Vichwa vya habari vya Magazeti hapo tarehe 3 oktoba 2011

GeniusBrain

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,315
306
Baada ya tarehe 2 oktoba 2011 wananchi wa Igunga kupiga kura za kumchagua Mbunge wao. Kuanzia tarehe 3 oktoba 2011, vichwa mbali mbali vya habari vya magazeti vitakuwa hivi :

  • CHADEMA yapigishwa kwata Igunga
  • Mgombea Ubunge CHADEMA akataa kusaini matokeo
  • Wananchi wa Igunga wamchagua Kafumu
  • Dkt. Slaa apata ugonjwa wa moyo kwa matokeo ya Igunga
  • CHADEMA yatumia Tshs 2.5 bilioni uchaguzi wa Igunga na kuondoka patupu
  • Polisi Igunga yadhibiti vurugu za CHADEMA
  • Wananchi Igunga wakesha kusheherekea ushindi wa CCM
  • Viongozi wa CHADEMA wapoteana na kulaumiana
  • Mbunge wa CCM Igunga ajiandaa kuapishwa bungeni, ashinda kwa kishindo
  • Wananchi wa Igunga wafanya maamuzi ya busara kumrudisha Mbunge wa CCM Igunga
  • Helikopta ya CHADEMA yarudi yaondoka, mmiliki wake aidai CHADEMA Tshs 1 billion
  • Igunga kwawaka moto, viongozi wa CHADEMA waondoka kimya kimya baada yakushindwa
 
kiwango chako cha kuwaza ndipo kimefikia mwisho mkuu na hapo kitakuwa kinyume chake watakao kuwa wanalalamika ni ccm co chadema
 
kiwango chako cha kuwaza ndipo kimefikia mwisho mkuu na hapo kitakuwa kinyume chake watakao kuwa wanalalamika ni ccm co chadema

Ni ndoto kwa cdm kushinda Igunga ! mliyo wafanyia wana igunga wamesema basi .
 
Tukumbushane; hivi yule mbunge aliyeahidi kunywa sumu ni nani vile? Mbona ameacha kusisitiza ahadi yake?
 
GeniusBrain umepost hii thread muda wa saa 03:37 ambapo watu wengi wanakuwa busy na majukumu ya kujenga taifa.
Kwa ubunifu wako huo wa vichwa vya magazeti badala ya kubuni vitu vijengavyo, inaonyesha wazi kuwa wewe huenda ukawa miongoni mwa 3/4 ya watumishi (Watanzania) aliowasema Mh. Kayanda Pinda

Labda ni Mhariri wa gazeti usihukumu ili usihukumiwe.
na kama wahariri wanabuni headings za magazeti yao prior to the events, ndiyo uzembe wenyewe ...yaani kufanya kazi kwa mazoea badala ya malengo!
 
Ndio hali halisi kwani uchaguzi umeisha isha hv sasa ni formality tu

Sasa kupiga kura kuna maana na manufaa gani kama mmeshapoka ushindi? Najua uwezo wa kufanya hivyo mnao....wachezaji nyinyi....refa nyinyi.......mtangazaji nyinyi....mashabiki nyinyi.....hata mpira nyinyi !!!!!!!
 
Kafumu afumuliwa. Ccm igunga mbende mbende.kafumu amfumua mke wa mwigulu.mwanzo wa cdm kuelekea ikulu yaanzia igunga. Nape avalishwa nepi igunga
 
Ndio hali halisi kwani uchaguzi umeisha isha hv sasa ni formality tu
Watu wa CCM mnajivunia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama Watanzania wanavyojivunia Mlima Kilimanjaro. Mimi sibishi hayo kweli yaweza kuandikwa ila sitegemei uchaguzi huru mpaka nchi itakapopata Katiba mpya. Hivi unajua kwamba Katiba ingekuwa haizuii watu kuhoji wizi wa kura za Rais sasa hivi tusingekuwa na Baba Ridhiwani kama rais wa nchi maana ushahidi upo unaoonyesha uongo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 
Baada ya tarehe 2 oktoba 2011 wananchi wa Igunga kupiga kura za kumchagua Mbunge wao. Kuanzia tarehe 3 oktoba 2011, vichwa mbali mbali vya habari vya magazeti vitakuwa hivi :

  • CHADEMA yapigishwa kwata Igunga
  • Mgombea Ubunge CHADEMA akataa kusaini matokeo
  • Wananchi wa Igunga wamchagua Kafumu
  • Dkt. Slaa apata ugonjwa wa moyo kwa matokeo ya Igunga
  • CHADEMA yatumia Tshs 2.5 bilioni uchaguzi wa Igunga na kuondoka patupu
  • Polisi Igunga yadhibiti vurugu za CHADEMA
  • Wananchi Igunga wakesha kusheherekea ushindi wa CCM
  • Viongozi wa CHADEMA wapoteana na kulaumiana
  • Mbunge wa CCM Igunga ajiandaa kuapishwa bungeni, ashinda kwa kishindo
  • Wananchi wa Igunga wafanya maamuzi ya busara kumrudisha Mbunge wa CCM Igunga
  • Helikopta ya CHADEMA yarudi yaondoka, mmiliki wake aidai CHADEMA Tshs 1 billion
  • Igunga kwawaka moto, viongozi wa CHADEMA waondoka kimya kimya baada yakushindwa

Nakubaliana nawe 100%
 
Sasa kupiga kura kuna maana na manufaa gani kama mmeshapoka ushindi? Najua uwezo wa kufanya hivyo mnao....wachezaji nyinyi....refa nyinyi.......mtangazaji nyinyi....mashabiki nyinyi.....hata mpira nyinyi !!!!!!!

Mambo yameanza kuwa magumu mnaanza kuomba huruma ya watanzania, wananchi wa igunga wameisha amua cdm hawaitaki, ni bora hizo 2.5bn mngeimarisha matawi vijijini, hayo ndio mambo yakutema big g kwa karanga za kuonjeshwa
 
Ccm yaigaragaza cdm na cuf. Mgombea wa chadema azimia baada ya matokeo kutangazwa. chadema yakataa matokeo. kidume chama cha mapinduzi chafanya kweli igunga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom