Vicent Nyerere kutikisa Kasamwa na Katoro - Geita 05, Disemba 2012

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
0
Ndiyo Wakuu, heshima kwenu!

Baada ya Kamanda Wenje, mbunge wa Nyamagana kuitikisa Geita katika mkutano mkubwa uliofanyika katika uwanja wa magereza 1.12.2012 pamoja na mafanikio yake kama vyombo vya habari vilivyo ripoti, kesho kamanda Vicent Nyerere, mbunge wa Musoma mjini atafanya mikutano ya hadhara miwili kesho katika miji ya Kasamwa na Katoro .

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa Katibu wa CHADEMA wilaya ya Geita, ambaye pia ni Mbunge kivuli jimbo la Geita, ndugu Rogerz Mwana wa Luhega ni kuwa Kamanda Vicent ataanzia Kasamwa na jioni kumalizia katika mji wa Katoro.

Naomba kuwasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom