geita wana sifa nzuri na wanafanya kazi nzuri.

Mwandishi: Ni kweli kwamba wanawake wengi walioko kwenye siasa wanatumika kwenye rushwa ya ngono?

Kamata: Mimi kama mbunge wa viti maalum nilipigiwa kura na wanawake wenzangu, sasa ukiniambia kuna rushwa ya ngono sijui hata inakuwaje lakini sidhani, siwezi kulijibia hilo.

Mwandishi: Hivi karibuni tulishuhudia andiko lako katika mitandao ya kijamii ambalo liliibua hisia za watanzania na nikiona kila mmoja akiipost kwa walichodai umetoa povu, nini ilikuwa dhamira ya andiko lako?

Kamata: Ningeshangaa usingeniuliza hilo swali, dhamira ya andiko langu ilikuwa ni kukumbusha watanzania wenzangu au mtu yoyote ambae angepita kwenye 'page' yangu kwamba hapa duniani sio mahali petu pa kudumu, tujitahidi kusihi vizuri ili tutakapoondoka tuache historia nzuri kwasababu hakuna atakaebaki hapa, hapa tumepewa muda mchache tu lakini katika muda huu mchache tuyafanye yale mzee Mwinyi amekuwa akituambia, kwamba maisha ni hadithi tu.

Mwandishi: Kwanini viongozi wengi wanatumia nafasi zao vibaya kama ulivyosema?

Vicky Kamata: Nadhani ni hulka ya mtu mwenyewe, walikuwepo viongozi ambao wapo kwa ajili ya kutesa watu wa Mungu na Mungu alijua jinsi ya kushughulika nao leo tunawasoma kama historia.

Mwingine anapambana apate madaraka fulani ili amkomeshe fulani.

Mwandishi: Athari yake katika taifa ni nini?

Vicky Kamata: Athari yake ni kutengeneza Taifa la watu wanafki, waongo, wavivu wasiojiamini na madhara yake pia ni makubwa sana kwasababu hakuna kitakachoendelea, nchi itasimama.

Juzi nimemuona askofu Arusha akimwambia mama, mama tibu majeraha, kwanini amesema hivyo? Ina maana kuna waliojeruhiwa, mimi nataka kuongezea hapo kwa askofu, sio mama atibu majeraha ila ninawaomba viongozi wa dini wagange mioyo ya watu wamejeruhiwa kwasababu ile post yangu imenipa vitu vya ajabu, nimepigiwa simu nyingi sana, kila mtu anaelezea maumivu aliyopitia katika kipindi fulani.

Kwa hiyo nataka kusema kwamba, sio mama Samia, mama Samia hawezi kutibu majeraha lakini viongozi wa dini wanaweza kutibu majeraha ya watu walioumizwa.
Mbona mnamchonganisha mdada wa watu. Yeye alipata majeraha kwa mume wake kutumbuliwa. Ukitumbuliwa kwa ufisadi au uzembe sio ajabu wewe na jamaa zako kupata machungu.
Lakini umma wa wananchi walipata faida sana kwa viongozi fisadi na wazembe kutumbuliwa. Na kwa hili wanamkumbuka na kumlilia magufuli. Kusema Magufuli alikua kiongozi mkatili ni uongo. Alikua kiongozi mwema sana kwa umma na asiye na huruma kwa watu fisadi na wazembe. Huo ndio ukweli wala kama nchi tusije shiriki kilio cha fisadi na wazembe...acha walie wenyewe.
 

masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
15,942
2,000
Mbona mnamchonganisha mdada wa watu. Yeye alipata majeraha kwa mume wake kutumbuliwa. Ukitumbuliwa kwa ufisadi au uzembe sio ajabu wewe na jamaa zako kupata machungu.
Lakini umma wa wananchi walipata faida sana kwa viongozi fisadi na wazembe kutumbuliwa. Na kwa hili wanamkumbuka na kumlilia magufuli. Kusema Magufuli alikua kiongozi mkatili ni uongo. Alikua kiongozi mwema sana kwa umma na asye na huruma kwa watu fisadi na wazembe. Huo ndio ukweli wala kama nchi tusije shiriki kilio cha fisadi na wazembe...acha walie wenyewe.
Mwambie hivyo marehemu Lwajabe aliyeuwawa na kutupwa porini Mkuranga.
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
31,222
2,000
Magonjwa Mtambuka mtu wangu kalike magoonjwaaaaaa uwiiiii magooooonjwa
Magonjwa Mtambuka
goaway.gif
 

CHARLES2016

JF-Expert Member
Mar 22, 2016
328
500
Sasa unafiki wake uko wapi kama alikuwa anaimba kumsifia mtu aliemshikia bunduki kichwani??

Mtu kama kashikikilia maslahi yako na unajua katili ..na kila mtu anamuimba apate nafuu why wewe usiunge tela?
Sasa Kama alimsifia kwa ajili ya tumbo lake, haoni Kama ni busara kukaa kimya leo kuliko kulamba matapishi yake?!!

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 

Mbususu Enthusiast

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,000
2,000
Katoka mbali sana hadi kutishia kuvunja ndoa ya Amina Chifupa. Imagine Mpaka njia kapita nae. Ndo sasa akaja kujituliza kwa Jakaya. Akapelekwa London kusoma,alivyo kilaza huko akafeli ndo karudi Tanzania kupewa kazi BOT na JK.
Besti JK kweli hana 1980s disease? Na kama anayo jamaa inaonekana genes zake zina response vema na minjingu
 

Boniphace Bembele Ng'wita

JF-Expert Member
Dec 25, 2013
3,249
2,000
Mnafiki mkubwa huyo mbona hakuthubutu kuyasema haya Hayati alipokuwepo ili akione cha Moto vizuri?

Kwahiyo alitaka Hayati nae ampende na hata amtongoze kama alivyotongwa na Mstaafu Mswahili wa Chalinze ambaye alimwandikia namba yake ya Simu katika Simu yake katika Hafla ya CCM Mwanza Hotel 2006 ndipo akawa nae Kimahusiano na mpaka kumpa Vyeo mbalimbali Benki Kuu, katika Taasisi nyingine na Kumpambania awe Mbunge wa Viti Maalum?

Tena angekuwa na 'Akili' angenyamaza.
mkuu umetisha.. duh kwa hyo kunawatu walipumua?? Aseee
 

Ngamanda

JF-Expert Member
Jan 9, 2019
276
250
Tanzania inataka ukatili kama miaka 50 hivi kushape jamii.....binafsi naanza harakati za kuwa Rais wa hii nchi na nitakuwa Katili kuliko huyo mnayemsema muache kudekadeka...

Hili linchi lina WAPUMBAVU wengi wanaohitaji ukatili wa hali ya juu tena miaka za 50 hivi ili wakae sawa na jamii mpya ikija iwe ya watu wasiopenda upumbavu na ukijaribu upumbavu unakufa on the spot..

Hiyo ulaya na America mnayokimbilia iliwahi kuwa ma makatili kuliko huyu mnayemuita katili ( late JPM hakuwa katili aisee aliwapenda mno anahitajika katili kuliko yeye).... huko ulaya na america viliwahi kupita vizazi katili ndio maendeleo yakaja ya kweli sio hii sugar coating..

Leo hii Ulaya na America imeendelea na makatili wote wamekabi in back face kwa kazi fulani fulani za kikatili na huko front face imewekewa wanasiasa wanaotabasamu lakini ukatili unaendelea nyuma huko....Ndio waiRaq walinyonga Saadam, Walibya wakamuua Ghadafi, huu ni ukatili wa back stage wa hao mnaowaona wanademocracy...

Bila hii nchi kuwafanyia ukatili wapumbavu na mamia kwa maelfu wakapotea na kufa haiwezi siku kuja kuendelea kwa hayo tunayoita maendeleo ya kweli....
Ni kweli kabisa! Wachina legelege zaidi ya milioni 70, warusi zaidi ya milioni 20 waliuwawa na watawala katili wakina Mao, Stalin - sasa ona nchi hizo maendeleo walio piga! Sisi tunadanganywa kusudi tusiendelee eti democracy.
 

Mbususu Enthusiast

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
6,000
2,000
Ile kulazwa ilikuwa kuua soo tu,hakuwa anaumwa wala nini,awashukuru sana kina Mama Sitta walimsitiri sana kipindi hicho.
Mama Sitta kati ya wanawake we heshima huruma na utu. Mungu amjalie huyu mama maisha marefu na afya njema. You should know you have a son who truly love you so much
 

miss pablo

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
4,160
2,000
Kesha angukia pua huko,ndiyo maana unaona makasiriko kama yote
Updates please, nimekua busy sana aisee... nawachukia mno wanawake majambazi wa mali za watoto wa marehemu. Kumbe limeshaangukia pua? halaf kwa exposure gani aliyo nayo? Watoto wa likwe wapo vzr mno upstairs. Tena watu wazima kabisaa. Mjinga kweli

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,200
2,000
Ni kweli kabisa! Wachina legelege zaidi ya milioni 70, warusi zaidi ya milioni 20 waliuwawa na watawala katili wakina Mao, Stalin - sasa ona nchi hizo maendeleo walio piga! Sisi tunadanganywa kusudi tusiendelee eti democracy.
Tatizo la ukatili wa afrika na Tanzania ni ukatili unaoangalia vyama ,yani wa chama hiki akifanya kosa linaonekana ni kosa na wachama hiki akifanya anaonekana ni shujaa . Ukatili wa Afrika unaoangalia Makabila , ukanda n.k. Kwa hali hiyo huo sio utawala wa kunyoosha ila ni utawala wa kutafuta maslahi. Ndio maana unaona watu akipewa madaraka anageuka na kupigania maslahi ya waliompa madaraka badala ya Sharia .

Dunia ya sasa ina wasomi wengi ,huwezi kuwapekeka kama ngombe eti unawatafutia maendeleo !!
Hata Tanzania tulitawaliwa kikatili na waherumani na waarabu tukatolewa kwenye Giza kuu lililokuwepo baada ya Vita ya pili ya Dunia vijana wetu wasomi walianza kuona umuhimu wa kuwa na maendeleo ya kujisimamia wenyewe kistarabu mana waliona adha ya vita katika kutafuta maendeleo.

Hata hivyo ni vyema Vyama vilivyowekwa na wakaloni Afrika vikaondolewa madarakani ili Pawe na tawala zisizojali Vyama bali nchi na maendeleo ya nchi kwa kuchagua watu wenye uchungu na nchi sio mawakala wa Wakoloni kana ilivyo hapa kwetu.
CCM ni wakala wa Wachina ambao ni Koloni jipya la dunia nzima . Na wanaanda vijana wao kuisaidia China kupora rasilimali zetu nakuwafanya vijana wa Kitanzania kuwa wachuuzi wa bidhaa toka China.

Gine wamejikomboa mpaka sasa.
Ni vigumu sana kwa kundi la Raia chini ya Chama kuleta maendeleo eti kibabe kwa kutumia majeshi wakati huo majeshi yakiwa yametelekezwa kimaslahi na wanasiasa wanaokalia madaraka kwa mgongo wa jeshi wakiwa wanajilimbikizia Mali na kuwa mabilionea kwenye nchi maskini. Eti pawe na rais Katili ,ni kujenga civil war miongoni mwa wananchi wasio na hatia ,huku wahalifu wakichanua mitaani na kulewa madaraka na fedha. Na majeshi yakitumika kama kulinda waovu.


Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom