Vichekesho vya TFF na Play-Offs za Daraja la Kwanza

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
29,002
10,631
Kama ilivyotarajiwa timu za daraja la kwanza, Pamba na Geita Gold zimebaki kule kule baada ya kuvuja jasho na damu ili zipande Ligi Kuu, matokeo yake ukabuniwa mtindo sijui wa wapi eti play-off na timu zilizoshuka Ligi Kuu!!!!! Mwisho wa siku zile za Ligi Kuu zimerudi huko huko badala ya kushuka. TIFUTIFU nyambavu kabisa hii.
 
Wanabomoa badala ya kujenga.....Halafu timu zote mbili ndogo zilianzia mechi zao nyumbani kwao....ulitarajia nini pale .....TFF Bure kabisa....
Kama walitaka Play off.....basi ingekuwa moja...halafu neutral ground.......hapo matekeo yangekuwa hayana utata.....
 
ina maana pamba na geita wangeenda kutia aibu
 
We nawe ndo walewale... huo ni upumbavu wa bodi ya ligi,kama ni playoff wangechukua timu 6 za mwisho zicheze ligi ndogo ili kupata timu 4 za kushuka,au wangechukua timu 4 kuanzia nafasi ya 15 mpaka 18 nu kuchezesha plyaloff wangepata mbili za kuungana na 19 na20 jumla zingekuwa 4 za kushuka.
Lkn walichifanya ni uhuni wa soka wa vilabu hv viwili vya Geita na Pamba.
ina maana pamba na geita wangeenda kutia aibu
 
Kama ilivyotarajiwa timu za daraja la kwanza, Pamba na Geita Gold zimebaki kule kule baada ya kuvuja jasho na damu ili zipande Ligi Kuu, matokeo yake ukabuniwa mtindo sijui wa wapi eti play-off na timu zilizoshuka Ligi Kuu!!!!! Mwisho wa siku zile za Ligi Kuu zimerudi huko huko badala ya kushuka. TIFUTIFU nyambavu kabisa hii.
Huu mfumo mbovu saaana
 
Hii TFF ndiyo ile iliyoimbwa na Mkoloni katika wimbo wa soka la bongo, tumeshapiga kelele sana na haya mambo ila kila awamu ya TFF ina yake mambo
 
Wanabomoa badala ya kujenga.....Halafu timu zote mbili ndogo zilianzia mechi zao nyumbani kwao....ulitarajia nini pale .....TFF Bure kabisa....
Kama walitaka Play off.....basi ingekuwa moja...halafu neutral ground.......hapo matekeo yangekuwa hayana utata.....
Sawa kabisa. Ila England play offs ni za kupanda tu toka madaraja ya chini. Aliyeshuka kashuka.
 
Kama ilivyotarajiwa timu za daraja la kwanza, Pamba na Geita Gold zimebaki kule kule baada ya kuvuja jasho na damu ili zipande Ligi Kuu, matokeo yake ukabuniwa mtindo sijui wa wapi eti play-off na timu zilizoshuka Ligi Kuu!!!!! Mwisho wa siku zile za Ligi Kuu zimerudi huko huko badala ya kushuka. TIFUTIFU nyambavu kabisa hii.
Very unfair. Timu itoke daraja la Kwanza ije kucheza playoff na timu ya TPL. Si sawa.
Zishuke nne, zipande nne. Kwisha
 
Tatizojamii forum imevamiwa na mabwege wengi wanachangia tu kwenye uzi wanavyotaka: huu utaratibu ulishapangwa muda mrefu na nchi nyingi zina mtindo huu wa play off. wakati huo mlikaa kimya wala hamkutoa maoni yoyote. ila kwa sababu imetolewa timu ya mkoani kwako ndo unakuja kulalama humu!! hivi kama hiyo pamba kwa mfano imeshindwa kwa kagera sugar ambayo ni kibonde ligi kuu unategemea ipewe nafasi ili ije icheze na simba, yanga au uzam?
 
Timu mbili za juu kwenye ligi daraja la kwanza zinapanda moja kwa moja, na Timu mbili za chini za ligi kuu zinashuka moja kwa moja.huu ndio utaratibu uliokuwepo zamani na mwaka huu umeendelezwa.
Kilichoongezeka ni kwamba tff wameongeza wigo wa timu zingine mbili (iliyoshika nafasi ya 3 na 4) za ligi daraja la kwanza kupanda ligi kama watazifunga timu za ligi kuu zilizoshika nafasi ya 3 na 4 kutoka mkiani.
Kwahiyo ukimaliza nafasi ya 1 na 2 kwenye ligi daraja la kwanza unapanda moja kwa moja ligi kuu, ila ukishika nafasi ya 3 na 4 inabidi ucheze play off kupanda
 
Shukrani chief apa nimeelewa kumbe ni sawa tu
 
Back
Top Bottom