Viboko mashuleni: Gili Sekondari ya Kibaha yawatibua wazazi

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,108
37,644
Habari za Pasaka wapendwa.

Shule ya Secondary Gili (wasichana) iliyopo Kibaha, Loliondo imeingia kwenye sintofahamu baada ya Wazazi wa Wasichana wanaosoma hapo kucharuka dhidi kukithiri kwa vichapo.

Kwenye kikao cha leo cha Wazazi na Uongozi wa Shule wakiwemo walimu, wazazi wamecharuka kiasi agenda kuu ya mkuutano ikawa uchapaji uliokithiri. Wapo wazazi waliosema watoto wamejeruhiwa ikiwemo kuvunjwa kwa vidole. Mzazi wa bint X wa kidato cha 4 yeye aligundua bint yake ana majeruhi ya mkono baada ya bint kushindwa kushika mwiko wa kupikia huko nyumbani.

Mzazi mwengine alimwambia shuhuda mm wa JF kuwa bint yake kidole kimoja kimekufa ganzi. Kisa ni fimbo za shuleni.

Shuhuda huyu wa JF ambaye halipwi zaidi ya kiherehere tu aliwaskia mabint wa kidato cha 4 walokaa kikundi wakihamasishana kuwasihi wazazi wao wasiwarudishe shuleni hapo kwa Masomo ya FORM 5 2022!

Shuhuda huyu alishuhudia Mama Mmoja alievalia suruali nyeusi ya kitambaa na blauzi yenye madoa meusi akiwa ktk foleni ya kumuona Headmistress hoja ikiwa bint kuchapwa kiasi cha kuvimba mkono.

Leo ilikuwa visiting day ya wazazi ya F4 na F2. Jana ilikuwa visiting day ya F6 shuleni GILI SECONDARY.
 
Wazazi wamewaachia kazi ya kulea kushauri kufundisha na kuwakuza kimaadili watoto wao halafu hawataki wachapwe? Mzazi hajishughulishi na mwanae toto lina develop tabia mbaya likinyooshwa mzazi analalama wakiachwa mwisho wa siku ziro za kutosha zigo looote kwa mwalimu.

Poleni walimu
 
Shule nilienda sikumoja wale wanafunzi niliogopa kama kuku wa mayai wanafunzi wanene miili imekaa kimayai mguu mnene umekatika nikasema hapa hawa wanafunzi hawataniheahimu mwanafunzi mwili ×2 yangu.

Ninahisi viboko vyakawaida ila miili ya wanafunzi mayai sana.
 
Kuna walakini kwa walimu au Mwalimu Mkuu.

Haiwezekani wanafunzi wote wakafanana tabia na wakawa na malalamiko yanayofanana.

Njia ni moja, ondoa Mkuu wa shule, ondoa mwalimu wa nidhamu, unda tume ya uchunguzi.
 
Walimu wa boarding bwana kuna siku ticha alituchapa Dom zima kisa ugomvi na Dom lingine.

Miye nilikuwa nimelala zangu hata walivyoitwa sikuwa na habari.

Wananiamsha nakutana na fimbo nilimind mpk ticha aliona aibu baada ya adhabu yake.
 
Kuna walakini kwa walimu au Mwalimu Mkuu.

Haiwezekani wanafunzi wote wakafanana tabia na wakawa na malalamiko yanayofanana.

Njia ni moja, ondoa Mkuu wa shule, ondoa mwalimu wa nidhamu, unda tume ya uchunguzi.
Ungekuwa wewe ni mwalimu sidhani kama ungesema haya. Walimu wanateseka sana kuwajenga watoto. Wanafunzi ni watu wa lawama hata uwape pipi. Ukiwa mpole utasikia mwalimu fulani poyoyo kweli na kazi zake hawafanyi kwa makini. Ukiwashupalia utasikia limwalimu lile likali kweli. Mwalimu afanyaje?
 
Mwalimu anayejielewa hachapi viboko. Na nchi hii elimu bora inapatikana kwenye shule ambazo hawachapi. Hizo wanachapa ni utopolo mtupu.
 
Mwalimu anayejielewa hachapi viboko. Na nchi hii elimu bora inapatikana kwenye shule ambazo hawachapi. Hizo wanachapa ni utopolo mtupu.
Unaongea ujinga gani hapa.
Wewe siyo mwalimu hujakaa na watoto kwa hiyo kaa kimya.
 
Back
Top Bottom