Elections 2010 Vibweka vya Uchaguzi Igunga: Mabasi kukamatwa, masanduku kwa DC na mengineyo..

Kama watoto wadogo vile,ovyo sana.
Wana JF habari;

Leo asubuhi nimeamka vibaya hasa kwa kutune redio ya CCM (Uhuru FM) habari ya kwanza kusikia ni kua basi nne zenye watu waliobeba silaha kama Marungu, Panga na Bunduki madawa ya kulevya kama Bangi toka Mara zimekamatwa Tinde zikielekea Igunga kama maandalizi ya kufanya vurugu j2 kwenye uchaguzi.

Kwa mjibu wa redio CCM wanasemekana ni Vijana wa CDM waliosafirishwa kufanya vurugu hizo. Wadau mlioko maeneo husika Habari hiz ni za Ukweli? Au ni visingizio tu, manake siamini kama kweli hii ikitu inaweza kutokea, na sijui wamewajuaje kama ni watu wa CDM.

Naombeni kwa mwenye taarifa zaid atujuze!
 
hapo kwenye nyekundu ni kwamba taarifa za uhakika huwa hazina kawaida ya kudai bali huwa zinaeleza kwa kuwa tayari zina uhakika! pili si mara ya kwanza kwa chadema kudai kuna kura za wizi,rejea mwaka jana kule tunduma mlipodai masanduku ya kura yameingizwa nchini kumbe vipodozi na msivyo waungwana mpaka leo mmeshindwa hata kuomba radhi wakati ile ilikuwa ni fitna ambayo ingeweza kuligawa taifa vipande,tatu,msipoanza kusema uongo kama huu hamtaonewa huruma na mengi na akina sabodo tena make wamekufadhilini magari na helkopta so mnatengeneza mazingiira ya kuwa pleased! bye,tarehe 2 october kichapo kikali igunga
Huyo bwana yako sabodo ni kada wa c.c.m kuliko wewe lakini anakubali sera za cdm sembuse wewe chokest soda anasa! Kwee kwee kwee!! Kweli wewe pust.
 
Kama sikosei katika nchi za Magharibi kuna vyuo vinatoa shahada za Public Misinformation! Nawashauri CCM wapeleke watu wao huko kwa sababu hawana kabisa uwezo wa kutunga uongo na sisi wananchi tukadanganyika! Tinde ni mbali kidogo na Igunga, unapita kwanza Nzega ambayo ni njia panda ya kwenda Kahama na baadae Kigoma au hata Kagera, Tabora (kwa maana ya makao makuu ya mkoa) na hiyo ya kuja Igunga Singida hadi Dsm. Maswali walijuaje mabasi yalikuwa yanaenda Igunga (kama ni kweli waliyakamata) na sio kwingineko? Hao watuhuwa wako wakoje hadi waseme wanatokea Mara? Silaha walizostukia zilikuwa kwenye mabegi au mikononi au ilikuwakuwaje hadi wakawa na mashaka na hayo mabasi au ni taarifa za kiinteligensia?

Daah! yani unafikiri sana mzee!!
Kama unatoka shinyanga mjini Tinde ni juction! ukinyoosha unaelekea nzega/tabora au igunga na iwapo utakara kulia utaelekea kahama/kagera rwanda au burundi! radio uhuni wanauhakika gani kuwa walikuwa wanaelekea Igunga na si burundi au rwanda any way ni ile ukitaka kuumua mbwa mpe jina baya! wamegota ccm hizo trik zao zimeshastukiwa siku nyingi.
 
Hii redio haina tofauti na ile ya Rwanda, CCM, Vyombo vya habari na baadhi ya Wana habari iko siku watalipia vitendo vyao.
Mkuu, unajua yalianza hivihivi kule Ruanda??!!!
Hawa CCM wana akili timamu kweli?? haya mambo wanayoyapandikiza kwa watanzania ni kwa gharama za nani??
 
hawa na redio yao tuwaeleweje?
si wameenda kuwaomba CDM kufanya kampeni za kiungwana?
hata kama wamekata gari la namna hiyo, haitoshi kutoa taarifa kituoni na kuwaachia vyombo vya dola kama vipo vifanye uchunguzi kisha vitoe taarifa?
N je ikibainika walikodiwa na CCM tuwaelewe vipi na huku wameshawachafua CDM?

Kama uyazungumzayo ni ya kweli, kuna ulazima wa kuwauwa CCM wote tuanze upya

Mkuu Ntamaholo una hasira sana na hawa Magamba: any way usijali mkuu Mungu yupo nasi wapenda mabadiliko
 
Angalau tungejaribu kuutafuta ukweli wake halafu tungejadili kwa ukweli wake au uongo wake. Tatizo hapa ni kwamba nature, mazingira na source ya habari haviaminiki. Na mkishamfahamu mtu kuwa ni mwongo, hata akisema ukweli, hamuwezi kuamini!

kweli kabisa.
 
Wana JF habari;

Leo asubuhi nimeamka vibaya hasa kwa kutune redio ya CCM (Uhuru FM) habari ya kwanza kusikia ni kua basi nne zenye watu waliobeba silaha kama Marungu, Panga na Bunduki madawa ya kulevya kama Bangi toka Mara zimekamatwa Tinde zikielekea Igunga kama maandalizi ya kufanya vurugu j2 kwenye uchaguzi.

Kwa mjibu wa redio CCM wanasemekana ni Vijana wa CDM waliosafirishwa kufanya vurugu hizo. Wadau mlioko maeneo husika Habari hiz ni za Ukweli? Au ni visingizio tu, manake siamini kama kweli hii ikitu inaweza kutokea, na sijui wamewajuaje kama ni watu wa CDM.

Naombeni kwa mwenye taarifa zaid atujuze!

Unategemea nini kama ndio hiyo radio, Ni uongo tu huo. Labda ni hao hao watu wa kijani ndio wanafanya hivyo. Bora ungelala kuboresha afya yako kuliko kusikiliza hiyo radio.
 
Kama ingekuwa ni kweli CCM wasingekaa kimya bila kuitisha mkutano wa waandishi wa habari kwani hiyo ingekuwa turufu yao kubwa kwa ushindi wa Igunga. Jambo baya lolote la CDM polisi wangelitangaza haraka sana, so far huo ni uzushi na upuuzi tu.
 
Kuna kila sababu ya kutokuwa na wasiwasi na madai ya Mbowe. Kitendo cha jimbo la Igunga kuhamia Chadema CCM wanakitafsiri kama bonge la pigo kwao, aibu kubwa, na alama ya kudhoofika kwa chama chao kwamba inawezekana hali ikawa mbaya zaidi 2015.

Kwa kuzingatia hilo hawataki kufanya bahati nasibu ya uchaguzi halali kupitia ushindani halali. Na wapo tayari kuua kuhakisha Mbunge anatoka CCM. Niia ya kuiba kura wanayo, uwezo wa kuiba kura wanao na sababu za kuiba kura wanazo. Kwa upande wa Chadema, jukumu lao ni moja tu nalo ni kumpinga adui kwa kila namna. Vijana wa Chadema wako Nzega tayari kufatilia hayo masanduku ya kura.

Na kama Mbowe alivyosema..."wana Igunga wasiwe na wasiwasi hakuna kura ya mtu itakayoibiwa, tumejipanga kisawasawa, tutapambana nao mpaka kieleweke."
 
Back
Top Bottom