Elections 2010 Vibweka vya Uchaguzi Igunga: Mabasi kukamatwa, masanduku kwa DC na mengineyo..

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Chadema zimedai kuwa karatasi hizo pamoja na maboksi hayo ya kura yamehifadhiwa nyumbani kwa mkuu wa wilaya hiyo, taarifa ambazo zimekanushwa vikali na kiongozi huyo.

Chadema kimesema kuna njama za kuingiza kura bandia Igunga na kwamba tayari karatasi na masanduku ya kura yamefikishwa mjini Nzega kwa ajili ya kuingizwa Igunga siku ya uchaguzi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana majira ya saa tano asubuhi katika Kata ya Nkinga, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema Chadema kina taarifa za uhakika kwamba tayari karatasi hizo zimeshawasili wilyani Nzega.

"Ndugu waandishi mlioko katika mkutano huu, hii ni taarifa rasmi ya chama na kwamba tuna taarifa za uhakika kwamba karatasi hizo zimehifadhiwa nyumbani kwa ofisa mmoja wa Serikali," alisema Mbowe.

Aliendelea kusema kuwa tayari karatasi hizo zimeshapigwa kura na kudumbukizwa kwenye maboksi ya kupigia kura tayari kwa kuyaingiza kwenye vituo vya kupiga kura.

Mbowe alisema kuwa tayari vijana wa Chadema wameshakwenda Nzega kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha karatasi hizo haziingii Igunga.
Mbowe aliendelea kusema kuwa mpango huo wa CCM unatekelezwa kwa msaada mkubwa wa usalama wa taifa na kuonya kuwa iwapo zinaingia Igunga basi hapatakalika.

Source: Mwananchi
 
Wana-Igunga, ni jukumu letu kulinda kura zetu, kama watu wa mara, mpaka kutangazwa kule. CCM ikiiba kura tena ndani ya nchi hii basi ni bore kimoja kieleweke.
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Chadema zimedai kuwa karatasi hizo pamoja na maboksi hayo ya kura yamehifadhiwa nyumbani kwa mkuu wa wilaya hiyo, taarifa ambazo zimekanushwa vikali na kiongozi huyo.

Chadema kimesema kuna njama za kuingiza kura bandia Igunga na kwamba tayari karatasi na masanduku ya kura yamefikishwa mjini Nzega kwa ajili ya kuingizwa Igunga siku ya uchaguzi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana majira ya saa tano asubuhi katika Kata ya Nkinga, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema Chadema kina taarifa za uhakika kwamba tayari karatasi hizo zimeshawasili wilyani Nzega.

"Ndugu waandishi mlioko katika mkutano huu, hii ni taarifa rasmi ya chama na kwamba tuna taarifa za uhakika kwamba karatasi hizo zimehifadhiwa nyumbani kwa ofisa mmoja wa Serikali," alisema Mbowe.

Aliendelea kusema kuwa tayari karatasi hizo zimeshapigwa kura na kudumbukizwa kwenye maboksi ya kupigia kura tayari kwa kuyaingiza kwenye vituo vya kupiga kura.

Mbowe alisema kuwa tayari vijana wa Chadema wameshakwenda Nzega kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha karatasi hizo haziingii Igunga.
Mbowe aliendelea kusema kuwa mpango huo wa CCM unatekelezwa kwa msaada mkubwa wa usalama wa taifa na kuonya kuwa iwapo zinaingia Igunga basi hapatakalika.

Source: Mwananchi

hapo kwenye nyekundu ni kwamba taarifa za uhakika huwa hazina kawaida ya kudai bali huwa zinaeleza kwa kuwa tayari zina uhakika!

pili si mara ya kwanza kwa chadema kudai kuna kura za wizi, rejea mwaka jana kule tunduma mlipodai masanduku ya kura yameingizwa nchini kumbe vipodozi na msivyo waungwana mpaka leo mmeshindwa hata kuomba radhi wakati ile ilikuwa ni fitna ambayo ingeweza kuligawa taifa vipande, tatu, msipoanza kusema uongo kama huu hamtaonewa huruma na mengi na akina sabodo tena make wamekufadhilini magari na helkopta so mnatengeneza mazingiira ya kuwa pleased!

bye, tarehe 2 october kichapo kikali igunga
 
hapo kwenye nyekundu ni kwamba taarifa za uhakika huwa hazina kawaida ya kudai bali huwa zinaeleza kwa kuwa tayari zina uhakika! pili si mara ya kwanza kwa chadema kudai kuna kura za wizi,rejea mwaka jana kule tunduma mlipodai masanduku ya kura yameingizwa nchini kumbe vipodozi na msivyo waungwana mpaka leo mmeshindwa hata kuomba radhi wakati ile ilikuwa ni fitna ambayo ingeweza kuligawa taifa vipande,tatu,msipoanza kusema uongo kama huu hamtaonewa huruma na mengi na akina sabodo tena make wamekufadhilini magari na helkopta so mnatengeneza mazingiira ya kuwa pleased! bye,tarehe 2 october kichapo kikali igunga

panapo toka roho si mchezo lazma kuna kutapatapa,wamesha anza tayari kulalama CDM.
 
hapo kwenye nyekundu ni kwamba taarifa za uhakika huwa hazina kawaida ya kudai bali huwa zinaeleza kwa kuwa tayari zina uhakika! pili si mara ya kwanza kwa chadema kudai kuna kura za wizi,rejea mwaka jana kule tunduma mlipodai masanduku ya kura yameingizwa nchini kumbe vipodozi na msivyo waungwana mpaka leo mmeshindwa hata kuomba radhi wakati ile ilikuwa ni fitna ambayo ingeweza kuligawa taifa vipande,tatu,msipoanza kusema uongo kama huu hamtaonewa huruma na mengi na akina sabodo tena make wamekufadhilini magari na helkopta so mnatengeneza mazingiira ya kuwa pleased! bye,tarehe 2 october kichapo kikali igunga
Taarifa za Tunduma zilikuwa taarifa za ukweli. Hebu fikiria kwa nini TRA waliita polisi? TRA wanajua vitu vinavyoingizwa nchini na vinavyopaswa kutozwa kodi lakini wakati huu walilazimika kuita polisi. Ni kwa nini? Usitetee kitu usichokijua.

