Viboko 12 vyamsubiri Dk. Loius Shika, 'bilionea' nyumba za Said Lugumi


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,654
Likes
51,721
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,654 51,721 280
7b86a1a4b5222241060f8de03781f8c9.jpgSiku moja baada ya Jeshi la Polisi kumwachia kwa dhamana, Dk. Luois Shika ambaye alikuwa ameshikiliwa kwa siku sita kwa madai ya kuharibu mnada wa nyumba za Said Lugumi, familia ya daktari huyo imesema lazima achapwe viboko 12 kama anataka kusamehewa.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake katika Kitongoji cha Misheni katika kijiji cha Chamugasa juzi, Kaka mkubwa wa Dk. Shika, Pelanya Lunyalula alieleza kuwa mila na tamaduni za kabila la Wasukuma hazitoi msamaha hivi hivi pale kikao cha baraza la ndugu kitakapoketi na kumpa adhabu ya viboko.

"Mpaga ibanza Iya badugu (hadi kwenye kikao cha baraza la ndugu wa ukoo) wakiketi kumjadili na yeye akiwepo ndipo uamuzi hufanyika wa kumuonya kwa tabia kudharau ukoo na huchapwa viboko zaidi ya 12 na kutakiwa kujirekebisha vinginevyo atafutwa kabisa", alisema.

Lunyalula alisema uamuzi huo hufanywa endapo mtu kama huyo ameamua kutengana na ndugu zake kama anavyodaiwa kufanya Dk. Shika kwa madai misiba mingi imetokea na yeye kupatiwa taarifa lakini hakufika kuhani.

"Hii ni dhahiri kwamba ameona ndugu zake hawaendani na elimu yake kitendo ambacho kila mmoja alishakichukia, hivyo hata hilo suala lililomkuta huenda ni malipo ya matendo yake aliyoyafanya", alisema Pelanya mwenye umri wa miaka 84.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mpwa wa Dk. Shika ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Misheni, Emmanuel Komanya ambaye nafasi hiyo kuwaonya watu wengine wasiige tabia kama hiyo.

Ndugu hao ambao kwa pamoja walionekana kuwa na huzuni wakati wakizungumza na Mwananchi baada ya kupata taarifa kushikiliwa kwake, walisema hawataweza kwenda kuonana naye.

"Kwanza familia yetu ni masikini hatuna uwezo wa kutafuta fedha za kwenda huko, lakini pia hata kama tungekuwa na uwezo tusingeweza kwenda (Dar es salaam)", alisema.

Hata hivyo, Dk Shika mwenyewe alipozungumza kuhusu familia yake hiyo alisema hawasiliani nayo kwa kuwa huenda wenzake hawana simu na hadhani kama atakwenda huko kwa kuwa wazazi wake wote wameshakufa hivyo hata akienda haitasaidia.

Juzi Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam lilifikia uamuzi wa kumwachia baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kujidhamini mwenyewe kutokana na kukosa mtu wa kumwekea dhamana.

Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema, "Uchunguzi wa tuhuma dhidi yake unaendelea lakini mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyefika kutaka kumwekea dhamana, yaani anaishi kama mtu wa nyikani".

Chanzo: Mwananchi
 
E

eddy

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2007
Messages
10,748
Likes
4,615
Points
280
E

eddy

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2007
10,748 4,615 280
Masha kajiongeza angekula mboko
 
Mhadzabe

Mhadzabe

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2009
Messages
2,425
Likes
2,139
Points
280
Mhadzabe

Mhadzabe

JF-Expert Member
Joined May 20, 2009
2,425 2,139 280
Mijitu mingine hovyo kabisa, wamchape kawakosea nini?....Yani yakotokea maswala kama haya ndio wanaojiita ndugu huibuka na kutapika uhoro wao. Dr. ni smart sana. Wangesililiza au kuona clip ya video kwa AYYO TV akijibu shutuma za kushindwa nadhani wangekuwa kimya.
 
Jamalm335

Jamalm335

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Messages
2,247
Likes
3,969
Points
280
Jamalm335

Jamalm335

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2015
2,247 3,969 280
Ama kweli hakuna anaejua kesho yake. Yani siku chache tu zilizopita hakuna aliyekuwa anamjua Dr. Shika, leo amekuwa maarufu kiasi cha kufuatiliwa chimbuko la familia yake.
 
Liwagu

Liwagu

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2017
Messages
1,535
Likes
1,188
Points
280
Age
40
Liwagu

Liwagu

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2017
1,535 1,188 280
Wampime kwanza afya siokumchapatu.

Wampime then wamchape kulingana na afyayake itapendeza.
 
Mr Miller

Mr Miller

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
10,415
Likes
22,593
Points
280
Mr Miller

Mr Miller

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
10,415 22,593 280
hao ndugu nao akili kichwani hamna, karne hii ya kuchapana viboko tena mtu mzimaa!!!!

wamfute tuu kwenye huo ukoo wao...undugu sio lazima damu moja, waTZ wapo wenye mioyo safi. wamuache tu.
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,654
Likes
51,721
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,654 51,721 280
hao ndugu nao akili kichwani hamna, karne hii ya kuchapana viboko tena mtu mzimaa!!!!

wamfute tuu kwenye huo ukoo wao...undugu sio lazima damu moja, waTZ wapo wenye mioyo safi. wamuache tu.
Inashangaza sana. Kuona kuwa kumbe watu bado wanaishi enzi za TANU
 
chibalangunamchezo

chibalangunamchezo

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Messages
1,525
Likes
2,586
Points
280
chibalangunamchezo

chibalangunamchezo

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2017
1,525 2,586 280
Mmmh, wamhurumie tu dokta
 
aggyjay

aggyjay

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2015
Messages
3,938
Likes
6,158
Points
280
aggyjay

aggyjay

JF-Expert Member
Joined Feb 16, 2015
3,938 6,158 280
msiongee sana kuhusu huyu baba..mda urasema wenyewe.

je mkija kugundua ni kweli alikuwa na kampuni urusi akadhurumiwa mabilioni yake mtasemaje?
mi nahisi mateso na kutekwa kumemwaribu saikolojia yake..but alipewa ushirikiano atakua sawa.
 

Forum statistics

Threads 1,235,907
Members 474,863
Posts 29,240,062