Vicky Kamata Anastahili Pongezi! Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
vickyy.JPG
vicky kamata1.jpg
Vicky Kamata MFA2.jpg
15047962_1639214626377412_6800979244613632000_a.jpg
hqdefault (1).jpg

Wanabodi,

Siku Wabunge wa Bunge hili walipokuwa wanaapishwa mjini Dodoma, nilikuwepo, na nilipandisha uzi Huu ambapo kuhusu wabunge wa viti maalum, nilisema hivi!.

Kwa muda wote wa uhai wa bunge hili, lazima tukubali, tukatae, baadhi ya waheshimiwa wabunge wetu wa viti maalum, hawajaweza ku deliver anything worthwhile of substance Kipindi chao chote cha kuwa bungeni, hivyo naweza kuwa right, niliposema, baadhi yao, wako pale kwa kutimiza tuu huduma za kijamii za kibinaadamu!.

Miongoni mwa wabunge hawa wa viti maalum, ambao mimi niliwahesabu kama wapo wapo bungeni kutimiza mahitaji ya huduma za kijamii za kibinaadamu, ni Mhe. Vicky Kamata, kwa jinsi ilivyo Mrembo vile na Mungu amempendelea na kujaaliwa, nilimdhania mchango wake mkubwa mule bungeni ni pambo la bunge kwa kuvaa vizuri, na kupendezea kwa sana vikiwemo vikuku vya miguu yote miwili kuashiria anacheza kote kote kiasi kwanza uwepo wake, unasaidia kupunguza stress za wabunge kwa kiwango kikubwa na kwa wale wazee wasinziaji, kuwa hamasisha wasisinzie!, lakini kiukweli leo ndio nimemsikia na kumfahamu vuzuri kuliko nilivyomdhania!.

Kikubwa alichokifanya leo, ni kusimama kidete, kumvaa Zungu, uso kwa uso kumpinga kuliendesha bunge, kibabe, kwa ubaguzi, kwa uonevu na kwa double standards za hali ya juu, na kuamua kuliko kunyanyaswa, ni bora ajikalie kimya kuliko kuburuzwa!.

Hali ilikuwa hivi.

Jana Mhe. Kamata, alipeleka jina lake kuwa ni miongoni mwa wabunge, watakaochangia leo.

Leo akaangalia majina yaliyopitishwa kuchangia akajikuta yupo, muda wa kawaida kuchangia kwa mujibu wa kanuni ni dakika 10 kila mbunge. Mwenyekiti wa Bunge kikao cha leo, ni Mhe. Iddi Azan.

Uliopofika muda wake wa kuchangia, akashanga kujikuta jina lake limerukwa, na badala yake akaitwa Mhe. Hamad Rashid, ambaye jina lake kwenye walioomba kuchangia leo, halikuwepo, hivyo Mhe. Zungu, amemchomekea tuu.

Baada ya Hamad Rashid kumaliza, ndipo Vicky akaitwa na kupewa muda wa dakika 5 tuu, kuchangia!, hapa sasa ndipo nikapata fursa ya kumjua Vicky Kamata wa ukweli!, alimgomea Zungu kuwa iweje yeye, ambaye ni mchangiaji halali aliyepeleka jina toka jana, apewe dakika 5, wakati wachangiaji ambao majina yao hayapo, wamefanya kuchomekewa tuu, wapewe dakika kumi?!, Vicky akaomba apewe dakika zeke 10!. Zungu akamgomea kuwa muda umeisha, hizo dakika tano alizompa ni kumhurumia tuu ili angalau achangie, vinginevyo asubiri kuchangia kikao kijacho!. Vicky akamgomea, Zungu akamuamuru akae chini, na kumuita mchangiaji anayefuata ambaye ni Mhe. Magret Mkanga, kabla Mkanga hajaanza kuchangia, Vicky akawasha kipaza sauti na kuuliza kwa sauti ya ukali na very authoritative, Mkanga anachangia kwa dakika ngapi?!. Zungu akamjibu anyamaze, ndipo Vicky akasimama na kuwasha kipaza sauti kuongea, Zungu nae akasimama, kikanuni, Mwenyekiti akisimama, mbunge husika anapaswa kukaa chini, Viky akagoma kukaa!, ndipo Zungu akamuamuru akae chini, Vicky akamjibu kwa ukali kuwa sikai chini, sikubali, huu ni uonevu, kwa nini uchomekee wengine wachangie dakika 10, sisi wengine ndio tupewe dakika 5, na ulipomuita Mkango hukusema umempa dakika ngapi, huu ni uonevu, haiwezekani!.

