Vibwengo ni mizimu au jamii ya majini

Nakumbuka zamani kidogo nikiwa namsindikiza mzee mmoja Kwake akitokea kwa babu yangu tulikua tukipiga story za dizaini hii.Tulipita pahala kuna soko la jioni watu wamejazana ilikua mida ya saa mbili usiku,ndipo mzee huyu akanambia unataka kuona inavyokua nikamjibu ndio, akadai nisionyeshe hofu. Basi bana akanipakaa vijidawa flani machoni, niliona mambo ya kutisha sasa sijui ndo vibwengo, ni ķama vitoto lakini vichwa Vyao nivibabu na vibibi. Pia hapo niliona bàadhi ya wamama wakiwa uchi na Wengine wamekalia mafuvu ya vichwa vya watu. Pia baadhi walionekana kama wendawazimu. Yule mzee aliniambia umetosha nikamwambia ndio. Basi akanipakaa dawa nyingine nikaona mambo yamekua kawaida. Badala ya kuendelea kumsindikiza ilibidi yeye tena anirudishe home, tulipofika tulimkuta babu akauliza vp ameona hapo nikagundua nilikua nafunzwa kitu. Mpaka kesho maeneo haya sili wala situmii muda mwingi kuwepo. Babu alinambia nisije pakwa dawa hii tena kwani huharibu macho.
Uchawi ulikuwa unafundishwa
 
Back
Top Bottom