Viboko majumbani na mashuleni,ni suluhisho la utovu wa nidhamu uliokithiri wa watoto? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viboko majumbani na mashuleni,ni suluhisho la utovu wa nidhamu uliokithiri wa watoto?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Feb 20, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Viboko ilikuwa sehemu ya maisha yangu nilipokuwa shuleni au nyumbani.Adhabu hii wala sikuichukia, ingawa nilipochapwa niliumia.Hata hivyo mara nyingi nilipochapwa iwe shuleni au nyumbani nili azimia kuto rudia kosa lilonifanya nichapwe.Hali hii ilinifanya hatimaye niwe na tabia nzuri na niwe kama nilivyo leo.

  Kwa watu wengi wenye umri kama wangu,watakubaliana na mimi kwamba viboko ni njia nzuri ya kumuelekeza mtoto na kumumbia tabia njema.Nakumbuka nyakati zile nzuri ambapo mtoto alikuwa analelewa na kila mtu.Leo mtoto ni wa baba na mama tu, mtu mwingine hahusiki kabisa.Kuta mtoto wa mtu anafanya ovu fulani, halafu umchape kiboko,varangati lake hapatakalika!Lakini hasa kilichotusibu ni nini mpaka tukaacha msimamo ule mzuri tulio kuwa nao,kwamba kiboko hurekebisha tabia mbaya?

  Sio siri kwamba tumeingiziwa kwa siri mawazo haya potofu na nchi za magharibi,na sisi kwa upumbavu wetu,tena kinyume kabisa na utamaduni wetu,tumeyakubali.Katika kitabu cha Mithali22:15,Agano la kale, tunasoma maneno haya:"Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali." Maneno haya maana yake ni kwamba, asiyemchapa mwanae anamfanya awe mjinga,kwa vile hatma ya kutomchapa ni kubaki na ujinga wake.Maandiko mengine ya Biblia pia katika kitabu cha Mithali 23:13 yanasema "Usimnyime mtoto wako mapigo,maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa." Katika kitabu hicho hicho cha Mithali(23:14) pia tunasoma maandiko haya "utampiga mtoto kwa fimbo na kumuokoa nafsi yake na kuzimu."Katika maandiko yote haya Mungu anasisitiza umuhimu wa adhabu ya fimbo kwa mtoto.Yeye anajua kwamba fimbo kwa mtoto ni lazima.

  Sasa mawazo haya yanayopingana na Mungu mwenyewe, kwamba mtoto asipigwe, yanatoka wapi?Sisi wanadamu ni nani hata kupingana na Mungu?Jibu ni rahisi,anayempinga Mungu anashirikiana na shetani,kwa hiyo mafundisho haya yanatoka kwa shetani mwenyewe!Sasa kwa kubali maagizo na mafundisho ya mashetani,tunadhani Tanzania itakwepa ghadhabu ya Mungu?Jibu ni hapana.Kwanza tunaona wazi kwamba tayari Mungu ameshaishushia Tanzania ghadhabu yake.Sina haja ya kusema kwa vipi,kwa sababu kila mtu ana masikio na macho.Tugeuke basi ili Mungu atuhurumie.

  Mwisho niseme kwamba Watanzania hatuko waangalifu na makini katika kuiga mambo mbalimbali tunayoletewa na matapeli ya nchi za magharibi,likiwa na hili la kutowachapa watoto viboko.Sasa wenzetu Uingereza wameruhusu ngono ifundishwe mashuleni,tutaiga?Katika ujinga wetu, si ajabu tukaiga,tusubiri tuone.Yametutapeli katika kila jambo, hata mpaka kwenye kulea watoto wetu!No,tunapashwa kuwa more diagnostic!
   
  Last edited: Feb 21, 2009
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Jibu ni HAPANA..Viboko si solution, Watumwa na manamba walimwe vioboko na sisi tuwafunze watoto wetu the same? Adhabu ziwepo lakini viboko kwa maoni yangu si solution...Na havimfunzi mtoto, hata jamii za mataifa yaliyoendelea hayaku rely kwenye mboko tuu.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mboko muhimu haswa kwa wezi wa mali ya Taifa, wabadhirifu na mafisadi!

  Sasa tunabembelezana ili iweje?

  Eti haki za binadamu..je haki hizo wakuu..wakati wajanja wanapeta? Unajua adhabu ingekuwa kubwa watu hata wangeogopa..sasa kila mtu anaiba..kwa kuwa sheria tulizoiga ni dhaifu kuwawajibisha wezi!

  Kwa wanafunzi..mimi nadhani mboko zirudishwe tu..haya mambo ya kuiga ulaya eti kisingizio human rights!

  Sasa mbona zamani heshima ilikuwa kubwa kuliko leo?

  Hamna kitu mbaya kama kuiga kila kitu!
   
Loading...