Ndipo Zungu akamuamuru tena kukaa chini, na kumuamuru kama ana malalamiko yoyote, amuandikie spika malalamiko yake!, yeye anaendesha bunge kwa mujibu wa kanuni, na wote aliowaita, ameletewa majina. Ndipo Vicky akaa na kikae kikaendelea kwa waliobaki kuchangia kwa dakika tano tano!.

My Take.
Nchi yetu tumefikishwa hapa tulipo kwa sababu ya kukubali kuburuzwa, na kukosekana moyo wa udhubutu kusema hapana!, hata wakati mambo yanakwenda ndivyo sivyo, sisi na viongozi wetu, na wabunge wetu kazi yatu ni kusema tuu yes!, hewala!. Kitendo cha Vicky Kamata kusema no, alipoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo, huu ndio ndio uthubutu, unaotakiwa sasa kulikomboa taifa hili na sio kupelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe!.

Hongera Sana Vicky Kamata!.

Big Up!.

Pia Hongera kubarikiwa!.

Thanks.

Paskali
 
Mmh bora hata uyo shemeji kama wadau wanavyodai ila mtu na akili yako timamu unamchagua lukuvi kuwa mbunge? Yani mmekosa mtu anayeweza kuongoza ? Uyu jamaa ni moja kati ya wabunge mizigo yupo kimaslai zaidi kuliko umma
 
Hapa hisia zimewakilishwa vile inatakiwa....... Tumekusoma Mkuu Pasco na sisi tutaanza kumfuatilia tuone Kile ulichoona Kamanda.
 
Ndio mara ya kwanza kumsikia tokea Bungen, Hivi vitu maalumu ni hatari sana.
 
Yawezekana Zungu alipima uzito wa mchango ambao angeweza kutoa Vick Kamata dhidi ya ule unaoweza kutolewa na Hamadi Rashid, akaona Hamad amezidi sana hivyo apewe kipaumbele! (Priorities setting).
Zangu ni mtoto wa mjini, hakua tayari kuhusu mipasho toka kitu maalumu.
 
something something,WHAT?..!!!

Hao wengine wamekwenda huko kutoa huduma za kibinadamu, na kigezo kikubwa kilichofanikisha kuingia huko ni appearance yao na si vinginevyo! Hivyo utetezi wowote utakaotolewa dhidi ya hawa wa viti maalumu wasio na mchango wowote ni upuuzi tu! Wengine(kumradhi ni marehemu) tuliwashuhudia wakibishana na spika kwenye bunge la 2006 kwa mavazi waliyokuwa wamevaa! Hivyo hao(wa viti maalumu) mara nyingi huwa ni "chakura" cha wenyewe! Ova
 
Pasco wa JF wewe ni Shidaaa.... Vick ulitaka achangie nini Zaidi ya mipasho? Kifaa cha Mzee Mzima wewe kama unajipenda endelea kujipendekeza! Zungu alikuwa anamuokoa bi mdogo asibwabwaje ... ametumia ule msemo maarufu " kila mtu ana hekima mpaka aongee" ... Jafu leo amesoma taarifa nikajikuta nafunga TV maana English yake Dah!! Mungu saidia ...
image.tiff
Wanabodi,
image.tiff

Siku Wabunge wa Bunge hili walipokuwa wanaapishwa mjini Dodoma, nilikuwepo, na nilipandisha uzi Huu ambapo kuhusu wabunge wa viti maalum, nilisema hivi!.

Kwa muda wote wa uhai wa bunge hili, lazima tukubali, tukatae, baadhi ya waheshimiwa wabunge wetu wa viti maalum, hawajaweza ku deliver anything worthwhile of of substance, hivyo naweza kuwa right, niliposema, baadhi yao, wako pale kwa kutimiza tuu huduma za kijamii za kibinaadamu!.

Miongoni mwa wabunge hawa wa viti maalum, ambao mimi niliwahesabu kama wapo wapo tuu, ni Mhe. Vicky Kamata, kwa vile Mungu amempendelea na kujaaliwa, nilimdhania mchango wake mkubwa mule bungeni ni pambo la bunge kwa kuvaa vizuri, na kupendezea kwa sana, kiasi kwanza uwepo wake, unasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa wale wazee wasinziaji!, lakini kiukweli leo ndio nimemsikia na kumfahamu vuzuri kuliko nilivyomdhania!.

Kikubwa alichokifanya leo, ni kusimama kidete, kumvaa Zungu, uso kwa uso kumpinga kuliendesha bunge, kibabe, kwa ubaguzi, kwa uonevu na kwa double standards za hali ya juu, na kuamua kuliko kunyanyaswa, ni bora ajikalie kimya kuliko kuburuzwa!.

Hali ilikuwa hivi.

Jana Mhe. Kamata, alipeleka jina lake kuwa ni miongoni mwa wabunge, watakaochangia leo.

Leo akaangalia majina yaliyopitishwa kuchangia akajikuta yupo, muda wa kawaida kuchangia kwa mujibu wa kanuni ni dakika 10 kila mbunge. Mwenyekiti wa Bunge kikao cha leo, ni Mhe. Iddi Azan.

Uliopofika muda wake wa kuchangia, akashanga kujikuta jina lake limerukwa, na badala yake akaitwa Mhe. Hamad Rashid, ambaye jina lake kwenye walioomba kuchangia leo, halikuwepo, hivyo Mhe. Zungu, amemchomekea tuu.

Baada ya Hamad Rashid kumaliza, ndipo Vicky akaitwa na kupewa muda wa dakika 5 tuu, kuchangia!, hapa sasa ndipo nikapata fursa ya kumjua Vicky Kamata wa ukweli!, alimgomea Zungu kuwa iweje yeye, ambaye ni mchangiaji halali aliyepeleka jina toka jana, apewe dakika 5, wakati wachangiaji ambao majina yao hayapo, wamefanya kuchomekewa tuu, wapewe dakika kumi?!, Vicky akaomba apewe dakika zeke 10!. Zungu akamgomea kuwa muda umeisha, hizo dakika tano alizompa ni kumhurumia tuu ili angalau achangie, vinginevyo asubiri kuchangia kikao kijacho!. Vicky akamgomea, Zungu akamuamuru akae chini, na kumuita mchangiaji anayefuata ambaye ni Mhe. Magret Mkanga, kabla Mkanga hajaanza kuchangia, Vicky akawasha kipaza sauti na kuuliza kwa sauti ya ukali na very authoritative, Mkanga anachangia kwa dakika ngapi?!. Zungu akamjibu anyamaze, ndipo Vicky akasimama na kuwasha kipaza sauti kuongea, Zungu nae akasimama, kikanuni, Mwenyekiti akisimama, mbunge husika anapaswa kukaa chini, Viky akagoma kukaa!, ndipo Zungu akamuamuru akae chini, Vicky akamjibu kwa ukali kuwa sikai chini, sikubali, huu ni uonevu, kwa nini uchomekee wengine wachangie dakika 10, sisi wengine ndio tupewe dakika 5, na ulipomuita Mkango hukusema umempa dakika ngapi, huu ni uonevu, haiwezekani!.

Ndipo Zungu akamuamuru tena kukaa chini, na kumuamuru kama ana malalamiko yoyote, amuandikie spika malalamiko yake!, yeye anaendesha bunge kwa mujibu wa kanuni, na wote aliowaita, ameletewa majina. Ndipo Vicky akaa na kikae kikaendelea kwa waliobaki kuchangia kwa dakika tano tano!.

My Take.
Nchi yetu tumefikishwa hapa tulipo kwa sababu ya kukubali kuburuzwa, na kukosekana moyo wa udhubutu kusema hapana!, hata wakati mambo yanakwenda ndivyo sivyo, sisi na viongozi wetu, na wabunge wetu kazi yatu ni kusema tuu yes!, hewala!. Kitendo cha Vicky Kamata kusema no, alipoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo, huu ndio ndio uthubutu, unaotakiwa sasa kulikomboa taifa hili na sio kupelekwa pelekwa tuu kama ling'ombe!.

Hongera Sana Vicky Kamata!.

Big Up!.

Pia Hongera kubarikiwa!.

Thanks.

Pasco.
 
Back
Top Bottom