Elections 2010 Vibweka vya Uchaguzi Igunga: Mabasi kukamatwa, masanduku kwa DC na mengineyo..

Kilichonisutua zaidi ni kusikia jinsi yule reporter wao aliyekua ameunganishwa live toka Tinde akitoa karipio kwa viongoz wa CDM. Sijui yeye amethibitisha vp tukio hilo had atoe karipio direct kwa CDM.

Tukio litakua la kweli lakini walioanda njama hizo ndo bado ni kitendawili. Kwani kelele na vurugu zilikua zinasikika live redion, maaskari kadhaa wamemwagwa huko.

Watuhumiwa naskia ni mchanganyiko Mabinti na Vijana wa kiume,maaskari waliokuwepo mapema asbh walikuwa wakiuume kitu kilichowafanya washindwe kuwakagua watuhumiwa wa kike!.

Sasa maswali ya kujiuuliza wamejuaje kwamba wamtoka Mara? Kama hawajawaanda wao wenyewe?.
Siasa nimekubali ni mchezo mchafu,ukiweza kumchafua mwenzako ndo mafanikio yako.
 
Nadhani hawa watu wataenda Jera tu, Hebu tukumbushane ule mwaka wamekamata makontena ya visu vya Cuf kwa ajiri ya kuvunja amani kesi yao iliishaje vile?

heheheeee. Aisee ile kesi sikumbuki iliishaje. Mi naona wanadanganya tu. Hiyo redio ni mali ya CCM
 
Uongo huo! nani wa kuaminika CHADEMA?
Kama nyie mnaendelea kuweka nta kwenye masikio yenu, shauri yenu. Mimi sitaki kuja kuanguka presha siku hiyo, nimeshaanda mavazi ya kuomboleza Msiba wa Livingstone Lusinde tarehe 3 October 2011.

Nimeshakodisha na waliaji. Pole na Ban, ukijifunza kuongea kistaarab kama sie utaziepuka hizi ban za mara kwa mara.
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Chadema zimedai kuwa karatasi hizo pamoja na maboksi hayo ya kura yamehifadhiwa nyumbani kwa mkuu wa wilaya hiyo, taarifa ambazo zimekanushwa vikali na kiongozi huyo.

Chadema kimesema kuna njama za kuingiza kura bandia Igunga na kwamba tayari karatasi na masanduku ya kura yamefikishwa mjini Nzega kwa ajili ya kuingizwa Igunga siku ya uchaguzi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana majira ya saa tano asubuhi katika Kata ya Nkinga, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema Chadema kina taarifa za uhakika kwamba tayari karatasi hizo zimeshawasili wilyani Nzega.

Ndugu waandishi mlioko katika mkutano huu, hii ni taarifa rasmi ya chama na kwamba tuna taarifa za uhakika kwamba karatasi hizo zimehifadhiwa nyumbani kwa ofisa mmoja wa Serikali, alisema Mbowe.

Aliendelea kusema kuwa tayari karatasi hizo zimeshapigwa kura na kudumbukizwa kwenye maboksi ya kupigia kura tayari kwa kuyaingiza kwenye vituo vya kupiga kura.

Mbowe alisema kuwa tayari vijana wa Chadema wameshakwenda Nzega kuimarisha ulinzi ili kuhakikisha karatasi hizo haziingii Igunga.
Mbowe aliendelea kusema kuwa mpango huo wa CCM unatekelezwa kwa msaada mkubwa wa usalama wa taifa na kuonya kuwa iwapo zinaingia Igunga basi hapatakalika.

Source: Mwananchi

Ww Mbowe acha kutapatapa km kuku aliyechinjwa na akaachwa. Huko ni kujionyesha wazi hujiamini km ni kiongozi, na kama serikali ikiamua kuziingiza hizo kura Igunga huna ubavu wa kuzizuia , usifanye mchezo na dola inawza fanya kitu muda na saa yoyote.

Yaonyesha wazi kabisa mmeisha shindwa igunga hivyo ni visingizo tu
 
Huwa napenda kuitafakari habari kwa mapana yake lakini ni kupoteza muda kujadili habari ya namna hii tena kutoka radio uhuru!
Ninachoweza kuchangia hapa ni huruma ninayoipata kwa wafanyakazi wa hiyo redio. Wanalazimika kutunga au kuigeuza story ya kweli kwasababu ya chama, kinyume kabisa na walichofundishwa shuleni.

Nawaonea huruma sana maana licha ya kuufahamu au kuushuhudia ukweli bado hawawezi kuusema. Ni kinyume na katiba lakini hawawezi kutetea haki yao. Inawezekana hawapendi lakini njaa inawauma sana, wataenda wapi? Wako katika hali mbaya, tena kandamizi!

Kama tunaweza kuwasaidia ni vema tukawasaidia ndugu zetu hawa. Tunaweza tukaanza na Mwita25, tbc, polepole hadi redio uhuru!
 
Masanduku hayo yanaweza kuingizwa usiku huko Igunga kwa kutumia magari ya Mawaziri, kama Wassira, Magufuri, Vuai pia usalama wa Taifa. Chadema kuweni makini, hakuna kuogopa mtu hata ikitulazimu kufa tuko tayari.
 
Mara ya mwisho kusikiliza redio Uhuni ni siku ile walipokanusha kuwa JK anasingiziwa eti kanunuliwa Suti 5 na Mwarabu wakati ukweli ni kwamba alimnunulia Msuli mmoja tu! Baasi nikazima redio nikaenda kulala.
 
Kama sikosei katika nchi za Magharibi kuna vyuo vinatoa shahada za Public Misinformation! Nawashauri CCM wapeleke watu wao huko kwa sababu hawana kabisa uwezo wa kutunga uongo na sisi wananchi tukadanganyika!

Tinde ni mbali kidogo na Igunga, unapita kwanza Nzega ambayo ni njia panda ya kwenda Kahama na baadae Kigoma au hata Kagera, Tabora (kwa maana ya makao makuu ya mkoa) na hiyo ya kuja Igunga Singida hadi Dsm.

Maswali walijuaje mabasi yalikuwa yanaenda Igunga (kama ni kweli waliyakamata) na sio kwingineko? Hao watuhuwa wako wakoje hadi waseme wanatokea Mara? Silaha walizostukia zilikuwa kwenye mabegi au mikononi au ilikuwakuwaje hadi wakawa na mashaka na hayo mabasi au ni taarifa za kiinteligensia?
 
Aaah!!Kumbe ni Uhuru fm,mi nilisha acha siku nyingi kusikiliza hiyo redio,ku watch TBC1 na kusoma Uhuru,Mzalendo,Daily News,Habari leo etc
 
Tunataka tuone watu hao wanafikishwa mahakamani mara moja na picha zao tuzione kama wale watu wa samaki wa Magufuli walivyokuwa wanaonyeshwa, la sivyo Magamba waombe msamaha kwa Watanzania kwa kuendelea kuwafanya wajinga na kuwaletea uongo wa kitoto. Hawa jamaa wamezoea sasa kutuletea habari za kwenye magazeti wanayosoma ya Udaku na kuzileta kutaka sisi great thinkers tuzisadiki.

welcome back mkuu amiliki..
 
Mara ya mwisho kusikiliza redio Uhuni ni siku ile walipokanusha kuwa JK anasingiziwa eti kanunuliwa Suti 5 na Mwarabu wakati ukweli ni kwamba alimnunulia Msuli mmoja tu! Baasi nikazima redio nikaenda kulala.

wako bize kumsafisha mtu ambaye kajichafua mwenyewe..
 
Wakuu, hivi hiyo habari ingekuwa imetolewa na MwanaHalisi mngesemaje?
 
Propaganda za ccm tushazizoea, hawana lolote.... wananchi wa igunga wamekunywa maziwa ya kutosha toka kwa CDM, nyie CCM hata mlete sumu ya aina gani ni kama mnajisumbua.. poleni!
 
Masanduku hayo yanaweza kuingizwa usiku huko Igunga kwa kutumia magari ya Mawaziri, kama Wassira, Magufuri, Vuai pia usalama wa Taifa. Chadema kuweni makini, hakuna kuogopa mtu hata ikitulazimu kufa tuko tayari.

Ww kweli upo tayari kufa ? pambana kwanza kuikoa familia yako ambayo iko hali mbaya na kutaabika !
 
Propaganda za jamaa wa magamba hizo.
Hawakawii kusema Obama anaisadia CHADEMA ishinde Igunga



Hah hah ha haha! Umenifurahisha sana Mkuu! Walishasema kwamba cdm inafadhiliwa na nchi za ulaya kufanya maandamano! Membe akawaita mabalozi akaongea nao kumbe ilikuwa propaganda tu!

Ccm wanaweza kusema kitu chochote na mahali popote bila kufikiria athari zake kwakuwa wanatumia masaburi kufikiri!
 
Back
Top Bottom