Vicenza
JF-Expert Member
- Oct 5, 2019
- 969
- 1,464
Wema unaponza ,Kuna watu ukiwasaidia ni kama unatafuta matatizo, ni Bora mtu akuone wa mbuzi kuliko kuwa social mwishowe muonane wabaya.kuna watu wana tembea na mikosi..ya ukoo.Nakumbuka zamani kidogo nilipanga chumba na sebule uswahilini vyumba vya uani. Mama mwenye nyumba alikuwa na mtoto wa dada yake wa kike anaishi naye. Huyu mtoto wa dada yake alikuwa na mtoto mdogo. Kwa sababu ya ubusy nikawa nampa hela yule dada anifulie nguo na hii ilimsaidia angalau kupata kipato. Mara nikirudi kutoka kwenye mizunguko yule dada alikuwa anakuja kwangu tunapiga story baadaye anaondoka. Sikuwahi hata kidogo kumtamani wala kuwaza kulala naye. Kipindi kile mdada mwenye mtoto mdogo hata anipe bure nilikuwa siwezi.
Siku moja rafiki yangu mmoja mwenye mazoea na yule mama akaja kuniambia mama mwenye nyumba anasema umempa mimba mtoto wa dadake. Dah! nikamuuliza yule rafiki yangu, yule mama nakaa naye nyumba moja kwanini asiniambie akuambie wewe? nikaona isiwe tabu. Asubuhi yake nikamvaa yule mama. Nikamwambia nasikia taarifa nimempa ujauzito mwanao? yule mama akasema afadhali umekuja. Yule mdada akaitwa. Nikamuuliza mbele ya mama. Nasikia nimekupa ujauzito? yule dada akaruka 'mimi ? nani kasema? mi hujanipa ujauzito'
Kabla ya hapo kama wiki moja hivi iliyopita yule mdada alikuwa ameniambia ana mazungumzo na mimi ila mambo yangu kifedha yalikuwa sio mazuri. Nilijua anataka hela. Kwa hivyo nikampotezea. Nikamwambia kuna sehemu nawahi nikirudi basi tutaongea. Hapo ndipo nikaunganisha dots. Kumbe labda siku ile alikuwa anahitaji msaada wangu kuhusu ujauzito.
Story ndefu ila siku mbili baada ya kumwuliza yule dada kama nina ujauzito wake mbele ya mama yake. Jioni wakati nimerudi nikakuta hirizi mlangoni kwangu. Nikaikota hiyo hirizi nikaifungua ndani kuna karatasi ina maandishi mekundu ya kiarabu na kucha. Baadaye nikampelekea mchungaji wangu tukaichoma moto.
Nilikuja kuhama ile nyumba na nasikia mtoto alizaliwa na akapewa jina langu. Sikuwahi kufatilia kwa sababu hata chuchu za huyo dada achilia mbali papuchi sikuwahi kushika. Maisha ya kupanga bwana.