CCM ni criminals na wako tayari, kama mafis, kjufanya lolote kuendeleza uhalifu wao.
 
Kama hali ikiendelea hivyo kwa mambo ya kihuni namna hii nitapanda Igunga kwa gharama zangu mwenyewe kuimarisha ulinzi kwa namna yoyote ile. Kama ni kushindwa wacha CDM. Ishindwe kwa haki lakini siyo kuwaibia kura zao.
 
That's democracy African style. Honestly, our mentality towards ballot power is at best pathetic. Zambia's case is demonstratively isolated. Just dare think of all the power and resources ushered by CCM gov't for merely a constituency election and u wouldn't be dumbfumbled by ailing and poverty so engraved the country.

Probably, ballots are not the only way of changing Tz, a credible amount of sheer will and force should put in the mix.
 
Hivi kweli, inakuja akilini kweli. Ninavyojua mawakala wote wanakagua maboksi yote kabla ya watu kuanza kupiga kura. Hizo kura bandia si wataziona?

Hizi kelele zinatuchosha, wajaribu kufikirisha ubongo.
 
Kama wanajua yalipo na yanavyopangwa kutumiwa kwanini wasitumie muda kupanga kuyakamata "live"? Ingekuwa ndio ushahidi mzuri kweli hasa kwenye mazingira ya digital camera na internet.. sasa yasipotokea Jumapili tutaamini kuwa yamedhibitiwa siyo? Na kama hayakuwepo? Chadema ina mawakala kwenye kila kituo?
 
CCM kura hizo za wizi huwa wanapeleka kwenye eneo la kukusanyia masanduku hasa kwa wakurugenzi wa halmashauri,na watu wakizubaa tu kidogo karata zinachanganywa na wanatangaza kutokana na walivyo chakachua.
 
hapo kwenye nyekundu ni kwamba taarifa za uhakika huwa hazina kawaida ya kudai bali huwa zinaeleza kwa kuwa tayari zina uhakika! pili si mara ya kwanza kwa chadema kudai kuna kura za wizi,rejea mwaka jana kule tunduma mlipodai masanduku ya kura yameingizwa nchini kumbe vipodozi na msivyo waungwana mpaka leo mmeshindwa hata kuomba radhi wakati ile ilikuwa ni fitna ambayo ingeweza kuligawa taifa vipande,tatu,msipoanza kusema uongo kama huu hamtaonewa huruma na mengi na akina sabodo tena make wamekufadhilini magari na helkopta so mnatengeneza mazingiira ya kuwa pleased! bye,tarehe 2 october kichapo kikali igunga
Wewe ulitaka wakubali CCM kuwa kweli yale yalikuwa ni mabox ya kura kule Tunduma? Tuache unafiki, madai haya si ya kuyapuuza hata kidogo inawezekana yakawa na element ya ukweli kwa maana tumeshuhudia mkurugenzi wa TISS kwa mara ya kwanza akijibu tuhuma kama hizi katika uchaguzi uliopita!

Mimi naomba tusiingilie demekrasia, tuliichagua tuache ifanye kazi kwa wana Igunga kumchagua kiongozi wao wanayemtaka.
 
Haya yanawezekana,kwani asiejua ccm walivyokua wezi wa kura ni nani? Wana mbinu chafu hawa na hawajaanza leo huu wizi wanaoufanya,ngoja tusubiri.
 
CCM kura hizo za wizi huwa wanapeleka kwenye eneo la kukusanyia masanduku hasa kwa wakurugenzi wa halmashauri,na watu wakizubaa tu kidogo karata zinachanganywa na wanatangaza kutokana na walivyo chakachua.
Triki hii hutumika sana maeneo ambayo wanakubalika na hayana ulinzi wa kutosha, yaani wasimamizi wanahongwa kisha linakuja box feki linawekwa kama ndilo lililotumika kupiga kura na kwenye kujumlisha kura, wanacheza na system kwa kuongeza kura kwenye baadhi ya majimbo tofauti kwenye vituo.

Mchezo huu unahatarisha amani sana endapo wananchi kuna siku watachoka.
 
Uongo huo! nani wa kuaminika CHADEMA?
Unafafana na ule wa CDM kuingiza makomandoo 33 au ule uliokiua chama cha CUF kuwa kimeingiza mapanga na visu? CCM ni mabingwa wa propaganda, isipokuwa saizi wamekutana na barrier kubwa ya uelewa wa wananchi na kiu kubwa ya kuona mabadiliko baada ya kuichoka CCM na sera zake zisizo tekelezeka.
 
That's democracy African style. Honestly, our mentality towards ballot power is at best pathetic. Zambia's case is demonstratively isolated. Just dare think of all the power and resources ushered by CCM gov't for merely a constituency election and u wouldn't be dumbfumbled by ailing and poverty so engraved the country. Probably, ballots are not the only way of changing Tz, a credible amount of sheer will and force should put in the mix.

andika kiswahili, unatuibia mda mwingi wa kutafakari lugha yako ya kigeni. Au wewe mkenya?
 
Back
Top Bottom